Tafuta

2020.04.24 Kardinali charles Bo, Rais wa Baraza la maaskofu Cbcm) 2020.04.24 Kardinali charles Bo, Rais wa Baraza la maaskofu Cbcm)  

Myanmar:wito wa maaskofu kwa wamini wajitoe ili kununua chanjo

Dominika tarehe 17 Januari 2021 Kanisa nchini Myanmara imetoa wito wa kuota kuchangia ununuzi wa chanjo dhidi ya Cpvid/19.Imetoa rai hiyo mara baada ya mkutano wao wa mwaka uliofanyika kwa njia ya mtandao.Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la habari UCA inasema kuwa mwaliko wa wa ukusanyaji huo ukabidhiwemaaskofu ambao wataweza kuhamisha fedha hizo katika mfuko wa Taasisi ya Serikali.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Maaskofu nchini Myanmar wametoa wito kwa wakatoliki nchini humo ili wajitoa  kutoa michango kwa ukarimu katika kampeni ya hukusanyaji fedha iliyo hamasishwa na mamlaka ya Birmania kwa ajili ya ununuzi wa chanjo ya kuzuia Covid. Wito huo umetangazwa Dominika tarehe 17 Januari 2021, mara baada ya mkutano wao wa mwaka uliofanyika kwa njia ya mtandao. Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la habari UCA inasema kuwa mwaliko ni kuwa sadaka yao wanapaswa kuwakabidhi maaskofu ambao wataweza kuhamisha fedha hizo katika mfuko wa Taasisi ya Serikali.

Katika barua iliyotiwa siani na Rais wa Baraza la maaskofu(Cbcm) nchini humo, Kardinali Charles Bo, na Askofu  John Saw Yaw Han, katibu mkuu, maaskofu hao wanabainisha kuwa ugunduzi wa chanjo unawakilisha machweo mapya ya matumaini kwa ajili ya ulimwengu, huku wakikumbuka kuwa janga ni taadhari kwa ajili ya amani na maelewano na asili yaani dunia mama yetu. Wote kama wazazi  maaskofu wanasema lazima kuacha nyuma yao ukijani kwa namna ya kwamba watoto wao wanaweza kurithi kile ambacho walitakiwa kupata bila kutumia vibaya na rasilimali hizo ,wamesisitiza maaskofu wa Birmania, ambapo Kardinali Bo amerudia kukumbusha mwaliko  aliokuwa tayari ameutoa mwishoni mwa mwaka 2020. Katika barua hiyo ya maaskofu (Cbcm)wamepyaisha shukrani zao kwa watu wote ambao wako mstari wa mbele katika harakati za kuzìsaidia  kuzuia  maambukizi ya janga.

Kwa sasa nchini humo zaidi ya kesi za covid-19, ni 134, 000 na vifo vya watu 3,000 na inabaki kuwa  nchi ya tatu iliyopata pigo kubwa la Covid-19 katika mkoa wa Asean, baada ya Ufilippini na Indonesia. Kinacho athiri  kwa namna ya pekee katika nchi ya Asia ni udhaifu wake wa mfumo wa kiafya kitaifa. Katika miezi hii, shughuli ya upendo wa Kanisa mahalia katika kusaidia waamini na watu wote waliokumbwa na janga haikusimama kamwe.  Baraza la Maaskofu wameanzisha kamati maalum inay oongozwa na Kardinali Charles Bo ili kuratibu usaidizi wa familia wenye kuhitaji zaidi. Kanisa limeandaa ukusanyaji mbalimbali wa  fedha za kuweza kusaidia .Pia shughuli ambayo ni muhimu ni kwa njia ya watu wa kutolea. Wiki iliyopita, Jimbo Kuu la  Mandalay, Marco Tin Win, ametoa Milioni 10 za  kyat, zenye thamani ya dolani 7.560 kwa serikali mahalia kwa ajili ya kununua chanjo. Kati ya tarehe 6 hadi 12 Januari, serikali ya Birmani imekusanya 2.67 milioni za dola kwa ajili ya chanjo. Lengo la chanjo ni asilimia 20% ya watu wote kufika mwishoni mwa mwaka.

19 January 2021, 13:51