Tafuta

Wakimbizi wa migogoro ya Kaskazini mwa Tigray -Ethiopia Wakimbizi wa migogoro ya Kaskazini mwa Tigray -Ethiopia  

Ethiopia:wito wa Wcc kwa ajili ya suluhisho la mgogoro wa Tigray

Baraza la makanisa Ulimwenguni(Wcc) linaonesha wasiwasi mkubwa kufuatia na ongezeko la mzozo katika Kanda ya Kaskazini mwa Tigray nchini Ethiopia.Hata hivyo Addis Abeba imekanusha uwepo wa upatanisho kutoka kwa rais wa Uganda.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Maombi na mshikamano kwa ajili ya watu na Kanisa la Ethiopia na kushutumu vikali mashambulizi dhidi ya raia na Makanisa, umetoka kwa  Baraza la makanisa Ulimwenguni (Wcc) ambalo linaonesha wasiwasi mkubwa kufuatia na ongezeko la mzozo katika Kanda ya Kaskazini mwa Tigray nchini Ethiopia. Ni katika taarifa yao mara baada   ya ile ya maskofu wa Ethiopia, Shirikisho la Mabaraza ya maaskofu wa  afrika mashariki AMECEA,  hata Papa Francisko kuzindua wito wake akiomba  kusitisha mizozo  ili kutafuta mchakato wa mazungumzo hivi karibuni wakati wa sala ya Malaika wa Bwana.

Wasiwasi juu ya raia wanaokimbia migogoro

Katika taarifa yao mara baada ya Mkutano wa Kamati yake tendaji ya chombo hiki cha kiekumene kinahukumu vikali mashambulizi mabaya sana yaliyofanywa na kundi hili la kisilaha dhidi ya Makanisa na jumuiya na kuwashambuliwa kwa namna ya pekee Makanisa ya kiorthodox ya Tewahedo.  “Tunatoa salam zetu za rambi rambi kwa waathiriwa” wanasema, WCC na kwamba wasiwasi ni kuhusu maelfu ya raia ambao wako katika kikimbia mapigano, ambao kwa sasa ni zaidi ya watu 20,000.   “Tunasali ili waweze kuhakikishiwa usalama wao na uhuru wa dini, na kwa sababu waweze kurudi katika nyumba zao” lakini wakati huo huo wakinyoshea kidole  wale ambao wanajaribu kuchochea mvutano, mafarakano, uhasama na umwagaji damu kwa malengo yao ya kisiasa.

Wcc inatoa wito kwa serikali ili kuondokana na upeo wa janga jipya

Kufuatia na hili, wametoa wito wa nguvu kwa serikali ya Addis Abeba na waasi wa Tigray (Tplf) ili kujiondoa kwenye upeo wa janga jipya na kutafuta mazungumzo badala ya mizozo, ushirikiano badala ya mgawanyiko na wakikumbusha kuwa mateso yamekuwa mengi ya wakati uliopita kwa raia wa Ethiopia. Ethiopia inue sauti zao za kinabii kwa ajili ya mazungumzo , amani na haki, umoja dhidi ya vurugu na chuki na wakati huo wanapongeza juhudi zilizofanywa na vongozi wakristo na waislam wa Ethiopia katika kutafuta amani na maelewano kijamii katika Nchi.

Wcc inaunga wito wa maaskofu Ethiopia, Aacc, Amecea na Papa 

Katika hitimisho la taarifa yao, Baraza la Makanisa Ulimwenguni wanaonesha mshikamano kikristo kwa Makanisa na watu wote wa Ethiopia, pia msaada wao wa kuendeleza  mchakato wa amani ulionzishwa tayari na Baraza la Makanisa barani Afrika (Aacc), pamoja na jumuiya za kikristo mahalia, huku wakihimiza jitihada za kusaidia hata mazungumzo na ushirikiano kati ya makanisa na jumuiya za dini nchini Ethiopia na  Eritrea ili kuweza kuimarisha  uhusiano wa amani katika kanda.

Hatari inayonyemelea vita katika Pembe ya Afrika

Wakati huo huo, hali katika upande wa mapigano bado ni mbaya na hatari ikizidi  kupanuliwa kwa vita katika eneo zima la Pembe ya Afrika. Jumamosi tarehe 14 Novemba baadhi ya maroketi yalioondoka  kutoka Tigray kuelekea Asmara, mji mkuu wa nchi jirani ya Eritrea, iliyoshtakiwa kuunga mkono vikosi vya shirikisho la Ethiopia. Tarehe 16 Novemba serikali ya Addis Ababa imetangaza kushinda mji mwingine na kukana uwepo wa upatanisho na Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

16 November 2020, 18:32