Tafuta

Vatican News
2020.10.28 Patriaki Pizzaballa 2020.10.28 Patriaki Pizzaballa 

Patriaki Pizzaballa kukutana na viongozi wakuu wa Yordani!

Patriaki Pierbattista Pizzaballa,wa kilatino wa Yerusalemu yuko katika ziara yake rasmi katika Ufalme wa Yordani tangu tarehe 7 Januari ambaye tarehe 18 Januari amekutana na viongozi wakuu wa nchi kwa maana ya Mfalme Abdullah II na Spika wa Bunge la nchi hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Yordani inawakilisha mtindo katika kutafuta amani na mazungumzo kwa namna ya kukataa vurugu na kila aina ya ubaguzi. Amesema hayo Patriaki Pierbattista Pizzaballa, wa kilatino wa Yerusalemu ambaye yuko katika ziara yake rasmi katika Ufalme wa Yordani tangu tarehe 7 Januari ambaye tarehe 18 Januari amekutana Spika wa Bunge la serikali Abdul Mun’im Odat. Wakati wa mazugumzo yao kwa mujibu wa Tovuti ya Upatriaki wa Yerusalemu, Patriaki ameeleze kwa kina shukrani nafasi yake aliyo nayo Mfalme Abdullah II,  nafasi yake msingi katika kulinda hali halisi ya Kikristo huko Yerusalemu, katika mantiki ya usimamizi wake wa kifalme wa maeneo matakatifu ya mji.

Na zaidi amebainisha umuhimu wa uhusiano wa kihistoria kati ya Upatriaki wa kilatino wa Yerusalemu na Yordani. Na kwa upande wake Mwenyekiti wa Bunge amethibitisha kuwa Yordani chini ya uongozi wa mfalme Abdullah II, anaendelea kupongeza uwepo wa kikristo katika Nchi Takatifu na dini nyingine na kusisitiza kuwa ulinzi wa kufalme katika maeneo matakatifu na ya kiislam huko Yerusalemu utabaki kuwa wa kihisitoria zaidi ya kuwa na uhakika wa uhifadhi wake. Bwana Abdul Mun’im Odat vile vile ameleza kuwa Yordani ni Serikali inayojali iwe mbele ya wazalendo wake wa kiislamu na wakikristo, ambapo Yordani wameungana na Mfalme Abdullah II katika kusaidia nafasi ya Baraza la Makanisa Yerusalemu ambayo yanatazamia kuimarisha utamaduni wa kiasi, wa maungumzo na kulinda mali za Makanisa na taasisi zao Wiki iliyopita, Patriaki Pizzaballa alikuwa na mkutano na Rais wa Seneti Faisal Al Fayez. Akiwa bado anaelezea shukrani zake kwa juhudi zilizofanywa na Yordan, chini ya uongozi wa Mfalme Abdullah II, katika kuhifadhi maeneo matakatifu ya Yerusalemu,Patriaki huyo alidokeza juu ya uhusiano wa kipekee kati ya watu wa Palestina na watu wa Yerusalemu kwa upande mmoja na uongozi wa ufalme kwa upande mwingine.

Kwa upande mwingine, Rais wa Seneti alitoa wito wote wanasiasa, wasomi na dini za taifa kuimarisha madhehebu yao  kati ya waamini wa dini za Ibrahimu na kueneza maadili ya udugu, uvumilivu na kiasi. Faisal Al Fayez pia alisema kuwa Yordani imekuwa ikiunga mkono suala la Palestina, kwamba Mfalme Abdullah II anaendelea kulinda maeneo matakatifu ya Kikristo na Kiisilamu ya Yerusalemu, na kwamba Ufalme wa Hashemite unabaki kuwa mfano wa umoja, udugu na kuishi kwa amani kati ya Wakristo na Waislamu.  “Tunajivunia katika Yordani kubarikiwa na uongozi wenye hekima wa Mfalme,  ambaye kila wakati amekuwa ikitoa juhudi za kueneza utamaduni wa maisha ya pamoja, upendo na maelewano, kuhamasisha maadili ya kibinadamu, kukataa utamaduni wa chuki, vurugu na msimamo mkali na amekuwa ikihamasisha maadili ya pamoja  kudumisha usawa”m alihitimisha Rais wa Seneti.

20 January 2021, 15:14