Tafuta

2021.01.21: Shuke Katoliki nchini Gabon 2021.01.21: Shuke Katoliki nchini Gabon 

Gabon:Maaskofu katoliki wahimiza kipaumbele cha shule katoliki

Katika ujumbe wa Maaskofu baada ya Mkutano wao wa mwaka,wanahimiza kukarabati shule katoliki na kutoa kiapaumbele cha Kanisa kwa aili ya kuchangia maendeleo ya Nchi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika ujumbe wa Maaskofu nchini Gabon wakati wa kufunga Mkutano wao  wa 28 wa mwaka huko Libreville wiki iliyopita mawazo yao yote yameelekezwa juu ya elimu katoliki katika muktadha wa sasa, kijamii, kisiasa na kiuchumi. Katika ujumbe huo wanasema kuna aina nyingi za mateso ambayo kwa bahati mbaya yanaendelea kukatisha ulimwengu mzima, kwa namna ya pekee mgogoro wa kiafya, kiuchumi na kijamii ambao wanaishi mataifa yote. Mgogoro huo unawalika wote kuishi kwa imani kuu katika mchakato wa maisha ya kibinadamu kama vile kuona dhoruba kali inayokatisha bahari.

Shule katoliki inabaki kuwa mali ya Kanisa na kuapumbele cha maadili

Maaskofu katoliki nchini Gabon wameangazia yote hayo katika mchakato wa historia yao ya uinjilishaji nchini humo, katika Kanisa Katoliki kwa kuonesha thamani za kudumu na ambayo daima imeweza kutoa majibu ya ujasiri katika migawanyiko kijamii, huku wakifanya shule kama chombo cha huduma ya maendeleo kamili ya binadamu na katika kukua kwa taifa. Kwa mujibu wa Baraza la Maaskofu, Shule Katoliki inabaki kuwa mali ya Kanisa kama moja ya chombo msingi wa shughuli za uinjilishaji na kibinadamu. Ni lazima kutoa kipaumbele cha uendeshaji kinachosimika mzizi wake juu ya maadili na mafundisho maadili yanayofaa.

Jitihada za Kanisa katika mazungumzo na Taasisi za serikali

Katika ujumbe huo maaskofu wanathibitisha kujitoa kwa Kanisa Katoliki katika mazungumzo na taasisi za serikali huku wakigeukia Kurugenzi ya Kitaifa ya Elimu Katoliki kwa kihimiza utumiaji wa zana zinazofaa zaidi na ubora wa usimamizi, na wanaomba kuwe na uangalifu juu ya yote yanayotishia ubora wa elimu kama vile: udanganyifu, ufisadi, uwongo, na kuzorota kwa mazingira ya shule. Maaskofu wanawaalika mapadre, watawa wa kike na kiume kuwepo zaidi katika mchakato mzima wa ukarabati wa Shule Katoliki, kwa kusaidia na kutia moyo shule katoliki katika maeneo yote ya kichungaji na kushirikiana na mapadre wasimamizi wa vikanisa vidogo, ambamo utume unahitaji ubunifu aminifu katika maono ya elimu ya Kanisa, uwepo wa kweli na upendo mkuu. Maaskofu wanahimiza kufundisha mawakala kwa ajili ya uchungaji shuleni na kuanzisha madaraja muhimu ya kiinjili kati ya uchungaji wa familia na uchungaji wa shule.

Wahusika wakuu wa taasisi na wazazi

Kwa upande wa wahusika, Wakuu wa taasisi za elimu wamealikwa kuwa sio wataalamu wa elimu tu bali kuwa wataalamu wote wa imani katika utume wa elimu na kushirikiana na wafanyakazi  wote kufanya usimamizi ulio wazi zaidi wa kibinadamu, kielimu, kiutawala, kifedha na kichungaji kwa shule. Kwa upande mwingine, wazazi kama waalimu wakuu wa watoto wao na wanaohusika na kurithisha huku wakionesha imani na elimu ya dini, wanapendekezwa kufanya mazoezi ya kisakramenti na sala katika familia zao. Maaskofu pia katika ujumbe huo wanakumbuka hali fulani ya wale vijana ambao hawana sura ya baba katika maisha yao na ambayo wanasisitiza kuwa haiwezi kubadilishwa na shule. Na kwa maana hiyo vijana wote wameelekezwa  kuwa siku zijazo zinajengwa kupitia kila uamuzi watakaochukua wao wenyewe.

Vijana waamue maadili ya kiinjili

Wanawaomba vijana waamue kwa msingi wa maadili ya kiinjili ambayo imeoneshwa kwao. wajizoeze kila wakati kuchagua yaliyo bora, na sio vitu rahisi. Wajue namna ya kujitofautisha kwa kujitoa kwao katika masomo na kwa kufuata elimu ambayo inawahakikishia maisha ya baadaye yenye furaha. Vijana watengeneza nafasi za hali yao ya kiroho. Ujumbe wa Baraza la Maaskofu unahitimishwa kwa kupendekeza kujitoa kwa wote katika mchakato wa uwezeshaji na ukarabati wa shule ya Katoliki nchini Gabon na kwa mtazamo wao wanamgeukia Mtakatifu Joseph, wakiomba wote wawe katika shule ya Mtakatifu Yosefu, Baba wa Mtoto Yesu, ambaye kwake Baba Mtakatifu Francisko amezindua mwaka wake ili wote kuweza kujifunza nini maana ya  kuwa baba wa kweli na Mungu Baba yetu.

21 January 2021, 13:59