Tafuta

CANON LAW :SHERIA ZA KANISA KUTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI CANON LAW :SHERIA ZA KANISA KUTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI 

Tanzania:Mkusanyo wa Sheria Kanoni umetasfiriwa kwa lugha ya Kiswahili!

Baraza la maaskofu nchini Tanzania tarehe 17 Novemba 2020 wamepokea vitabu elfu 4 vya Sheria za Kanisa(Canon Law)au kwa jina “Mkusanyo wa Sheria Kanoni”vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.Vitabu hivi vilianza kutafiriwa na kamati iliyoundwa na Maaskofu tangu mwaka 2013 na kukamilika rasmi 2020.Ni maelezo kutoka kwa Padre H.Mchamungu,Katibu Mkuu wa Tume ya sheria za Kanisa ya TEC na Mwalimu wa Sheria za Kanisa,Seminari Kuu ya Segerea.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Imechukua muda wa miaka saba, lakini hatimaye miaka hiyo imewezesha kutoa matunda. Ni Mkusanyo wa Sheria Kanoni kwa  lugha ya kiswahili, (Canon Law) au (codex iuris canonici) ambayo kwa sasa inapatikana, shukrani kwa kikundi cha watafsiri mbali mbali chini ya uongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Tanzania (Tec). Hayo ni kutoka katika maelezo ya Katibu Mkuu wa Tume ya sheria za Kanisa ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padre  Henry Mchamungu, ambaye ni mwalimu wa sheria za Kanisa katika Seminari Kuu ya Segerea Tanzania  wakati wa akiwasilisha toleo jipya  kwa njia ya video kupitia YouTube. Akiendelea kueleza amesema “kunako mwaka 2013 maaskofu  katoliki wa Tazania waliagiza sheria za Kanisa ambazo zilikuwa katika lugha ya kiingereza zitafsiriwe kwa lugha ya kiswahili ili waamini wakatoliki wapate kuzielewa kwa urahisi zaidi”.

Shughuli ya kutafsiri haikuwa rahisi ilihitaji msaada

Kiswahili hata hivyo kinazungumzwa na watu milioni 150 nchini Tanzania, Kenya, Uganda, lakini pia nchini Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, na Jamhuri ya ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Cha msingi zaidi, ili kutimiza kazi hiyo ya kutafsiri, ambayo haikuwa rahisi  wamewezeshwa na msaada wa kifedha ili kuwasaidia wajumbe hata kugharimia mikutano kutoka “Shirika la Kanisa hitaji” kwa upande wa Ujerumani pia kutoka Jimbo Kuu Katoliki la  Linz nchini Austria, ambao wamewezesha kwa kiasi kukubwa sana kufanikisha zoezi hilo la kutafsiri kwa mujibu wa Padre  Mchamungu.

 Ugawaji wa kazi ya kutafsiri sura kwa sura

Padre akiendelea kuelezea amefafanua “ni kwa jinsi gani waligawana kazi kuhusiana na maandishi ya sheria kwa namna ya pekee ilivyo nguvu na ili kupata waandishi wa maneno fulani maalum kutoka lugha moja hadi nyingine, bila kubadilisha maana yake, ambayo haikuwa kazi ndogo”. Kwa njia hiyo ili kufanikisha kazi hiyo iligawanywa katika sura: kila mshiriki wa timu alitafsiri moja na ambayo baadaye ilipitiwa kwa pamoja wakati wa mikutano kadhaa. Kila tafsiri moja ilithibitishwa na Baraza zima la Maaskofu wa Tanzania”.

Mpango wa kutafsri ulihitimishwa 2019, lakini uchapishaji ulihitaji gharama

Na hatimaye “mpango huo ulihitimishwa mnamo 2019, kwa idhini ya maaskofu katika mwezi Juni”. Lakini kwa mjibu wa Padre Mchamungu amesema kuwa uchapishaji wa mwisho ilibidi usubiri bado sababu ya ukosefu wa fedha. “Tulipokea michango, lakini haikutosha, amefafanua na kwamba wakati wa kuzungumza na wamisionari wengine wanaosimamia machapisho ya Waklaretians, tunaweza kulipa gharama kwa mafungu, kadiri ambavyo tuytapata fedha wakati wa kuuza vitabu hivyo”. Kwa njia hiyo nakala za “Mkusanyo wa Sheria ya Kanoni za Kiswahili zimefika tarehe 17 Novemba 2020 ambapo wamepokea vitabu elfu 4 vya Sheria za Kanisa (Canon Law)au kwa jina “Mkusanyo wa Sheria Kanoni” ili kuanza kuviuza katika maduka mbali mbali ya vitabu, nchini Tanzania kwa bei ya elfu 20, yenye thamani ya dola 9, pia vinapatikana makao makuu ya Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC) huko Kurasini, Dar Es Salaam.

21 November 2020, 14:58