Tafuta

2020.07.28 -Askofu Mkuu  Miguel Cabrejos Vidarte,Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Amerika Kusini na wa Baraza la Maaskofu nchini Peru. 2020.07.28 -Askofu Mkuu Miguel Cabrejos Vidarte,Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Amerika Kusini na wa Baraza la Maaskofu nchini Peru. 

Amerika ya kusini Celam:Kpaumbele cha kulinda maisha na hadhi ya familia

Inahitaji kulinda maisha na hadhi ya familia.Ili kuweza kuwa familia ya kweli ya binadamu,lazima kutoa kipaumbele cha mshikamano,huruma,upendeleo wa wenye kihitaji zaidi na kwa namna hiyo kuweza kuonesha udugu wa ulimwengu na kutembea katika nyayo za haki na amani.Ni katika ujumbe wa Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Amerika ya Kusini(Celam)alioutoa katika Siku Kuu ya Familia Takatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Askofu Mkuu Miguel Cabrejos Vidarte, Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Amerika ya Kusini (CELAM) ametoa wito wa nguvu wa kulinda maisha na hadhi ya familia. Wito huo kutoka katika ujumbe wake, umesikika na kusambazwa  siku ya Dominika  tarehe 27 Desemba 2020,  wakati Mama Kanisa anaadhimisha Siku kuu ya Familia Takatifu ya Yesu Maria na Yosefu.

Kiungo cha kifamilia katika historia kinateseka na majanga mengi

Katika wakati wa kihistoria ambamo kiungo cha kifamilia kinajikuta kinakabilina na athari ngumu za janga la Covid-19, na zaidi janga la umaskini, anasisitiza  kiongozi huyo wa Kanisa  “ majanga mengi yanaumiza hadhi ya watoto wa kike na kiume wa Mungu”. Kwa namna ya pekee, Rais wa Celam anayataja  kama vile  “vurugu, unyonyaji, biashara ya binadamu na ubaguzi ambao unafanywa uzoefu na familia nyingi hata wahamiaji au baadhi ya wengine ndani mwao.”

Tuthibitisha upendeleo na kuishi kama familia Takatifu ya Nazareth

Kufutia na hiyo Askofu Mkuu Cabrejos anaandika: “Katika siku ambayo tuaadhimisha Siku kuu ya Familia Takatifu, tuthibitishe uchaguzi wetu kuwa mwingine wa kulinda maisha na hadhi ya familia nyingi za Amerika ya Kusini na Caribbien, kwa kukumbuka kwamba hata familia ya Nazareth ilishirikisha hali hii ngumu ya kuathirika hasa ilipokimbilia huko Misri kwa ajili ya kulinda maisha ya mtoto wao”. Hata hivyo katika ujumbe huo aidha amethibitisha juhudi za Celam kwa ajili ya kiungo cha kifamilia na kusisitiza juhudi za  Kanisa na umuhimu wa kutembea nao katika umoja, kusikiliza kilio chao huku wakihamasisha utamaduni wa maisha, kufanya kazi katika kutambuzi na kuheshimu haki zao”.

Familia ya kweli lazima kutoa kipaumbele cha mshikamano na uhuruma

Katika mtazamo huo ametaja  sehemu ya Wosia wa Baada ya sinodi wa “Amoris Laetitia”, uliotiwa sahini na Papa Francisko mnamo  2015, ambapo Askofu Mkuu Cabrejos amesisitiza kuwa familia ni  shule ya dhati ya Injili na Kanisa dogo la nyumbani, mahali ambamo ndani mwake, wanaishi na kuonesha thamani za upendo na udugu, kuishi kwa pamoja na kushirikishana, kuwa na umakini na kutunza mmoja na mwingine. Ili kuweza kuwa familia ya kweli ya binadamu, lazima kutoa kipaumbele cha mshikamano, huruma, upendeleo wa wenye kihitaji zaidi,  kwa namna hiyo kuonesha udugu wa ulimwengu na kutembea katika nyayo za haki na amani.

27 December 2020, 11:41