Tafuta

villaggi africani, siccita, poverta, acqua villaggi africani, siccita, poverta, acqua 

Baraza la wanawake katoliki wa Swaziland wazindua kampeni ya kutoa msaada wa wakimbizi!

Hivi karibuni nchini Swaziland,baraza la wanawake katoliki walizindua kampeni kwa ajili ya kusaidia wakimbizi walioko katika kambi ya mapokezi ya Malindza,wanapokea wakimbizi kutoka Burundi,Angola,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Rwanda na Somalia.

Na Sr. Angel Rwezaula- Vatican.

Baraza la wanawake katoliki nchini Swaziland wamezindua kampeni ya kuwasadia wakimbizi. “Kufikiria matumaini” ndiyo mada iliyochaguliwa kuongoza kampeni hiyo ya kuwasaidia wakimbizi katika kambi ya mapokezi ya Malindza. Wakifafanua juu ya mada hiyo kwamba kwa kufikiria hasa  kwa sababu mambo yanaponekana kuwa na vizingiti, magumu, wakati mitindo ya kizamani haifanyi kazi tena inavyotakiwa, hapo ndiyo kuna  ulazima wa kutafuta namna nyingine ya kufikiria na kuwa na tumaini, wanasema wanawake katoliki katika kubainisha mpango wao wa upendo kwa ajili ya wenye kuhitaji zaidi katika kesi hiyo, wakimbizi.

Hatua hii ya furaha ni matokeo ya Baraza la wanawake wa eSwatini (Eccw),ambao walivuna matunda ya mpango huo ambao ulipelekea kupelekwa kwa vifaa vya safi na mambo mengine kwa wakimbizi kutoka Burundi, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rwanda na Somalia hivyo miezi ya  karibuni iliyopita. Mpango pia uliungwa mkono na askofu José Luis Gerardo Ponce de León wa Manzini, Caritas ya eneo hilo na Tume ya kiserikali ya wakimbizi, na ambapo wakati wa kukabidhi walikuwapo hata wawakilishi wa serikali. Kwa maana hiyo Bi Doris Makhubu rais wa wanawake katoliki nchini humo (ECW),  alisema “asante kwa kuturuhusu kutoa msaada kwa ajili ya mahitaji msingi ya usafi wa mazingira na ndugu, kaka na dada zetu”

Hata hivyo Rais wa wanawake Katoliki amewaalika  waamini wote na wenye mapenzi mema kusali kwa Bwana ili aweze kufungua akili na mioyo yao kwa namna pekee ya kwenda kukutana na mahitaji ya kila mtu kwa kuweza kubadilisha hali yao ya woga, wasiwasi na hisia za upweke ili wapate kuwa na matumaini, kwa namna ya kwamba wote wanaweza kushuhudia uzoefu wa kweli wa uongofu wa mioyo.

04 November 2020, 18:06