Tafuta

Kardinali Angelo De Donatis, Makamu wa Papa Jimbi la Roma Kardinali Angelo De Donatis, Makamu wa Papa Jimbi la Roma 

Kard.De Donatis:acha tufufue azma ya ulimwengu wa udugu!

Makamu wa Papa wa Jimbo la Roma ametoa hotuba yake kwenye mkutano kuhusu Waraka wa Fratelli tutti katika fursa ya Siku ya Maskini duniani anamshukuru sana Papa kwa zawadi ya Waraka huo katika kipindi cha namna hii kigumu katika historia ya maisha yetu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika kujitambua kuwa sisi ni ndugu, tunaweza kutembea katika matumaini katika wakati huu wa majaribu, kwa utambuzi zaidi wa kuwa na matumaini ambayo hayakatishi tamaa, maana yanatufanya tuondokane na kuwa mbali na hofu na giza nene. Ni kwa njia hiyo, tutaweza kweli kutembea kidugu katika Kanisa, kati ya waamini wa kila dini na katikati ya watu wote. Ni maneno ya Kardinali Angelo De Donatis, Makamu wa Papa wa Jimbo la Roma ambaye amechagua katika Siku ya Maskini duniani Dominika tarehe 15 Novemba 2020 jioni kuungana pamoja katika kutafakari waraka wa 'Fratelli tutti' yaani wote ni ndugu.

Shukrani kindugu kwa Papa

Katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Upatanisho wa Jumba ya Lateran, Roma Kardinali De Donatis amesema kuwa ni “hazina halisi ya sanaa na yenye ukuu ambao  unashuhudia sio tu katika historia, lakini pia kuonesha uzuri wa imani inayoangaza mahali hapa ambapo kwa karne nyingi ilikuwa ni makazi ya Askofu wa Roma”. Amesisitiza akiwasilisha shughuli zilizoanzishwa kwa kipindi hiki  na wakati huo huo kutoa shukrani kubwa za kindugu kwa Papa, "kwa ajili ya zawadi maalum ya Waraka wa Fratelli tutti katika kipindi kigumu sana namna hii cha historia ya maisha yetu".

Nyayo za watangulizi

"Papa Francisko anaweka maandishi mapya baada ya mafundisho ya kitume ya watangulizi wake,amesema Kardinali na kuongeza: ambayo ni ishara za nyakati zinaoonesha uwazi kuwa udugu wa kibinadamu na utunzaji wa mazingira ndiyo njia pekee ya kuelekea maendeleo fungamani na amani, ambayo tayari ilioneshwa na Watakatifu Papa Yohane  XXIII, Paulo VI na Yohane  Paulo II”.  Aidha amesema kuwa "Askofu wetu anafunulia kwamba ametumia mambo muhimu ya uhusiano ulio wazi ambao anafanya iwezekane kutambua, kuthamini na kumpenda kila mtu kupitia ukaribu wa kimwili, mbali na umbali wa  ulimwengu ambapo alizaliwa au anapoishi na zaidi Papa wa upendo wa kindugu, wa unyenyekevu na wa furaha", amesisitiza Kardinali De Donatis.

Mwaliko wa kusoma waraka wa Fratelli tutti

Kwa kuanzia na kugundua hadhi ya kila mtu, tunachagua kufanya kuwa na azma ya kuzaliwa kati ya wote ile shauku ya ulimwengu wa kidugu, ameshauri Kardinali De Donatis, huku akishauri waamini wote kuusoma waraka huu, kwa maana ya uwajibikaji ili katika waraka huo ni kwamba, tutaweza kupata baadhi ya njia za kupitia na kuanza kuwa na mahusiano yetu ya kila siku, kwa ajili ya kujenga ulimwengu wenye haki zaidi na kidugu. Kardinali De Donatis aidha amezidi kusisitiza juu ya kulinda ushauri wa maisha ambayo Papa Francisko anabainisha kwamba hakuna yoyote anayeweza kukabiliana maisha akiwa peke yake. Kwa njia hiyo kuna haja ya kuwa jumuiya ambayo inasaidia, itusaidie na mahali ambamo tunasaidiana sisi pamoja kutazama mbele”.

Kuota ndoto kwa pamoja

Ni muhimu kuota ndoto kwa pamoja! “Na ni kweli upweke unahatarisha kupata mwanya ikiwa tunaanguki katika udanganyifu wa kuona kile ambacho hakipo wakati ndoto zinatakiwa kujengwa kwa pamoja. Hatupaswi kuogopa kuota pamoja! amesisitiza”. Hata hivyo walio  changia kutoa mada hiyo alikuwa ni Kardinali Gianfranco Ravasi, Rais wa Baraza la Kipapa la Utamaduni ambaye ametoa mada ya waraka wa Fratelli tutti, pamoja Padre Fabio Baggio, katibu msaidizi wa kitengo cha  Wahamiaji na Wakimbizi Cha  Baraza la Kipapa cha Maendeleo Fungamani watu, ambaye ametazama mada inayohusu  “Changamoto leo hii za jamumuiya ya Kanisa”, na Stefania Falasca, makamu wa  chama cha Mfuko wa Vatican wa Yohane  Paulo I, aliyejikita kufafanua mada ya Fratelli tutti katika magisterio ya Papa Francisko. 

16 November 2020, 16:00