Tafuta

Mgogoro bado unaendelea huko Armenia Mgogoro bado unaendelea huko Armenia  

Nagorno-Karabakh:mshikamano wa maaskofu wa Ubelgiji

Mshikamano wa Kanisa la Ubalgiji katika eneo la mizozo ya kivitia la Nagorno-Karabakh,hasa kwa jumuiya za kikristo za Kiarmenia.“Nyumba,hospitali na shule zimeharibiwa,kama vile maeneo ya ibada”,maaskofu wanabainisha kwamba uharibifu hauhusu mali tu,bali pia ni pamoja na vidonda vya kiroho.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Maaskofu wa Ubelgiji wanasali kwa ajili ya amani ya Nagorno-Karabakh na kuonesha wasiwasi wao kwa ajili ya vurugu katika kanda hiyo. Katika ujumbe walioulekeza kwa wakristo wa Kiarmenia, maaskofu wanaonesha mshikamano wao na msaada, wakiwa na uchungu mkubwa kutokana na waathiriwa wa migogoro, na walio wengi ni raia  ambao wamekuwa na misiba ndani ya familia zao.

“Nyumba, hospitali na shule zimeharibiwa, kama vile maeneo ya ibada, maaskofu wanabainisha kwamba, uharibifu hauhusu bidhaa za mali tu, bali pia ni pamoja na vidonda vya kiroho”. Katika ujumbe wao, maaskofu wa Ubelgiji wanaungana na maombi ya Papa ambaye katika wiki za hivi karibuni aliomba  amani ya kudumu kwa ajili ya eneo hilo la  Nagorno-Karabakh.

Kwa mujibu wa maaskofu wa Ubelgiji wanaonyesha mshikamano na jamuiya za Kikristo za Armenia ambazo uhamisho unaogopwa. “sitisheni mapigano nakuwa na  makubaliano ya amani yaliyosainiwa hivi karibuni ambayo lazima yawe kama wito na sio tu kukomesha vurugu lakini pia uwezekano wa Wakristo kuishi kwa amani katika nchi za mababu zao, wakiheshimu utamaduni wao wa Kikristo.”

17 November 2020, 14:36