Tafuta

Mary (infermiera) e Peter Lochoro (Cuamm) nel centro di salute di Siripi, Rhino Camp.JPG

Sudan Kusini:Vijana wajiandaa na sikukuu ya Don Bosco,Jimboni Tombra-Yambio

Askofu wa Jimbo la Tombura-Yambio anawaalika vijana kujikita katika njia ya Don Bosco."Mnakabiliwa na changamoto na shida za kijamii na kiuchumi?Kwa hiyo ninataka kuona mipango yenu binafsi,mapendekezo yenu ili kuvishughulikia”.Ni katika muktadha wa kuelekea katika siku kuu ya Mtakatifu Don Bosco,Mtatifu wa vijana ambapo jimbo hilo lintafakari zaidi juu ya shida ya vijana kwa mwaka 2021.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Changamoto za vijana zitakuwa ndiyo kiongozi katika sherehe zinazo andaliwa na Jimbo katoliki la Tombura-Yambio, nchini Sudani Kusini, kwenye tukio la ukumbusho wa kiliturujia wa Mtakatifu John Bosco, ifanyikayo kila mwaka tarehe 31 Januari. Don Bosco alikuwa mfano halisi wa kikuhani kwa vijana ambao aliwapatia suluhisho halisi kwa shida zao. Mwaka wa 2021 katika Jimbo hilo limejikita katika mada ya kazi. Kwa maana hiyo, “sikukuu ya Don Bosco kwa vijana, ambao wanapata changamoto nyingi katika ulimwengu wa ajira, inamaanisha kuwapa maoni na tafakari”. Amesema hayo Askofu Eduardo Hiiboro Kussala wa Jimbo hilo kwa kuwaalikwa vijana kujiandaa na siku kuu hiyo. Akiendelea kueleza Askofu amesema Mtakatifu huyo ndiye mtakatifu mlinzi wa suluhisho kwa mambo magumu, kwa sababu alijitoa wakati wake na maisha yake kusaidia na ili kuokoa vijana ambao walikuwa na shida, bila mategemeo yoyote yale.

Akiwageukia vijana moja kwa moja, Askofu Kussala amewahimiza kubuni mipango yao binafsi itakayofanyika kwa mwaka 2021 kwamba: “Vijana wapendwa wa Tombura Yambio mwaka huu lazima uchukue njia ya Don Bosco: unakabiliwa na changamoto za kijamii na shida na nafuu? Kwa hivyo ninataka kuona mipango yenu, kumbukumbu zenu ili kukabiliana nazo”. Kwa sababu hiyo, askofu amewalika kila kijana kuchagua, mnamo Januari 31, malengo matatu binafsi ili yaweze kutumizwa mwishoni mwa mwaka wa 2021. “Nataka kila mmoja wenu aangalie changamoto ambazo mnazo nyumbani au parokia na mjitoe kwa chanamoto hizo katika mwaka. Malengo yaliyotambuliwa na suluhisho zinazowezekana basi zitawasilishwa kwa jumuiya ya jimbo. “Lazima kuomba na jimbo lote kukaa karibu na nanyi katika kutafuta suluhisho la shida zenu,” amependekeza kwa vijana hao, Askofu Kussala ambaye baadaye anawaahidi kuwa: “Nitakuwa nanyi kwa asilimia mia moja, kwa chochote mtakacho chagua na kufanya katika mwaka huu 202.”

Kwa upande wa maisha ya Mtakatifu John Bosco alizaliwa mnamo tarehe 16 Agosti 1815 huko Asti mkoa wa Piemonte nchini Italia na kifo chake mnamo tarehe 31 Januari 1888. Alikuwa Padre na mwanzilishi wa Shirika la Mtakatifu Fransisko wa Sales ambao wanajulikana kama ‘Wasalesiani’ pia alikuwa mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mtakatifu Francis wa Assisi na mwanzilishi na mtawa wingine wa kike wa Shirika la mabinti wa Maria Msaada wa Wakristo. Alitangazwa mwenyeheri mnamo 1929 na kutangazwa mtakatifu mnamo 1934, wakati wa upapa wa Pio XI, mwishoni mwa mwaka wa Ukombozi. Yeye ndiye Msimamizi na mlezi wa waalimu, vijana, wanafunzi na wachapishaji.  Katika maisha yake kwa hakika alijitahidi hasa kuwaelimisha watoto na vijana wa kiume. Mbinu zake za malezi ni kwa pamoja: akili, dini, hisani. Hakutaka kurekebisha vijana kwa ukali, bali kuwakinga dhidi ya maovu kwa wema. Upendo wake wa ajabu kwa vijana ndio siri ya mafanikio yake ya ajabu katika malezi.

23 January 2021, 12:10