Tafuta

Maaskofu wa Ethiopia wanaomba uwepo mchakato wa amani kati ya Asmara na Tigre ili kuepuka vita visivyo na maana. Maaskofu wa Ethiopia wanaomba uwepo mchakato wa amani kati ya Asmara na Tigre ili kuepuka vita visivyo na maana. 

Maaskofu Ethiopia wataka amani kati ya Asmara na Tigre!

Wito wa aaskofu kwa ajili ya kutafuta suluhisho la amani katika mgogoro kati ya Asmara na Mko wa wa Tigrè umetolewa na Maaskofu nchini Ethiopia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wito mzito umetolewa kwa pande zote mbili ili kusuluhisha kati yao ile mitafaruko kwa namna ya urafiki na katika roho ya kuheshimiana na imani ya pamoja. Wito huo umezinduliwa tarehe 4 Novemba 2020 na Sekretaritei Katoliki ya Ethiopia (ECS), wakati Nchi nchi inapulizwa na upepep wa matukio ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mara baada ya maamuzi yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kutangaza dharura ya Mkoa wa Tigrè na kuanzishwa mashambulizi ya kijeshi.

Mahusiano kati ya Addis Ababa na Macallè, mji mkuu wa Mkoa wa Tigre yanalenga kusuluhisha serikali ya Abiy, tangu tarehe 2 Aprili 2018, lakini hali imekuwa mbaya sana katika wiki za hivi karibuni, ambapo  hivi karibuni  baada ya wanajeshi wafuasi wa  chama cha watu cha Ukombozi wa Tigre (Tplf)) kuvamia na kuchukua kituo cha jeshi. Asili ya mivutano ni madai ya TPLF ambacho, baada ya kudhibiti nguvu kwa karibu miaka thelathini, kilifutwa kazi na Waziri Mkuu mpya wa kabila la Oromo.Wao waliona kuongezeka mnamo Septemba, wakati serikali ya mkoa ilipanga uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanywa mnamo Agosti, licha ya maamuzi ya Asmara ya kuahirisha kwa sababu ya dharura ya kiafya ya Covid-19. Tangu wakati huo kumekuwa na mashambulizi ya silaha na waathiriwa kadhaa hadi hatua ya nguvu ya hivi karibuni ambayo imesababisha kutangazwa kwa hali ya hatari na kuzinduliwa kwa operesheni za kijeshi dhidi ya Tigré.

Uingiliaji wa viongozi wa kidini ili kukomesha ongezeko hilo haukuwa na faida yoyote, kama inavyothibitishwa na tangazo lililosainiwa na Kardinali Berhaneyesus Souraphiel, askofu mkuu wa Addis Ababa, ambaye ameonya juu athari ya vita mpya vya silaha nchini humo, ambavyo viliibuka mnamo 2000 vya umwagaji damu kwa  nchi jirani ya Eritrea: Ikiwa ndugu watajiua, amesema Ethiopia haitapata chochote, lakini itaangamia na haitamnufaisha mtu yeyote, kwa mujibu wa  taarifa iliyonukuliwa na shirika habari za Kanisa (la Aciafrica). Kwa maana hiyo wito kwa Waethiopia ni kutodharau mzozo unaoendelea na kuchangia katika sababu ya upatanisho, kuimarisha umoja na kuhakikisha amani na usalama.

“Kipaumbele cha nchi yetu ni kutetea utawala wa sheria” maaskofu wanasisitiza, na kuongeza kuwa “Serikali ina jukumu la kuhakikisha kuwa hatua zote zinachukuliwa ili maisha ya raia na nchi yasiwe hatarini. Kwa kuongezea, wanalaani mashambulizi ya hivi karibuni ambayo yamesababisha waathiriwa kadhaa na watu waliohamishwa makwao: “Hakuna sababu au lengo linaloweza kuhalalisha umwagaji damu”, maaskofu wanasema. Hatimaye wito kwa Wakatoliki wote ili wafuate kwa karibu hali nchini na kusali  kwa pamoja na waamini wa dini nyingine zote kwa ajili ya  amani na upatanisho. Mzozo mpya wa silaha nchini Ethiopia unahatarisha  hali ya hatari ambazo tayari zilikuwapo katika eneo hilo, ambapo kama nchi jirani za Somalia na Sudan Kusini zimekuwa hazina utulivu kwa miongo kadhaa, wakati tishio la kigaidi likiendelea kutanda. Kilicho hatarini, hasa, mchakato mgumu tayari wa utulivu na Eritrea ulioanzishwa na Waziri Mkuu Abiy baada ya kuibuka kwa nguvu na ambayo pia alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo 2019

07 November 2020, 15:36