Tafuta

Kimbunga kikali ( Goni) kilipiga nchini Ufillippine. Kimbunga kikali ( Goni) kilipiga nchini Ufillippine. 

Ufilipino-dhoruba Goni:Caritas yaomba msaada kwa ulimwengu kwa ajili ya waathirika!

Mkurugenzi wa Caritas nchini Ufillipino ametoa ombi kwa unyenyekevu kwa watu wote wenye mapenzi mema ulimwenguni kuwa na ukarimu wa kusaidia wale walioathiriwa na kimbunga kikali kiitwacho Goni nchini humo kilichotokea Jumapili,tarehe Mosi Novemba na kusababisha madara makubwa mno.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Monsinyo Jose Colin Bagaforo, Mkurugenzi wa Caritas nchini Ufilipino akizungumza na shirika la habari za Kanisa ameomba kwa unyenyekevu ili pawepo na matendo ya dhati ya ufadhili, ukarimu na huruma kutoka wote. Amesema hayo akizindua ombi la kimataifa ili kusaidia wale walioathiriwa na Kimbunga kikali kiitwacho Goni (au Rolly), chenye nguvu zaidi cha mwaka 2020, ambacho kilipiga kusini mwa Luzon siku ya Jumapili, tarehe Mosi Novemba na kikasababisha vifo vya watu wasiopungua 20 na kuathiri mamia ya maelfu ya Wafilipino.

Hadi sasa watu 390,000 wamehama makazi yao na karibu 347,000 bado wako katika vituo vya mapokezi ya muda. Katika picha za  kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha vijiji vilivyozama na maji ya mafuriko, nyumba kuharibiwa, miti iliyokatwa na uchafu. Zaidi ya nyumba 300 zilizikwa chini ya maporomoko ya udongo katika mkoa wa Albay, zilizoathiriwa vibaya na dhoruba hiyo.

Monsinyo Bagaforo, akisisitiza jinsi kimbunga kikali ambacho kitazidisha umasikini mkubwa kwa jamii ambazo tayari zimekwisha jaribiwa vikali na janga la corona alisema kwamba timu za Kanisa zinazoingilia kati kwa haraka zimepelekwa mara moja na watu wa kujitolea na vikundi vya majimbo wanaleta misaada kwa wakimbizi kutoka mparokia mbalimbali.

Jimbo kuu la Manila limetenga takribani  milioni moja ya kwanza kusaidia mahitaji ya haraka ya jamuiya zilizoathiriwa. Kwa kuongezea, mkurugenzi mtendaji wa Caritas Jimbo Kuu la Manila, Padri Anton Pascual, ametangaza kwamba Jimbo kuu la Caceres na majimbo ya Virac, Daet, Gumaca na Legazpi,  kila mmoja atapokea pesa 200,000 za nchi hiyo.Katika nyakati hizi ngumu, ambazo tunamwinulia Mungu wetu kila kitu, amesema Padre Tony Labiao, katibu mtendaji  a Caritas Ufilippino  kwamna tunajua pia kwamba kila mtu ulimwenguni ataweza kusikia maombi yetu na kutuma msaada”..

03 November 2020, 15:24