Tafuta

Caritas ni chombo cha Kanisa kwa ajili ya mahitaji ya wenye shida mbali mbali. Caritas ni chombo cha Kanisa kwa ajili ya mahitaji ya wenye shida mbali mbali. 

Tanzania:Mkutano Mkuu wa Caritas:Caritas ni zaidi ya NGOs,ni utume wa upendo wa Kanisa!

Neno Caritas,ni upendo ambao kulingana na dhana ya Kikristo unaunganisha waaamini na Mungu na kwa kila mmoja kupitia Mungu,hivyo inaweza kuwa ari,bidii,tendo zaidi ya hisani.Ni mitindo ambayo kwayo mtu hutangaza upendo kwa mtu wa Mungu na kwa jirani kwa sababu ya kumpenda Mungu.Amefafanua Askofu Mkuu Askofu Mkuu Thaddeaus Ruwai'chi OFM Cap,wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa Caritas nchini Tanzania.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Caritas ilizunduliwa kwa ajili ya utume wa Kanisa, yaani kwa ajili ya utume wa pendo. Sio shirika kama lisilo la kiserikali(NGOs). Amesema hayo hivi karibuni  Askofu Mkuu Jude Thaddeaus Ruwai'chi OFM Cap,; wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa Caritas nchini Tanzania, huko  Dar es Salaam. Kwa mujibu wa maelezo ya Tovuti ya Amecea, Askofu Mkuu katika hotuba yake amesisitiza kuwa kila mjumbe wake lazima aelewe uhitaji wa maana ya utume huo. Neno Caritas, ni upendo ambao, kulingana na dhana ya Kikristo, unaunganisha waaamini na Mungu na kwa kila mmoja kupitia Mungu, hivyo inaweza kuwa ari, bidii, tendo la hisani, mitindo ambayo kwayo mtu hutangaza upendo kwa mtu wa  Mungu na kwa jirani kwa sababu ya kumpenda Mungu. Ni kitendo cha kishujaa cha hisani. Na katika taalimungu  Katoliki, tendo  la hiari linalotolewa na waamini na kwa Mungu. Ni upendo wa dhati kwa jirani ambao umeoneshwa juu ya yote kupitia matendo ya huruma kwa wenye kuhitahi. Kwa maana hiyo  ndiyo lengo kuu la  Kanisa. Kuhudumia wahitaji hasa maskini na kujibu maombi yao  yanapotokea kutokana na majanga. Kutokana na kutafsiri huko Caritas haiwezi kubadilishwa kuwa kama aina ya shirika lisilo la kiserikali (NGOs), ni zaidi ya hilo kwani  ni chombo cha upendo cha Kanisa na kinachoangazia zaidi ukaribu wa mahitaji muhimu ya ndugu.

Askofu Mkuu Ruwai'chi vile vile amewaalika wakurugenzi wa majimbo yote kufanyia kazi mkakati wa kuweza kujibu mahitaji yaliyowekwa mbele na majanga ya asili na umaskini huku akigusia hasa suala la dharura ya sasa ya kiafya. “Miezi michache iliyopita Covid-19 imeyumbisha ulimwengu hata chi yetu. Lazima kuwatia moyo watu wafuate mwongozo wa kiafya, ushauri uliotolewa na wataalam ili kuepuka kuabukizwa”. Akiendelea hata hivyo amesema “Covid-19  imeleta umaskini wa kutisha na wasiwasi. Umewafanya watu wasiwe na usalama kwa ajili ya wakati wao ujao na usio na furaha”. Mbele ya chanagmoto hizi, lazima kujiuliza, “ni majibu gani tumetoa? Ni wangapi tumehusika? Wajibu wetu ni upi? Hii ni kwa sababu Caritas ina utume mmoja wa kipekee ambao ni wa  huruma na upendo ambao tunapaswa kuelewa kuwa inapobainisha mkakati mmoja ambao sisi tumeitwa, basi lazima kutafuta majibu kwa wakati, majibu ambayo yanakwenda zaidi ya upeo wa majanga hayo”, mesisitiza Askofu Mkuu wa Dar es Salaam.

Katika Mkutano huo hata hivyo  sauti nyingine  imetoka katika hotuba ya Makamu Katibu  Mkuu wa Baraza la Maakofu Tanzania (TEC), Padre Daniel Dulle ambaye katika kuwapokea wawakilishi hao amewashuri wafanyie kazi mkakatati wa kuingilia kati ambao uweze kusaidia maskini kwa muda mrefu huku akisisitiza na kuunga mkono yaliyosema kwamba kutokana na umaskini lazima kutambua kuwa Caritas sio shirika lisilo la kiselikali (hisani, kazi yake inapaswa iwe aminifu na kwa namna ya kuwa sababu ya amani na masaada  wa ubinamu kwa waathirika wa majanga na matatizo mengine”. Na kwati wa kufunga Kazi hiyo Askofu Mkuu Ruwai'chi amekumbisha  kuwa “utume wa Caritas unatazama wakatoliki wote; kila mtu mbatizwa anaalikwa kusaidia jirani, hata maskini. Ikiwa tutaweza kufika lengo hilo, ona maana tume wetu utakuwa na mafanikio.”

24 November 2020, 16:17