Tafuta

Askofu mkuu Tarcisius Gervazio Ziyaye wa Jimbo kuu la Lilongwe, Malawi amefariki dunia tarehe 14 Desemba 2020 huko Namibia ambako alikuwa anapatiwa matibabu. Askofu mkuu Tarcisius Gervazio Ziyaye wa Jimbo kuu la Lilongwe, Malawi amefariki dunia tarehe 14 Desemba 2020 huko Namibia ambako alikuwa anapatiwa matibabu.  

TANZIA: Askofu mkuu Tarcisius Zizaye Amefariki Dunia! Jembe!

Askofu mkuu Tarcisius G. Ziyaye alizaliwa tarehe 19 Mei 1947. Tarehe 14 Agosti 1977 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 26 Novemba 1991 akateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katokliki la Dedza, Malawi na kuwekwa wakfu tarehe 23 Mei 1992. Tarehe 4 Mei 1993, akateuliwa kuwa Askofu mkuu mwandamizi Jimbo kuu la Lilongwe na kusimikwa rasmi tarehe 11 Novemba 1994.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Baraza la Maaskofu Katoliki Malawi, linasikitika kutangaza kifo cha Askofu mkuu Tarcisius Gervazio Ziyaye wa Jimbo kuu la Lilongwe, kilichotokea tarehe 14 Desemba 2020 huko nchini Namibia ambako alikuwa anapatia matibabu. Taarifa iliyotolewa na Padre Henry Saindi, Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Malawi inabainisha kwamba, mipango ya mazishi inaendelea na mara tu itakapokamilika, watu wa Mungu ndani na nje ya Malawi, watapewa taarifa rasmi! Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Tarcisius Gervazio Ziyaye wa Jimbo kuu la Lilongwe alizaliwa tarehe 19 Mei 1947 huko Khombe, Malawi.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 14 Agosti 1977 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 26 Novemba 1991 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu wa Jimbo Katokliki la Dedza, Malawi na kuwekwa wakfu tarehe 23 Mei 1992 . Tarehe 4 Mei 1993, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteua kuwa Askofu mkuu mwandamizi wenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Lilongwe na kusimikwa rasmi tarehe 11 Novemba 1994. Tarehe 23 Januari 2001 kwa mara nyingine tena, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Blantyre, Malawi.

Na hatimaye tarehe 3 Julai 2013 Baba Mtakatifu Francisko akamateuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Lilongwe, Malawi. Na tarehe 14 Desemba 2020, Kristo Yesu, Hakimu mwnye haki na huruma, amemwita kwake, ili aweze kumkirimia usingizi wa amani. Askofu mkuu Tarcisius Gervazio Ziyaye wa Jimbo kuu la Lilongwe ataendelea kukumbukwa sana kutokana na mchango wake kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu katika Nchi za Ukanda wa AMECEA.

 

 

14 December 2020, 10:22