Tafuta

CHANGAMOTO ZA MAGONJWA YA WANAWAKE NA WATOTO AFRIKA CHANGAMOTO ZA MAGONJWA YA WANAWAKE NA WATOTO AFRIKA 

Sudan Kusini:Imeanzishwa Hospitali ya walioathirika zaidi huko Rambek

Wasalesiani walijenga hospitali ya kusaidia watu wenye matatizo zaidi huko Rambek na wanawake walioko nchi za nje wameingilia kati kusaidia waliokumbwa na mafuriko huko Duk tangu Julai mwaka jana nchini Sudan Kusini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Hospitali ambayo imebobea masuala ya magonjwa ya wanawake na uzazi, mbayo inajikita kutoa huduma kwa wanawake walio katika mazingira magumu na wenye shida zaidi, ndiyo iliyoundwa na Wasalesiani kwenye utume wao huko Tonj, katika Jimbo la Rambek Sudan Kusini. Muundo jengo, uliobuniwa na Padre Omar Delasa, daktari wa asili ya Italia,ambayo  ina vyumba viwili vya kufanyia  upasuaji, vyumba kadhaa vya kujifungulia, maabara ya uchambuzi na nyumba inayoweza kukaribisha watu wa  kujitolea kumi na watano ambao husaidia kujaza mapengo katika sekta ya afya, ikitoa kusaidia wale ambao vinginevyo wasingeweza kupata huduma ya matibabu. Hospitali hiyo imepewa jina la Padre John Lee Tae-seok, mmisionari wa Kikorea wa Shirika hilo la Wasalesiani daktari ambaye alikufa mnamo 2010, baada ya kutumikia kwa muda mrefu katika utume wa Tonj, kiasi cha kujulikana kama “Don Bosco wa Tonj”. Inapaswa kusisitizwa kuwa, kulingana na data ya hivi karibuni, katika wilaya ya Warrap ambapo utume wa Tonj upo, vifo vya akina mama viko juu sana (vifo elfu 2 kati ya kesi 100 elfu), na zaidi ya asilimia 40 ya wanawake ambao, kabla, wakati na baada ujauzito hawapati msaada wowote. Pia kuna uzazi mwingi ambao hufanyika nyumbani, bila msaada wowote.

Hospitali hiyo ilianzishwa 2006

Kwa mujibu wa Padre Delasa amesema kuwa wazo la hospitali hiyo lilizaliwa mnamo 2006, wakati mmisionari huyo alipokwenda katika nchi ya Afrika kwa mara ya kwanza na Sudan Kusini ilikuwa bado kuwa huru kutoka Sudan. Kwa kuguswa na kuona wakazi wa eneo hilo ambao walikuwa na kidogo, Mtawa huyo mara moja alichukua hatua kujaribu kuanzisha mpango huo. Katika Sudan Kusini kuna maisha mengi yaliyosahaulika na shida ambazo hakuna mtu anayetaka kubeba, kama vile umaskini, vita, njaa, kutengwa. Kwa bahati nzuri, karibu na mchezo huo, kuna ulimwengu mzuri wa watu wa kujitolea maisha yao ambao, pamoja na msaada wa vifaa, wanachangia mafunzo ya wafanyakazi wa afya amesistiza Padre Delesa. “Tonjproject” ilianzishwa mnamo Novemba 2008, na leo inafanya mipango kadhaa ambayo inalenga kuhakikisha upatikanaji na usimamizi endelevu wa vifaa vya maji na usafi wa mazingira katika hospitali na mazingira ya misheni, pia kusadia shida ya njaa na kutoa elimu bora na nafasi ya kujifunza kwa wote.

Msaada wa watu nchini Sudan waingiliwa na wanawake wa diaspora

Mafuriko makali yaliyoikumba Duk na sehemu nyingine ya Serikali ya Jonglei mwezi Julai mwaka jana, ilikacha zaidi ya watu 350 elfu bila kuwa na paa la nyumba na bila kuwa na mambo ya lazima ya kuishi. Viwango vya maji vinaendelea hadi sasa kuongezeka, katika maeneo ambayo ni ya juu sana kutembea, watu hutumia rafu za muda zilizotengenezwa kwa karatasi ya plastiki au matangi makubwa yamegeuzwa mitumbwi. “Siku chache zilizopita tulipokea nguo, vyandarua na karatasi za plastiki ambazo tunatumia kama makao ya muda. Msaada huu ulitokana na misaada kutoka kwa wanawake wengine wa Duk walioko ughaibuni au diaspora”. Ndivyo inasomeka barua iliyotolewa na kituo cha redio kilichopo Duki nchini Sudan Kusini na kupelekwa kwa shirika la Habari za Kimisionari Fides.

Mafuriko yameharibu maisha ya watu na kuwaacha katika matatizo makubwa

Mafuriko hayo yameharibu maisha yote na kuwaacha watu katika hali ya hatari kabisa tangu Julai 2020. Elijah Manyok Deng, ambaye ni Kamishna wa Muda wa Duk, aliripoti kwamba wazee 2,500 walifaidika na misaada waliyopokea na kurudia wito kwa mashirika ya kibadamu ya misaada kutoka Jonglei kuingilia kati hali hii ya kibinadamu ambayo inabaki kuwa mbaya. Ripoti ya hivi karibuni iliyochapishwa kwa pamoja na serikali na Umoja wa Mataifa ilitabiri kuwa watu milioni 7.24 katika maeneo fulani ya nchi watakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula mnamo 2021 kutokana na athari za pamoja za mafuriko, mizozo na janga la Covid. -19.

22 January 2021, 10:44