Tafuta

Vatican News
Nchi Takatifu Patriaki Pizzaballa Nchi Takatifu Patriaki Pizzaballa   (AFP or licensors)

Nchi Takatifu,Siku ya Amani duniani:wakristo wahimizwa kushinda ukiritimba na upendeleo

Kiunganishi cha shida zote kama ukiritimba na upendeleo ni ubinafsi ambao umekuwa kiini katika mawazo ya kawaida pia katika Kanisa la Yerusalemu.Njia ya kuzishinda na kuboresha ni kuanzia na uhusiano wetu na Kristo,sio kutokana na mahitaji yetu bali kuweka moyo wetu ndani ya moyo wa Kristo,kusoma ukweli wetu,hata wa kikanisa,katika mwanga wa Neno la Mungu.Ni mawazo ya tafakari ya Patriaki Pizzaballa huko Yerusalemu.

Na Sr.angela Rwezaula- Vatican.

Kushinda ukiritimba na upendeleo wa ndani ambao unahatarisha  na kuzuia safari ya kikanisa ya Kanisa mahalia, kwa kuanzia  na Kristo, Yule aliyevunja ukuta wa utenganisho kwa njia ya mwili Wake (Efe. 2,14-18). Huu ndiyo umekuwa kiini cha mahubiri mkuu wa Upatriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, Patriaki Pierbattista Pizzaballa,(Ofm), katika sherehe ya Bikira Maria Mama wa Mungu, sambamba na Siku ya Amani Ulimwenguni, tarehe Mosi Januari 20201. Wakati wa Misa, kiongozi huyo ametaka kutafakari juu ya mada ya amani kutokana na mtazamo wa ndani, akizingatia “vizuizi ambavyo wakati mwingine bila kujua tunajiwekea ndani mwetu na kati yetu” amebainisha Patriaki.

Patriaki Pizzaballa miongoni mwa mengi ameorodhesha manne. Katika nafasi ya kwanza amezungumzia kuhusu umbali kati ya makasisi na walei, hasa kama jambo lililoenea kama ilivyoonyeshwa mara kadhaa na Baba Mtakatifu Francisko, lakini ambalo Patriaki ameliona kuwa inaonekana wazi katika Kanisa la Yerusalemu. Ushirikiano kati ya makuhani na walei mara nyingi haueleweki na kuishia “kufanya tu kile anachotaka kuhani” alisema Patriaki. Mantiki za kiutamaduni hazisaidii kuwa na mtazamo wa pamoja wa maisha ya kikanisa na kwa upande mmoja ni ngumu kuwashawishi watu kuwa na mabaraza ya parokia na kujua jinsi ya kushiriki maoni na mipango na kwa upande mwingine pia ni ngumu kupata watu waliofunzwa, wanaojitolea ambao wanataka kutoa mchango mzuri kwa jumuiya” amesisitiza.

Kulingana na Patriaki Pizzaballa ni kizuizi halisi ambacho kinahitaji kuzingatiwa, hasa kwa kuzingatia kizazi kijacho, ambacho kinataka kuwa mhusika mkuu wa maisha ya Kanisa, na sio watekelezaji tu wa maagizo na maelekezo”. Patriaki wa Yerusalemu alizungumza pia juu ya “pengo la kizazi kati ya wale ambao wanajutia mitindo ya zamani na wanajuta mfano wa Kanisa na jamuiya ambayo leo hii  inaonekana haipo tena, wakisahau hata hivyo kuwa kuishi sasa na utulivu wa Kikristo, na vijana ambao wanataka kubadilisha hata kile labda ambacho hakihitaji kubadilishwa. Nafasi zote mbili, alisema, zimetoweka katika wakati wa sas ana wakati kinacho ombwa katika Kanisa ni kusikilizana, kushukuru kwa kile ambacho kimefanywa hadi sasa na kufungua njia mpya kulingana na neema ya Mungu”.

Mkuu huyo pia aliangazia “umbali uliopo kati ya eneo la ndani na sehemu ya ulimwengu ya Kanisa la Yerusalemu, ambao ni jaribu, lililoenea katika wilaya zote zilizojumuishwa katika Patriaki huo, kuchukulia sehemu ya ulimwengu kama mgeni na sio kama sehemu fungamani ya  Kanisa”, wakati badala yake, alithibitisha, roho hizi mbili lazima zisaidiane, zote kwa maana zinahitajika, zote ni kitambulisho na historia ya Kanisa letu”. Vizuizi vingine vinawakilishwa na vitambulisho vinne vya kitaifa vya majimbo ya (Yordani, Israeli, Palestina, Cyprus),kwamba “mara nyingi hujengwa dhidi au kinyume pia kwa sababu ya muktadha ambao Kanisa mahali linaishi na tofauti za lugha ambazo ni "utajiri wa ajabu, lakini pia sio kikwazo kidogo katika mkutano na kushirikishana.”

Patriaki Pizzaballa kwa maana hiyo ameangazia kwamba kiunganishi kikubwa cha shida hizi zote ni ubinafsi ambao umekuwa kiini  katika mawazo ya kawaida pia katika Kanisa la Yerusalemu. Njia ya kuzishinda na kuboresha kwa njia hiyo  ni kuanzia na uhusiano wetu na Kristo na sio kutokana na mahitaji yetu; ni kuweka moyo wetu ndani ya moyo wa Kristo, kusoma ukweli wetu, hata wa kikanisa, kwa mwanga wa Neno la Mungu. Hatuwezi kuishi bila upendo na upendo utakaoanzia ni katika upendo wa Yule aliyetoa uhai wake kwa ajili yetu na kwa ajili ya wokovu wetu ”,alihitimisha Patriaki mahubiri yake katika siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu sambamba na Siku ya Amani ulimwenguni tarehe Mosi Januari 2021.

02 January 2021, 10:19