Tafuta

Vatican News
2020.09.21 Askofu Mkuu Richard Gagnon wa Winnipeg, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Canada. 2020.09.21 Askofu Mkuu Richard Gagnon wa Winnipeg, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Canada. 

Canada:Noeli 2020 ni kipindi muafaka ili kuwa bora!

Janga la covid-19 limeweka bayana udhaifu na matatizo yasiyo na mwisho,lakini Noeli ni kipindi muafaka kwa ajili ya kuweza kuondokana tukiwa bora.Bwana anaweza kuleta mabadiliko ndani mwetu.Ni katika ujumbe wa Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana 2020 uiloandikwa na Askofu Mkuu Richard Gagnon,Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Canada.

Na Sr.Angela Rwezaula-Vatican.

Noeli ni kipindi kilicho barikiwa na muafaka katika maisha yetu ambamo Bwana anaweza kutuletea mabadiliko ya ndani mwetu na kutufanya kuwa wafuasi walio bora zaidi. Ndiyo moyo wa ujumbe wa Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana kwa 2020  ulioandikwa na Askofu Mkuu Richard Gagnon, wa Jimbo katoliki la  Winnipeg na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Canada (Cccb). 

Janga la ulimwengu katika miezi ya mwisho limejionesha kutokuwa na uhakika na matatizo yasiyo na mwisho na ambayo yameoneshwa hata kuahirishwa maadhimisho ya liturujia kwa umma na kuanguka kwa kiasi fulani maisha ya kila siku katika maparokia na majimbo. Na zaidi umejionesha daima utambuzi wa janga hili jinsi binadamu kiukweli alivyo muathirika na yuko katika hali ngumu mbele ya majanga ya asili na magonjwa.  Pamoja na hayo yote, anaongeza Askofu Mkuu Gagnon, udhaifu na hofu pamoja na kuwa sehemu yetu ya maisha lakini si yote kwa sababu, shukrani kwa tafakari ya kina juu ya maisha yetu binafsi, familia na uhusiano na kwa njia ya sala na Neno la Mungu kila kitu kinapata maana yake.

Katika miezi hii ngumu, anasisitiza tena Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Canada (Cccb), imeruhusu kwa kile kiitwaco wakristo mafichoni au waliobatizwa bila kuweka imani yao katika matendo, kuweza kuthamanisha kwa kiasi kikubwa imani, huku wakijifungulia fursa mpya za kujenga kwa upya Kanisa kwa njia mpya na kwa msaada wa Bwana. Kwa kutazama liturujia za Noeli, Askofu Mkuu Winnipeg amesitiza jinsi gani zinazungumza katika mwanga mpya na tumaini jipya ambalo limezaliwa ulimwenguni kwa ajili ya kuangaza giza. Pamoja na utambuzi kuwa tangazo la utukufu wa kuzaliwa kwa Mtoto Yesu hakuwa ndiyo mwisho wa vivuli vilivyopo ulimwenguni, lakini Askofu Mkuu anabainisha kwamba tumaini la Noeli ambalo ni mwanga wa Bethlehemu uongoze njia zetu kuelekea upyaisho wa maisha ya kweli ya kikristo.

25 December 2020, 11:56