Tafuta

2020.11-06 Kardinali Christian Tumi, Askofu Mstaafu wa Douala, baada ya kukombolewa asubuhi tarehe 6 Novemba,alitekwa nyara tarehe 5 Novemba huko Kamerun 2020.11-06 Kardinali Christian Tumi, Askofu Mstaafu wa Douala, baada ya kukombolewa asubuhi tarehe 6 Novemba,alitekwa nyara tarehe 5 Novemba huko Kamerun  

Kamerun:Kard.Tumi aliyetekwa nyara amekombolewa asubuhi!

Askofu Kleda,wa Douala amethibitisha habari za kuachiwa huru kwa Karidinali Tumi,mwenye umri wa miaka 90 aliyekuwa ametekwa nyara tarehe 5 Novemba na kikundi cha watu wenye silaha Mkoa wa Kaskazini Magharibi mwa Kamerun katikati ya mji wa Kumba na Bamenda.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kardinali Christian Wiyghan Tumi, Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu la Douala (Kamerun) na ambaye ni Kardinali wa kwanza nchini humo mwenye umri wa miaka 90, amekombolewa kutoka mikononi mwa wateka nyara, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa  Askofu Mkuu wa Douala, Samuel Kleda. Hata hivyo vyombo vya habari mahali vilikuwa vimetoa taarifa ambazo zilikuwa bado hazijathibtishwa rasmi. Wateka nyara walianza tarehe 5 Novemba mchana katika mikono ya amri za wenye silaha wakiwa katika barabara katikati ya Bamenda na Kumbo. Mamlaka ya Kaskazini Magharibi ya nchi wamethibitisha.

Waliohusika katika utekaji nyara ni pamoja na Mfalme wa Kumbo, Fon wa Nso, mwenye mamlaka ya maadili ya utamaduni. Hata hivyo Elie Smith, mmoja wa wahudumu wa karibu wa Kardinali ameweza kuwafikia watekaji nyara kwa njia ya simu ili kuwa na habari zaidi. Aliyehusika na hatua hiyo ya kijeshi ni kama jenerali wa Waazonia (yani watenganishi wa Kiingereza kutoka mkoa wenye shida wa Ambazonia, kusini magharibi mwa nchi) ambaye anajiita Chaomao, aliyekuwa mchungaji wa zamani. Habari hizi pia zimethibitishwa na familia ya mfalme wa Kumbo.

Sababu za utekaji nyara ni kutokana na Kardinali kuendelea kutia moyo kwa upande wake watoto kwenda shule. Siku chache zilizopita, kiukweli, kikundi chenye silaha kilikuwa kimewateka nyara baadhi ya walimu walioachiliwa tarehe 5 Novemba. Kwa kuongezea, mnamo tarehe 24 Oktoba watoto wanane waliuawa katika shambulio lenye silaha katika  shule ya kimataifa ya lugha mbili iitwayo Mama Francisca ambayo Papa Francisko alikuwa ameelezea uchungu wake akitoa wito wa kukomesha vurugu na kuhakikisha elimu na mustakabali wa Vijana.

Kardinali Tumi, alizaliwa tarehe 15 Oktoba 1930 huko Kikaikelaki, katika parokia ya wakati huo ya Kumbo, ambaye kwa sasa ni Jimbo katoliki na ambaye  kama askofu na baadaye kama kardinali, amekuwa mstari wa mbele katika ugumu wa eneo lililoko kaskazini kabisa mwa Kamerun, mpakani na Chad, na karibu uliyosahaulika na mamlaka kuu, na kwa umaskini, ambao unaongezewa katika eneo hilo pia  mgawanyiko ya kikabila. Kwa kuhamasisha amani baada ya kuanza kwa mgogoro kaskazini na kusini magharibi mwa Kamerun, na kwa kupambana na ubaguzi dhidi ya watu wachache wa Kiingereza nchini Kamerun (karibu asilimia 20 ya idadi ya watu), Kardinali Christian Tumi alipokea Tuzo ya Nelson Mandela mnamo Julai 2019.

Kardinali Christian Wiyghan Tumi, Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu la Douala (Kamerun) na ambaye ni Kardinali wa kwanza nchini humo mwenye umri wa miaka 90, bado yumo mikononi mwa wateka nyara, baada ya vyombo vya habari mahalia kutangaza kukombolewa kwake. Kanusho hilo limetolewa na Askofu Mkuu wa Douala, Samuel Kleda. Wateka nyara walianza tarehe 5 Novemba mchana katika  mikono ya amri za wenye silaha wakiwa katika barabara katikati ya Bamenda na Kumbo. Mamlaka ya Kaskazini Magharibi ya nchi wamethibitisha.

 

06 November 2020, 11:11