Tafuta

Vatican News
2021.01.14 Kifuniko cha kitabu kipya kiitwacho"Non sparlare degli altri" yaani "isisengenye wengine" 2021.01.14 Kifuniko cha kitabu kipya kiitwacho"Non sparlare degli altri" yaani "isisengenye wengine" 

Papa Franciskio:Ukimya ni lugha ya Mungu&lugha ya upendo

Ni kuanzia na ukimya ndiyo unafikia upendo wa dhati kwa wengine.Ni maneno ya Papa Fancisko katika utangulizi wa toleo jipya la kitabu kinachoitwa"Non sparlare degli altri” yaani “Usisengenye wengine” cha Fra Emiliano Antenucci,ambapo Papa anasisitiza kuwa maneno yanaweza kuwa ya busu au kisu.Katika mahojiano na mwandishi amesema kutoka kwa Papa ni mwaliko wa kugundua sala ya kimya,kusali na siyo kusema sala.

Ni kuanzia na ukimya ndiyo unafikia upendo wa dhati kwa wengine. Anakumbusha Papa Francisko akimtaja Mama Teresa wa Kalkuta, katika maandishoi yake ya utangulizi au dibaji kwenye toleo jipya la kitabu ambacho kimejaa utajiri wa mafundisho mazuri, kilichopewa jina la “Non sparlare degli altri, yaani  "usisengenye wengine", ambacho kimeandikwa na Ndugu Emiliano Antenucci, wa Shirika la Ndugu wadogo wafransiskani Kapuchini. Mwandishi huyo ni mmisionari wa huruma ambaye tangu Mwezi Mei mwaka jana ni Msimamizi wa Madhahu ya Bikira Maria wa Kimya iliyoko huko Avezzano, mkoa wa Abruzzo, nchini Italia, kwa utashi mwema wa Papa Francisko.

Masengenyo ni tendo linalifanana na kuua 

Katika utuangulizi wa Papa Francisko kwa hakika unatajirishwa kitabu hicho kwa mafundisho ya kiroho na ambamo ni uthibitisho wa kiini cha huduma yake kama Papa na mada msingi wa mapambano dhidi ya masengenyo na matumizi mema ya maneno. Lakini hata hivyo kazi hii inataka kuwa mwaliko wa kuweza kugundua kwa namna moja sala ya ukimya kama alivyo bainisha kwa njia ya simu ya Radio Vatican, Ndugu mdogo Emiliano Antenucci. Katika maelezo yake anasema “Dibaji hii ya Papa imekuwa zawadi nzuri na  zawadi kubwa. Kusengenya  kiukweli kama vile  Papa Francisko anavyo elezea, kwa mtazamo wa kitaalimungu pia kulingana na Amri za Mungu, ni ishara inayoharibu picha ya uzuri ambao uko katika kila mmoja wetu. Tunapofanya mazungumzo yenye masengenyo, tunafanya kitendo kinachofanana na kile cha mauaji, kwa sababu kama Papa anavyo kumbusha "mtu haui tu kwa silaha, lakini pia anaweza kuuawa kwa ulimi wake".

Ukimya ni lugha ya Mungu 

Katika utangulizi wake Papa anasema kuwa ukimya pia ni lugha ya Mungu kwa maoni yake Ndugu Emiliano anasema inamaanisha kwamba lazima sisi sote tugundue tena maombi ya kimya, kwa sababu ukimya ni kama uchunguzi ambao tunaweka mioyoni mwetu kumsikiliza Bwana. Kwa upande mwingine, kama nabii Eliya anavyo kumbusha kwamba tunamsikiliza Bwana katika upepo mwanana, kwa njia hiyo ukimya ni chombo, ni njia ya kusikiliza sauti ya Mungu ambayo inazungumza ndani mwetu. Papa Francesco anasisitizia wazo ambalo anapenda sana  kulitumia kwamba kwa kutumia maneno kama mabomu, mtu anakuwa gaidi na maneno, yanaweza kuwa mabusu, ya kubembeleza, dawa au visu, panga na risasi ...

Kusengenya leo hii ni mchezo wa ulimwengu

Ndugu Emilian akiendelea na ufafanuzi wake amesema lazima tukumbuke kuwa leo hii kusengenya ni mchezo wa ulimwengu, unaofanywa katika mazingira yote, hata katika yale ya Kanisa. Mabomu ambayo Papa anazungumza ni uvumi na kashfa na kwa sababu hii ni muhimu, kama Baba Mtakatifu anavyoandika kwamba Bikira wa Ukimya atufundishe matumizi sahihi ya lugha. Frateli Emiliy kutokana na hili anafikiria hasa wale wanaofanya kazi katika mawasiliano kwa sababu, neno hasa linaweza kutoa uhai au kifo, maneno yanaweza kuwa kuta au madaraja. Aidha amependa kukumbusha kwamba mahali Patakatifu pa madhabahu ya Mama wa Ukimya huko Avezzano, ambaye yeye ni kama Mkuu ilizaliwa mnamo Mei mwaka jana hasa kwa mpango wa Baba Mtakatifu Francisko. Na zaidi Papa alimwandikia Mkuu wake wa shirika  na alitaka kabisa madhabahu hiyo  ambayo ilifunguliwa kwa agizo la askofu wa Jimbo  mnamo tarehe 13 Mei  mwaka jana. Ni kituo cha kiroho, cha kimya, sala na kufanya mnag’amuzi. Na itakapowezekana hasa baada ya janga na hati mpya za idhini na serikali, wannatarajia kuanza tena kozi zilizowekwa kwa ajili ya ukimya na kufanya mang’amuzi. Wakati huo huo, Madhabahu hiyo iko wazi wakati wote, imefunguliwa hata kwa  kuheshimu kanuni za umbali kijamii, lakini pia kuna sherehe za Ekaristi, kuabudu, kuungamna pia siku za mafungo.

Kwa nini mada ya ukimya ni muhimu kwa Papa Francisko

Akijibu swali ni kwanini anafikiri mada ya ukimya imekuwa muhimu sana katika mafundisho ya Baba Mtakatifu Francisko amesema “Hatupaswi kusahau kwamba mara tu alipochaguliwa, mnamo terehe 13 Machi yaani miaka minane iliyopita, mbele ya umati huo mkubwa ambao sisi wote tunakumbuka katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Papa Francisko alijionesha kama askofu wa Roma na akamwalika kila mtu amwombee kwa kimya kwa kuwaomba umati wote huo ukae kimya. Lakini haikuwa mara ya kwanza na ya pekee kwa sababu katika matukio mbali mbali ya mikutano yake , hata wakati wa mikutano ya sinodi, Papa Francisko ametaka uwepo wa ukimya. Walakini, kipinid cha ukimya sio wakati  usi ona mwafaka, ni wakati ambao kila mtu anajirudi kwake mwenyewe na anaomba na kuombea wengine, kwa sababu sala ya kimya pia ni maombi  kwa aili ya  kuwaombea watu wa Mungu...

Je utakayesoma kitabu hiki atafaidikaje?

Atakayesoma kitabu hiki, kwanza kabisa, kimekusudiwa kuwa kijitabu cha motisha, kwa sababu kama vile Mtakatifu Yohane Paulo II alivyosema ‘lazima tufanye kazi kwa bidii’ na labda ndiyo ingeweza kuwa kichwa kidogo cha kitabu kwa  maneno hayo maarufu ya miaka  iliyopitia ya Papa Wojtyla, amesisitiza Fr Emilliano. Kwa  njia hiyo "ni mwaliko wa kutopoteza wakati katika kusengenya, lakini kuishi maisha yetu na kujituma kila siku katika kazi, kwa njia ya maombi na katika yote ambayo Bwana anatuomba tufanye".  Ndugu mdogo Emilliano amesema kwamba hakutaka kutengeneza kijitabu cha uchunguzi. Lakini "katika sehemu ya kwanza kinachambua sababu ambazo zinatuongoza kufanya uvumi, lakini kuna suluhisho zaidi, kwa sababu ni muhimu kwa kila shida katika maisha yetu kupata suluhisho lililo bora".

Kufuatia mafundisho ya Baba Mtakatifu, amesema kwamba anawaalika kila mtu afumbe macho yake na kuomba amsaidie maskini na amuoneshe suluhisho nzuri za kushinda uovu huu ambao umeenea katika mazingira yote.  Kwa kuhitimisha amesema kitabu hiki ni kama kiongozi cha kiroho ambacho kinataka ugundue sala ya kimya kwa sababu ni jambo msingi. Sala ya kweli sio kusema sala ambayo hufanywa katIka ukumbi wa michezo. Kuomba ni kuwa mbele za Bwana kwa kimya, kwa sababu ukimya kama Baba Mtakatifu anakumbusha ni lugha ya Mungu lakini pia lugha ya upendo.

15 January 2021, 16:28