Tafuta

Vatican News
2020.12.29 Askofu  Moses Chikwe, Msaidizi wa Jimbo Kuu Owerri, Nigeria ametekwa nyara 2020.12.29 Askofu Moses Chikwe, Msaidizi wa Jimbo Kuu Owerri, Nigeria ametekwa nyara 

Watu wenye silaha wateka nyara Askofu wa Owerri nchini Nigeria

Wanaume wenye silaha nchini Nigeria wamemteka nyara Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Owerri,katika serikali ya Imo, Mashariki mwa Nigeria.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Jumapili usiku, watu wenye silaha walimteka nyara Askofu Msaidizi wa Jimbo la Owerri, nchini Nigeria, Moses Chikwe, na dereva wake, ambaye jina lake halijafahamika. Askofu Mkuu wa Owerri, Victor Obinna alithibitisha utekaji nyara huo katika taarifa iliyotolewa kwa Vatican News, kwa niaba yake na Kansela Mkuu wa Jimbo Kuu, Alphonsus Oha. Mhashamu Askofu Mkuu Anthony J.V. Obinna, Askofu Mkuu wa Owerri kwa uchungu anawajulisha waamini wa Kristo na watu wa Mungu kwa ujumla kuwa Mchungaji Moses Chikwe, Askofu Msaidizi wa Owerri alitekwa nyara jioni ya Jumapili tarehe 27 Desemba 2020. Tukio hilo lilitokea karibu na eneo la utoaji Huduma ya Owerri Mpya katika serikali ya Imo.

Katika mahojiano na Vatican News, Jumanne, tarehe 29 Desemba, Askofu Mkuu Obinna, amesema alikuwa akipokea ujumbe wa mshikamano na uhakikisho wa maombi kutoka ndani ya Jimbo kuu na nje ya nchi na watu wameogopa jambo ambalo  linaweza kumtokea Askofu. Na kwa kuoongeza pia amesema  Askofu Mkuu kwamba utekaji nyara ulikuwa ni ishara ya kuonesha kuwa Kanisa halijatengwa na mateso ya kawaida ya watu. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Obinna amesema:

 “Askofu Chikwe alitekwa nyara siku mbili zilizopita wakati alikuwa akirudi kutoka  ziara ya makazi yake huko Owerri, maili moja au mbili kutoka mji wa Owerri, ambako ana makazi yake. Utekaji nyara umekuwa ukiendelea huko Nigeria, katika sehemu tofauti za Nigeria. Na hiki kichotokea kwa  kwa Askofu wangu Msaidizi kinaonyesha kuwa hali ya usalama nchini Nigeria ni mbaya sana. Ulinzi, usalama ambao watu wanapaswa kuwa nao sio mzuri sana. Mara kwa mara tumebainisha juu ya  tahadhari kuhusu hali ya ukosefu wa usalama ambayo tunajikuta nayo… Kanisa haliko mbali na watu. Hatujatengwa kutokana na mateso ya watu. Tunachukulia kama sehemu ya ushuhuda wetu ambao tunapaswa kuubeba", alisema na Vatican News.

Kulingana na vyombo vya habari vya Nigeria, gari la Askofu Chikwe na mavazi ya maaskofu yameachwa na wahalifu karibu na eneo la Kanisa Kuu la Owerri. Shirika la hagabari za  kimisionari Fides zinaripoti kuwa polisi wameanzisha timu mbili maalum, ya kwana Timu ya Uingiliaji wa Haraka (QUIT) na Kitengo cha Kupambana na Utekaji Nyara (AKU), kumtafuta Askofu Chikwe na kuwakamata watekaji nyara. Kutekwa nyara kwa Askofu Msaidizi wa Owerri kunakuja wiki moja tu baada ya kutekwa nyara katika Jimbo la kuhani mwingine Mkatoliki Padre Valentine Oluchukwu Ezeagu, aliyetekwa nyara mnamo Desemba 15 na watu wenye silaha wakati akienda kwenye mazishi ya baba yake. Kuhani  huyo aliachiliwa baadaye mnamo tarehe 16 Desemba.

Askofu Chikwe, ni mwenye umri wa miaka 53, aliteuliwa kuwa Askofu Msaidizi wa Owerri mnamo Oktoba 2019. Katika miaka ya hivi karibuni, makuhani wa Nigeria na watawa wamekuwa walengwa wa utekaji nyara. Wahalifu huwateka nyara watawa na makuhani kwa kudhani kwamba mashirikiana au majimbo  watalipa fidia kwa kutolewa kwa mmoja wao. Watekaji nyara wa wafanyakazi wa Kanisa nchini Nigeria wametuma ujumbe wa kutisha kuhusu usalama binafsi. Sio wafanyakazi wa Kanisa tu ambao ni walengwa wa utekaji nyara bali na wengine. Wakati wanasiasa wa Nigeria, wafanyabiashara matajiri na wanawake na wanadiplomasia wa kigeni wanajibu kwa usalama zaidi wenye silaha na madirisha ya gari yaliyofifiwa, lakini kwa wafanyakazi wa Kanisa na Waigeria wa kawaida hawana chaguo hilo.

29 December 2020, 17:06