Tafuta

Vatican News
2019.04.26 vurugu za nyumbani, manyanyaso ya nyumbani 2019.04.26 vurugu za nyumbani, manyanyaso ya nyumbani  (©doidam10 - stock.adobe.com)

Australia:Noeli 2020,kuangazia mitindo mipya ya utumwa na waathirika wake!

Utume wa kisimisonari nchini Australia ulianzishwa jijini Sydney kunako mwaka 1847,na ambao unatoa mchango wa fedha na kusaidia mipango na shughuli mbali mbali zinazoendeshwa na Kanisa barani Afrika,Asia,Australia na Amerika ya Kusini katika muktadha wa mafunzo ya kiroho,huduma ya kichungaji na mafunzo,afya,huduma za usafi na mipango ya kilimo.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Utume wa Kimisionari ni kitengo cha Kurugenzi ya Kitaifa ya Shughuli za Kipapa za Kimisionari nchini Australia,  ambacho kimewaalika Jumuiya ya waamini nchini humo kukaribia Siku Kuu ya Noeli hasa kwa kujikita katika tafakari juu ya mantiki ya utumwa mamboleo na biashara ya binadamu. Haya yamezungumzwa na Francis Leong, Mkurugenzi wa kijimbo wa Utume wa Kimisionari huko Perth akizungumza na shirika la habari za kimisionari Fides. Kwa mujibu wa Leong amesema “kadiri ya wao watakavyoweza kuwa mwanga wa kupeleka mbele mada hiyo ndivyo itakuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na mabadiliko

Mada wanazo chagua kila mwaka, kwanza zinatafakari kila hali na si tu katika kuiga, bali kuwawezesha kutoa ushawishi wa ndani na kuwaalika kujikita katika matendo ya dhati. Mada hizi zinahusiana kwa upande mmoja wenye kivuli au zenye kubeba tumaini zaidi kama vile la  Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana na kwa maana hiyo kuweza kuwa kiini cha uzoefu kwa walio pembezoni, waliokandamizwa na waathirika wa ulimwengu leo hii. Vile vile mada ya utumwa mamboleo, ambayo imechaguliwa na kitengo hiki cha Utume wa Kimisionari  kuwa  tafakari ya Siku kuu ya Noeli, imezungumziwa hivi karibuni katika mkutano kwa njia ya mtandoa kwa ushirikiano na Chuo Kuu cha Mama Yetu na Shirika la Waoblati wa Maria Mkingiwa dhambi ya Asili.

Mkutano huo ulikuwa na mada ya Mtumwa ni dada yangu, mtumwa ni kaka yangu ambao ulifanyika katika kujaribu kutoa jibu la wito wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Australia kwa ajili ya kuhamasisha zaidi utambuzi na kuheshimu mada hii.  Papa Francisko mara nyingi  anasema kuwa Uinjilishaji wa dhati hauwezi kupatikana kwa mijadala bali kwa kuonesha jambo ambalo ni zuri. Katika kutekeleza hili, mada hizi ziliandaliwa kwa njia ya tukio la kiliturujia kwa muziki mtakatifu, huku wakiongozwa na kusoma masomo na kusikiliza historia  wakitoa umakini juu ya jeraha la utumwa mamboleo na lile la biashara ya binadamu!

PMS ya Australia inasaidia mipango ya baadhi ya mashikirika ya watawa, hawa wale wanaojikita kusaidia wanawake na watoto wahanga wa biashara hii mbaya na ambao wanawezesha kuwa na fursa za ujenzi mpya wa maisha yao na mafunzo ya kitaaluma. Utume wa kisimisonari ulianzishwa jijini Sydney kunako mwaka 1847, na ambao unatoa mchango wa fedha na kusaidia mipango na shughuli mbali mbali zinazoendeshwa na Kanisa barani Afrika, Asia, Australia na Amerika ya Kusini katika muktadha wa mafunzo ya kiroho, huduma ya kichungaji na mafunzo, afya, huduma za usafi na mipango ya kilimo.

25 December 2020, 12:32