Tafuta

Maaskofu wanatoa wito wa upatanisho na umoja wa kitaifa nchini Zimbabwe. Maaskofu wanatoa wito wa upatanisho na umoja wa kitaifa nchini Zimbabwe. 

Zimbabwe:Upatanisho na umoja wa kitaifa ndiyo wito wa maaskofu

Katika barua ya kichungaji ya Baraza la Maaskofu nchini Zimbabwe,katika fursa ya kuanza kwa kipindi cha Majilio tarehe 29 Noemba ijayo wanatoa wito kwa waamini katika mkatadha wa upatanisho na umoja kitaifa."Bwana Yesu anakuja kati yetu ili kutupyaisha.Ujio wake pia ni ujio wa mambo mapya,mawazo mapya,upyaisho wa matumaini katika Yeye na wengine na uwezo wa kutenda mema",wanaandika Maaskofu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Upatanisho na umoja wa kitaifa ndiyo wito wa uliozinduliwa na Baraza la Maaskofu nchini Zimbabwe (Zcbc) katika barua yao ya kichungaji, iliyotolewa katika fursa ya mwanzo wa kipinidi cha Majilio,  Dominika tarehe 29 Novemba. Kwa namna ya pekee Maaskofu katika barua hiyo wanawashauri waamini kwenda kukutana na mwingine, zaidi ya mipaka ya kijamii na kisiasa, na kusaidiana pamoja na utunzaji wa kazi ya uumbaji. Maaskofu nchini Zimbabwe wanaandika kuwa “Bwana Yesu anakuja kati yetu ili kutupyaisha. Ujio wake pia ni ujio wa mambo mapya, mawazo mapya, upyaisho wa matumaini katika Yeye na wengine na uwezo wa kutenda kwa pamoja ili tuweze kuwa na imani ya pamoja na kujikuta tukiwa pamoja zaidi ya mipaka kijamii na kisiasa”.

Bwana ameumba ili watu waishi kama ndugu

Katika mtazamo huo, hata hivyo maaskofu wanapongeza jitihada hizo za kuelekea umoja na mapatano, wakishauri sekta za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kidini kusikiliza Neno la Mungu. Kiini hasa kwa maaskofu hawa ni wito kwa viongozi wa serikali ili kweli waoneshe ukarimu kwa vyama vya upinzani kwa namna kwamba Majilio yanaweza kurudisha matumaini kwa watu wanaoteseka. Kwa mujibu wa Maaskofu wanasema “ siasa isiyo na upendo haiwezi kupelekea ustawi wa pamoja na upendo wa kisiasa kwa ajili ya taifa na wema wa pamoja unaonekana kwa namna ambayo wanahuduma wasio na uwezo. “Kwa hakika Mungu aliuumba binadamu wote sawa, haki sawa, wajibu na hadhi na kuwaita waishi pamoja kama ndugu kaka na dada; kwa pamoja na kutambua hadhi na haki za mwingine ambazo ni msingi wa kitaifa” wanasisitiza Maaskofu wa Zimbabwe.

Ulinzi wa mazingira:Unatakiwa uongofu wa ekolojia 

Kwa kile kinachotazama ulinzi wa mazingira, Maaskofu katoliki wa Zimbabwe wanatazama Waraka wa Papa Francisko  “Laudato si’  kuhusu utunzaji wa mazingira, na kuwaalikwìa waamini wawe na uongofu wa kweli wa ekolokia ili kusitisha  kwa hakika uharibifu wa mazingira. Mgogoro wa sasa wa mazingira, wanasema, unawatazama watu wote na ndiyo unazidi kuongezea umaskini. “Masilahi ya kibiashara na matumizi ya wateja, kwa sababu ya unyonyaji na uharibifu wa mazingira unaathiri maisha ya watu na haki yao, iliyotolewa na Mungu, kufurahia kile kilichoumbwa kwa wote”. “Wakati wa Majilio  mtazamo wa Wakristo lazima pia uelekezwe kwa kile kinachoweza kuzuia uharibifu wa nchi, ambayo ni kito cha Afrika”, wanasema Maaskofu. Ujumbe wa maaskofu haukusahau janga la Covid-19 ambalo, nchini Zimbabwe, limesababisha visa karibu elfu 9: 2020 na kwamba umekuwa  mwaka mgumu, wanasema maaskofu ambapo wanaalika waamini ili kwamba katikati ya mipango ya kufufua,  lazima waweke maslahi kwa wote  kutokana na dharura. “Lazima tusaidiane. Namna ya kuwa mkarimu kwa wengine ni ishara ndogo ya kufanya”. Katika mantiki hii, Kanisa linatumaini kwamba,  katika mwanzo wa majilio waamini wataweza kuanza tena kushiriki tena mwili katika sherehe za liturujia kwa sababu hii itasaidia kukuza ushirikiano wa kitaifa”. Hatimaye maaskofu wanahimiza kufikiria kwa ubunifu, vyema, "kwa hakika juu ya siku zijazo tnazoota  na tunachotaka ili kujenga Zimbabwe tunayoitaka”.

19 November 2020, 18:19