Tafuta

Kanisa nchini Ukranine Kanisa nchini Ukranine 

Ukraine:siku ya maskini.Kanisa la Kigiriki-Katoliki kampeni ya msaada wa chakula!

Maaskofu wa Kigiriki-katoliki nchini Ukraine wamewaalika waamini wote nchini mwao kushiriki katika kampeni mpya ya ufadhili inayoongozwa na kauli mbiu “wape maskini chakula” kwa namna ya pekee watu ambao wanaendelea kuteseka kwa sasa kutokana na janga la virusi vya corona au Covid-19.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tunataka kuwa Kanisa daima linalotoka nje kwa ajili ya kuhudumia: huo ndiyo mpango wetu, ndoto yetu na kiongozi wetu. Awali ya yote lazima kuhudumia wale ambao wanaishi karibu zaidi na hawapati  umakini wowote, msaada na kutiwa nguvu. Katika maneno hayo Maaskou wa Kigiriki -katoliki nchini Ukraine wamewaalika waamini wote nchini mwao kushiriki katika kampeni mpya ya ufadhili inayoongozwa na kauli mbiu “wape maskini chakula” kwa namna ya pekee watu ambao wanaendelea kuteseka kwa sasa kutokana na janga la virusi vya corona au Covid-19.  Mpango huo umeandaliwa na Kitengo kwa ajili ya huduma ya kijamii na ambao utazinduliwa tarehe 15 Novemba, sambamba na Maadhimisho ya Siku ya IV ya Maskini duniani 2020, ilipondekezwa na Papa Francisko. Hata hivyo mpango wao ni tunda la  sinodi  ya maaskofu wa Kigiriki katoliki nchini Ukraine (Ugcc), kwa mujibu wa taarifa zilizotangzwa kwenye tovuti vya Baraza hilo (Ugcc.)

Katika ujumbe wa kichungaji uliopewa kichwa “Utabaki na kitu kimoja tu: kile ulicho wapa maskini!”, Sinodi ilikuwa inakumbuka kwamba Kanisa la Kigiriki-Katoliki nchini Ukraine lina tamaduni ndefu ya mshikamano ambayo ilikuwa dhahiri hasa wakati wa majaribu.  “Mioyo ya Waukraine katika ulimwengu huru walihisi maumivu na ukandamizaji waliouishi wagiriki- katoliki chini ya utawala wa kikomunisti katika nchi yao asili. Kuanzia  na diaspora, maombi ya kila wakati yametolewa kwa  ajili ya kaka na dada wanaoteswa katika imani na kuwapa mkono wa mshikamano wenye huruma na ukarimu wetu hata baada ya Kanisa kuachwa katika maandaki”,  wanaandika maaskofu hao.

Ushirikiano wa  Kanisa la Ukraine leo hii  unalipa kwa kutuma makuhani wake mwenyewe katika  jamuiya za watu wanaoishi katika diaspora nyingine. “Na ni juu ya uzoefu huu wa thamani wa mshikamano na kuungwa mkono kwamba Kanisa la Kiukreni lazima lijengwe sasa na baadaye”, viongozi hao wamesisitiza. Kwa njia hiyo wanatoa mwaliko wa kuendelea kuwahudumia wahitaji, ambao wanazidi kuwa wengi nchini Ukraine pia kwa sababu ya chaguzi mbaya za kiuchumi ambazo zimesababisha  umaskini wa watu kuzidi kuadhibiwa na vita  vya mashariki mwa nchi na sasa janga la virusi vya Corona . “Hakuna hata mmoja wetu ni maskini hivi kwamba hatuwezi kushiriki chochote na wengine. Ni ugumu wa mioyo tu unaoweza kutuzuia kufanya hivyo. Moyo ambao una chembechembe za mawazo na hisia za Kristo hauwezi kukosa kusema 'Samahani kwa watu hawa' mbele ya maumivu na mateso” wamehitimisha maaskofu hawa.

13 November 2020, 17:22