Tafuta

Askofu Mkuu  Auza Balozi wa Kitume nchini Uhispainia Askofu Mkuu Auza Balozi wa Kitume nchini Uhispainia 

Uhispania:Ask.Mkuu apeleka salam za pole kwa niaba ya Papa

Katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza Maaskofu nchini Uhispania (CEE) tarehe 16 Novemba 2020,Balozi wa Kitume nchini Uhispania na ufalme wa Andorra,Askofu Mkuu Bernardito Auza, amepeleka salam za rambi rambi kwa niaba ya Papa Francisko kwa watu wote wa Uhispania waliofiwa na wapendwa wao kwa sababu ya janga la Covid-19.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza Maaskofu nchini Uhispania (CEE) tarehe 16 Novemba 2020, umefanyika kwa njia ya mtandao na washiriki wa moja kwa moja walikuwa ni maaskofu 38 tu, katika makao makuu huko Madrid. Na wajumbe wengine wa Baraza walifuatilia moja kwa moja kwa njia ya mtandao ili kuhakikisha usalama na kuzuia uwezekano wa maambukizi. Katika Ufunguzi huo, Balozi wa Kitume nchini Uhispania na Ufalme wa Andorra, Askofu Mkuu Bernardito Auza, amepeleka salam za rambi rambi kwa niaba ya Papa Francisko kwa watu wote wa Uhispania waliofiwa na wapendwa wao kwa sababu ya janga la Covid-19.

“Ninawatangazia hisia za ukaribu za salam za Papa ambaye, ninayo heshima ya kumwakilisha nchini Uhispania, kwa namna ya pekee, wagonjwa wa janga hili, na kama ilivyo salam za rambi rambi na kuwahakikishia sala za  Papa kwa familia zote ambazo zimepatwa na mkasa wa kupoteza wapendwa wao” alisema Askofu Mkuu Auza. Balozi wa Kitume amekumbusha kuwa “tabia na mtindo wa Papa ambaye shughuli za kuingilia kati katika usaidizi, hazikomi hata katika kipindi hiki kigumu cha mantiki ya Covid-19, anawatia moyo maaskofu wa uhispania ili kuongeza juhudi zaidi katika kazi yao.

Kwa namna ya pekee Askofu Mkuu  Auza emependelea kuonesha utambuzi wake hasa wa uhusiano wa kipapa na makuhani, watawa na watu wote wa Mungu wa kujitolea ambao wanaendelea katika utume wao na wametafuta kwa namna moja au nyingine ya ubunifua ili kawafikia waamini katika kipindi hiki cha janga la corona. Amwapa pole sana mapadre ambao katika kuendeleza huduma yao ya kichungaji ya kutoa sakramenti na msaada kwa waamini, wameambukizwa na virusi vya corona, wengine wamepona, lakini wengine wamekufa.

Askofu Mkuu Auza amewakumbuka kwa shukrani kubwa sana, watu wote wahudumu wa Afya, madaktari, wauguzi na makundi yote ya taaluma ya afya ambao kila siku wanatoa huduma zao muhimu. “Jitihada hizi zinastahili utambuzi kwa jamii nzima ambapo tunayo furaha kubwa kuungana nao katika hali hii ambayo hatujuhi kudumu kwake. Na ndiyo maana Papa anatukumbusha tangu mwanzo kuwa na ubinifu wa kusaidia wengine, lakini pia kwa ajili ya kuhifadhi ya kesho ili iweze kuwa bora kwa sababu itatusaidia".

17 November 2020, 15:03