Tafuta

Vatican News
Kardinali Jean Pierre Kutwa, Askofu Mkuu wa Abidjan nchini Pwani ya Pembe Kardinali Jean Pierre Kutwa, Askofu Mkuu wa Abidjan nchini Pwani ya Pembe 

Pwani ya Pembe:muwe manabii na shuhuda wa utamaduni wa utunzaji!

Askofu mkuu wa Abidjan nchini Pwani ya Pembe katika siku ya 54 ya Amani ulimwenguni amewageukia viongozi wa kisiasa wa nchi hiyo hasa,akirudia wito wake uliozinduliwa Oktoba iliyopita kwamba ni juu yao kuwa wafuasi wa utulivu na amani kati ya wanadamu,bila kusahau kuwa Mungu Baba ni mbunifu wa kweli wa amani duniani,kwani ndiye anayeongoza historia ya wanadamu na ndiye pekee anaweza kufanya mioyo ikatae uovu,kubatilisha vita na taabu.

Na Sr.Angela Rwezaula- Vatican

Kuwa manabii na mashuhuda wa utamaduni wa utunzaji ili kweza kutuliza ukosefu wa usawa mwingi wa kijamii, ndiyo mwaliko uliotolewa na Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa Siku ya 54 ya Amani Duniani ambayo inaongozwa na kaulimbiu ya "utamaduni wa utunzaji kama njia ya amani". Na ni katika muktadha wa maneno ambayo Kardinali Jean Pierre Kutwa, askofu mkuu wa Abidjan, nchini Pwani ya Pembe, emejikita nayo katika barua yake ya kichungaji ya tarehe Mosi Januari 2021. Katika  siku inayoashiria mwanzo mpya wa mwishoni wa mwaka ambao umeona mgogoro mkubwa wa ulimwengu wa Covid-19, lakini pia ulioleta uharibifu, huko Pwani ya Pembe,pia na vurugu za uchaguzi.

Kiukweli mnamo  tarehe 31 Oktoba, uchaguzi wa rais ulifanyika, ukitanguliwa na mvutano na mapigano makali ambayo yalisababisha vifo vya watu 85, majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali katika nchi ambayo tayari imepata mizozo miwili ya wenyewe kwa wenyewe katika miongo miwili iliyopita, kati ya 2002 na 2003 na kati ya 2010 na 2011. Mgogoro huo umerudia kwa sasa, baada ya kuanza, tarehe 11 Novemba, meza ya majadiliano kati ya Rais anayemaliza muda wake Alassane Ouattara, aliyegombea mshindi wa duru ya uchaguzi, na mpinzani wake mkuu Henri Konan Bédié, kiongozi wa Chama cha Kidemokrasia cha Pwani ya  Pembe (PDCI).

Baada ya tafakari ya  kina ya  Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko, Kardinali Kutwa anaelekeza mawazo yake kwenye mzozo huu mpya wa kisiasa ambao umerudisha wigo la vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Pwani ya Pembe “Kilichotokea Oktoba iliyopita kinapaswa kuhusisha zaidi ya mtu mmoja, anasema kardinali. Vifo 85 rasmi, mapigano, uharibifu wa mali, walio jeruhiwa na uharibifu wa kudumu, yote ni ukweli ambao unatufanya tujiulize  juu ya utunzaji ambao tunapaswa kuwapatia wengine! ”. Kardinali Kutwa anaona kuwa ni ngumu kuelewa ni kwa jinsi gani Watu wa Pwani ya Pembe wamefikia hatua ya kuua na kuchoma nyumba na wakazi wao ndani, kwani watu ambao hapo awali waliishi pamoja kwa amani katika vijiji vyao wamegeuka kuingia kwenye mapigano kama haya.

Askofu mkuu wa Abidjan amewageukia viongozi wa kisiasa wa Pwani ya Pembe hasa, akirudia wito wake uliozinduliwa katika  kura ya maoni ya mwezi  Oktoba  iliyopita kwamba ni juu yao kuwa wafuasi wa utulivu na amani kati ya wanadamu, bila kusahau kuwa Mungu Baba ni mbunifu mkubwa wa kweli wa amani na amani duniani, kwa sababu ndiye anayeongoza historia ya wanadamu na ndiye pekee anayeweza kushinikiza mioyo kukataa uovu,mbatilishaji wa vita na taabu ”. Kwa maana hiyo mwaliko kwa watawala, wapinzani na raia wote wa Pwani ya Pembe kuwa manabii na mashuhuda wa amani katika nchi yao, kufuatia dira ya kanuni za mafundisho ya kijamii ya Kanisa yaliyokumbushwa na Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake, ili kuibadilisha dira hiyo katika nyakati hizi za dhoruba: kuhamasisha hadhi ya kila mtu, mshikamano na maskini na wasio na kinga, na kujali mahali kwa ajili ya faida ya wote na kulinda kazi yote ya uumbaji.

Kwa kuhitimishwa, kwa maneno ya Papa Fransisko, Kardinali Kutwa anawahimiza watu  wote wa Pwani ya Pembe kufanya kazi pamoja ili kuelekea katika upeo mpya wa upendo na amani, undugu na mshikamano, kuungwa mkono na kukubalika. “Tusikubali jaribu la kutopenda wengine, hasa walio dhaifu, tusizoee kugeuka na kutazama mbali, lakini tujitoa kwa usawa kila siku  ili kuunda jamuiya  inayoundwa na ndugu ambao wanakaribishana na kujaliana mmoja na mwingine.

02 January 2021, 15:34