Tafuta

Maaskofu nchini Uganda wanahimiza kulinda kanuni za kidemokrasia zilizo kwenye Katiba ya nchi ambayo inahakikishia haki ya kila raia kuchagua viongozi wao wanao wataka Maaskofu nchini Uganda wanahimiza kulinda kanuni za kidemokrasia zilizo kwenye Katiba ya nchi ambayo inahakikishia haki ya kila raia kuchagua viongozi wao wanao wataka 

Uganda:maaskofu wanatoa wito kwa taifa,lisiwe na ghasia wakati wa kupiga kura

Bado siku chache za uchaguzi kwa watu wa Uganda tarehe 14 Januari,wakati huo maaskofu mahalia wana wasiwasi kwa sababu ya hali halisi ya kisiasa na kijamii katika kipindi hicho cha uchaguzi.Katika barua yao wanashuri kuwa na kura iliyo huru, aminifu na wito kwa vyama,mamlaka tawala na polisi kuwajibika kila mmoja katika nafasi yake kwa ajili ya wema wa wote,pia wapiga kura wanaitwa kuwajibika.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Katika barua ya kichungaji ya Baraza la Maaskofu nchini Uganda (Uec) katika fursa ya matazamio ya uchaguzi utakaofanyika tarehe 14 Januari 2021,wanaomba pasiwepo ghasia na uchaguzi uwe huru, uwe na usawa na wa kuaminika. Katika barua yao yenye  vipengele 58, imepewa jina “Heri wahudumu wa amani” huku wakiangazia umakini wa baadhi ya masuala msingi kuanzia na kukabiliana na dharura, uaminifu wote wa mchakato wa uchaguzi, hadi matokeo rasimi baada ya uchaguzi. Wakiomba awali ya yote ulazima wa uchaguzi huru, haki na uaminifu, viongozi hawa wanaelezea wasi wasi wao juu ya usimamizi wa matokeo ya uchaguzi wakibainisha kuwa ni moja ya changamoto kubwa katika nchi na ambayo ni moja ya sababu kuu ya ghasia. Wakati uliopita kiukweli, kumekuwa na umwagaji damu wa kweli baada ya uchaguzi na makovu ya vurugu hizo bado yapo. Walakini wakuu wa Kanisa wanasema waganda wote kuwa  badala ya kujifunza kutokana makosa kama hayo, wanaonekana kurudia tena. Kwa njia hiyo Baraza la Maaskofu  wanaomba pande zote zinazohusika kuruhusu mapenzi ya watu yashinde. Maaskofu wanasema “Kumbuka kwamba amri isemayo  Usiibe inatumika pia kwa wizi wa kura”.

Pasiwepo na upendeleo na wala pesa katika kura

Wasiwasi wa pili wa Kanisa la Uganda unahusu biashara ya upendeleo, kwani wagombea wengine wametumia kiasi kikubwa cha pesa kwa matumaini ya kupata pesa hizo mara baada  ya kushinda. Kwa hili Kanisa linaonya kwamba   “siasa sio biashara ya kupata pesa, hata hivyo, kwa kutusikitisha sana, hali imekuwa mbaya na inahatarisha mipango mizuri iliyozinduliwa katika sekta mbali mbali ili kuongeza utawala wa kidemokrasia wa kitaifa”. Vile vile  maaskofu wameonya dhidi ya ufadhili haramu wa uchaguzi na wanahimiza vyama na viongozi wao kuchukua jukumu, kwa sababu kwamba kuzidi kwa pesa kunaweza kusababisha ukosefu wa usawa kati ya watendaji wa kisiasa.

Ukiukaji wa haki za watu na wa amani ni sababu za ghasia

Miongoni mwa wasiwasi zaidi  pia uliooneshwa na Kanisa Katoliki ni ukiukaji wa amani na haki za watu: mnamo Novemba 2020, kiukweli, maandamano mengi yalitikisa nchi, kufuatia kukamatwa kwa Bobi Wine, mgombea urais wa chama cha Jukwaa la Umoja wa Kitaifa. Katika mapigano kati ya vikosi vya usalama na idadi ya watu, zaidi ya watu sabini waliuawa, wengi zaidi walijeruhiwa na uharibifu wa vifaa ulikuwa mkubwa. Maaskofu wanaandika kuwa “Kinacho tusumbua zaidi ni ukweli kwamba waathiriwa wengi walifariki au kujeruhiwa mikononi mwa vikosi vya usalama ambavyo vina jukumu la kulinda maisha na mali za raia. Tunachukulia kuwa ni matumizi mabaya ya mamlaka. Lakini pamoja na haya yote, wasio na hatia na wenye hatia bado hawajapata haki”.

kulinda kanuni za kidemokrasia katikaKatiba ambayo inahakikishia haki ya kila raia

Maaskofu wa Uganda aidha ametoa wito kwa mamlaka, ili kutekeleza jukumu lao kwa njia ambayo sio tu ya kukosea kimaadili, lakini pia inafikiria vizuri kuhakikisha au kukuza ustawi wa serikali na raia. Kwa kukabili shida, kwa dhati Serikali lazima ionyeshe kujizuia, ikijua kabisa kuwa serikali inayotawala au hasa kwa vitisho au ahadi za tuzo tu, haitoi kwa watu motisha yoyote ya kufanya kazi kwa faida ya wote na amani. Pia kuna wito mkubwa kutoka kwa Kanisa kulinda kanuni za kidemokrasia zilizo kwenye Katiba, ambayo inahakikishia haki ya kila raia kuchagua viongozi wao kwa kupiga kura, na kuiagiza Tume ya Uchaguzi kuandaa uchaguzi huru na wa haki ambapo haki hii inaweza kutekelezwa . Na tena, Maaskofu hao wanasema wana wasiwasi juu ya kutovumiliana, mafarakano katika vyama vya siasa, ufisadi, vitisho, matumizi ya lugha ya kukera na ya dharau kati ya wagombea, Ukosefu wa kujitoa kuwashirikisha vijana katika mchakato wa uchaguzi na utumiaji duni wa taratibu za kawaida za kupambana na Covid.

Hisia nzuri ya uzalendo ielekezwe kwenda kupiga kura

Kwa njia hiyo ni matumaini ya usimamizi mzuri wa mchakato wa uchaguzi katika siku zijazo, unapatikana ikiwa Tume ya Uchaguzi haina upendeleo, inaanzisha mipango ya ushirikiano na elimu kwa wapiga kura na inahusisha watendaji wote wa kisiasa. Vikosi vya usalama pia vimetakiwa kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unafanywa kwa kuishi kwa bidii na weledi. Kwa kuongezea, maaskofu wanaomba wapiga kura hisia halisi ya uzalendo ielezwe kwa kwenda kupiga kura mnamo tarehe 14 Januari 2021, wakati huo huo maaskofu wanaomba pia serikali kutafuta msimamo kati ya haki ya kupiga kura na haki ya afya, katika wakati wa janga. Hatimaye Baraza la Maaskofu nchini Uganda (Uec), wanashauri washindi wa siku za mbele  kuanza mchakato wa mazungumzo ya kitaifa na maridhiano, kwa sababu masuala mengi ambayo bado yanasubiriwa nchini hayawezi kutatuliwa kwa kura au kwa mabadiliko rahisi ya uongozi. Barua ya kichungaji inaishia kwa kuwahimiza wote kuwa mawakala wa amani na mashujaa hodari wa upendo wa Mungu kwa jirani.

08 January 2021, 12:20