Tafuta

Vatican News
Patriaki Bartholomew I Patriaki Bartholomew I  (ANSA)

Patriaki Barttholomew:La Civiltà Cattolica ni sauti ya hekima ya kikristo na kitaalimungu

Katika maadhimisho ya miaka 150 ya kihistoria ya jarida la Shirika la Yesu,Patriaki wa kiekumene amemwandikia Mkurugenzi Padre Antonio Spadaro anasema “La Civiltà Cattolica” inafunua kwa usahihi kiwango cha shida za leo hii na njia ya kuzitatua.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Patriaki wa Kiekumene wa Consantinople Bartholomew I ameandika barua yake aliyo mtumia Padre Antonio Spadaro, Mkurugenzi wa jarida la kizamani kwa lugha ya kiitalino ambalo linatimizia maiaka 170.  Patriaki anaadikia kuwa “Jarida la La Civiltà Cattolica linaangazia na kutoa mchango wa imani ya Kikristo katika tamaduni, tofuati kwa  mazungumzo ya Ukristo na falsafa na mikondo tofauti ya  kiitikadi, na kidini, kisayansi, na kwa jumla, ikiwa na  nafasi ya kisiasa na harakati za kijamii, kila wakati katika  msingi wa tamaduni  na kama dhihirisho la kujitambua kwa Kanisa Katoliki la Roma na Mkuu wake Papa. Ni maneno ya kusifu na kupongeza kwa ajili ya mshangao wa mchango wa jarida hili la Kanisa , la kijamii  na utamaduni na matashi yake ni yale ya kuendeleza utume mwema na kuwa shuhuda mwema na huduma yake.   Patriaki Bartholomew anasisitiza kuwa  “La Civiltà Cattolica  ni sauti ya usawa, yenye busara na wazi ya Kikristo na kitaalimungu ulimwenguni, ambayo hufunua kwa usahihi wa kuvutia vipimo vya shida kubwa za wakati huo na mwelekeo ambao suluhisho lao linapaswa kutafutwa.

Kutoka kwa tumaini lililo ndani mwenu linalisha mbio kwa ushuhuda wa Kikristo ulimwenguni na kubadilika kwake katika Kristo. Hakika, imani katika Kristo ni chanzo cha msukumo wa muda na hatua ya ubunifu. Inamuimarisha mwanadamu hata mbele ya vizuizi visivyo na shaka na bila njia ya kutoka. Ni hakika kwamba wakati imani katika hatima ya milele ya mwanadamu inakosekana, maisha hubeba alama ya ubatili. Uhusiano usiobomoka na umoja wa upendo kwa Mungu na upendo kwa jirani, kama ilivyoonyeshwa katika Agano Jipya, ndiyo maadili makuu ambayo wanadamu anayejua katika kipindi chote cha kihistoria. Kumpenda Mungu na kumpenda mwanadamu ni nguzo mbili za kuishi kwa Kikristo. Kutokana  na uhusiano huu maradufu wa maisha na hali ya kiroho ya mtiririko wa uaminifu, nguvu inayopendeza, mipango iliyoongozwa, mawazo ya kichungaji, kujinyima na tabia ya kumnufaisha jirani.

Uwepo na hatua ya Mapadre wajesuit ulimwenguni, ufahamu wa karibu wa tamaduni tofauti, mafunzo na uchunguzi wa kimfumo wa dini, ufuatiliaji wa maendeleo ya kisayansi, uchambuzi na tathmini ya data ya kijamii, kama kikomo cha lazima cha njia yao, inahakikishwa katika nakala za uhalali wao wa mara kwa mara na utajiri wa maoni. La Civiltà Cattolica ni sauti yenye usawa, yenye busara na wazi ya Kikristo na kitheolojia ulimwenguni, ambayo hufunua kwa usahihi wa kuvutia vipimo vya shida kubwa za wakati huo na mwelekeo ambao suluhisho lao linapaswa kutafutwa.

Pamoja na mawazo hayo Patriaki anampongea mkurugeniz huyo na , anashirikia wake wahudumu wotekwa maadhimisho ya heri  na kuwatakiwa mema katika  mwendelezo wenye matunda wa ushuhuda mzuri na huduma kwa Kanisa, kwa taalimungu na kwa tamaduni kupitia hiyo. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, upendo wa Mungu Baba na ushirika wa Roho Mtakatifu uwe pamoja na wewe na wale walio karibu nawe.

03 December 2020, 17:07