Tafuta

Vatican News
2020.04.10 Askofu Moses Hamungole wa Jimbo katoliki la  Monze, Zambia 2020.04.10 Askofu Moses Hamungole wa Jimbo katoliki la Monze, Zambia 

Zambia:Jimbo la Monze kuanza ujenzi wa Kanisa kuu la Utatu Mtakatifu

Kazi ya ujenzi wa Kanisa Kuu Katoliki la Monze nchini Zambia inaanza tarehe 21 Desemba 2020 ambapo ujenzi wa Kanisa kuu utasaidia kukidhi mahitaji ya jamuiya ya Wakatoliki inayoendelea kuongezeka,kwa Mujibu wa Askofu Moses Hamungole wa Jimbo hilo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jimbo katoliki la Monze nchini Zambia hatimaye watakuwa na Kanisa kuu jipya la kuweza kuwakaribisha waamini wake wengi zaidi. Baada ya kuzindua mpango huo mnamo 2015 na miaka mitano ya kutafuta fedha, kiongozi wa jimbo hilo Askofu Moses Hamungole, hivi karibuni alisaini Mkataba wa Makubaliano na kampuni moja iitwayo ‘Three RT Investments' iliyokabidhiwa kazi ya ujenzi ambayo itaanza tarehe 21 Desemba. Kanisa kuu litaitwa “Utatu Mtakatifu”.

Ardhi ambayo jengo litasimama ilitolewa na serikali ya Zambia ambayo ilitoa eneo la zaidi ya hekta mbili kwa Jimbo hilo. Gharama ya awali kwa ujenzi wake ilikuwa ni dola za kimarekani 800,000 lakini ambazo zitaongezwa dola za kimarekano 200elfu kwa ajili ya vifaa, zilizokusanywa na mchango mkubwa wa ukarimu wa waamini, kwa mujibu wa taarifa kutoka katika blogi ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki (Amecea). 

Kanisa kuu  jipya, litakuwa na mmuda wa kipenyo katikati na paa la mteremko uliofunikwa kwa sehemu na sura ya mstatili na mabawa mawili ya pembeni, na ambalo litaweza kuchukua zaidi ya watu elfu moja. Kwa mujibu wa maelezo ya Askofu Hamungole amesema, ujenzi wa Kanisa kuu utasaidia kukidhi mahitaji ya jamuiya ya Wakatoliki inayoendelea kuongezeka. Jimbo hili lilichaguliwa mnamo 1962, na mnamo 2016 jimbo hilo lilikuwa na Wakatoliki 402,000, karibu robo ya wakazi wa eneo hilo.

 

15 December 2020, 17:58