Tafuta

Vatican News
Ni mwezi wa Bikira Maria  na wa kusali  Rosari Takatifu kila siku. Ni mwezi wa Bikira Maria na wa kusali Rosari Takatifu kila siku. 

Vietnam:Fuateni Mfano wa Maria na kusali Rosari Takatifu

Askofu wa Long Xuyen nchini Vietnam amewaalika waamini kufuata mfano wa Maria huku wakisali Rosari Takatifu na kufanya jitihada za kazi ya Uinjilishaji katika fursa ya Mwezi wa Kimisionari Oktoba 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Askofu Joseph Tran Van Toan, wa Jimbo katoliki la Long Xuyen, katika barua yake ya kichungaji kwa mwezi wa Oktoba, 2020, Mwezi wa Rosari Takatifu na katika Siku ya Kimisionari Ulimwenguni inayotarajiwa kufanyika  tarehe 18 Oktoba, amewaalika wakatoliki wa Vietnam kufuata mfano wa Mama Maria kwa kusali Rosari Takatifu kila siku, hasa wakiombea kazi ya uinjilishaji na kufanya matendo ya upendo kwa ajili ya wale ambao bado hawajajua Habari Njema. Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la habari katoliki UCA, Askofu Toan amewashauri waamini wote kuishi  zile “HERI”, kwa mfano wa Bikira Maria, ili waweze kuwa mbegu ya Ufalme wa Mungu. Amewatia moyo ili waishi roho ya umaskini, huku wakikubali maisha rahisi na kushirikishana kile walicho nacho kwa  watu wahitaji.

Askofu Toan katika ujumbe wake amesisitiza kwamba Wakatoliki wanapaswa kukubali mapungufu yao na kusasahisina kwa uaminifu makosa ya wengine pia kumtendea adui kwa uvumilivu. Kubali, hayo kwa  kufuata na kushiriki maadili ya Kikristo, kwenye utume na matakwa ya ulimwengu, ili kuweza kuwa chumvi na nuru ya ulimwengu. Katika barua ya kichungaji Askofu wa Long Xuyen kadhalika amependekeza kwa maparokia kufanya uzinduzi mpya wa uinjilishaji na kwa vyama vya kitume ili kuimarisha mahusiano, kutembea kutoka nje  na kutoa msaada wa kifedha iwe binafsi au kiumuiya kwa ajili ya vituo vya kimisionari. Hatimaye, Askofu ameomba Tume ya shughuli za kijimbo kufanya kazi na Tume ya Uijilishaji ili kuweza kuunda chama cha kimisionari cha Utoto Mtakatifu.

Jimbo katoliki la Long Xuyen, lilipoundwa mwaka 1960 lilikuwa na parokia 68, vigango 86 na vituo vya kimisonari  18. Tangu wakati huo hadi sasa zipo parokia 151, vigango 59 na vituo vya kimisionari23 na pongezi kwa shughuli za kimisionari za Jumuiya katoliki mahalia ambao wameonesha nguvu ya uwepo wa wilaya mbili ya  An Giang na  Kien Giang  na sehemu nyingine ya mji wa Can Tho katika Delta ya Mekong. Idadi hiyo kwa mujibu wa Askofu Toan anasema imejionesha kama wakatoliki mahalia wanakirimiwa vizuri kati ya tamaduni za wakulima na watu wengine wa imani  tofauti na kwa kushirikishana pamoja matatizo na huku wakifanya kazi wote pamoja  ili kujenga ustaarabu wa upendo na maisha. Jimbo la Long Xuyen, ambalo linaleta pamoja wakatoliki 230.000 kati ya jumla ya wakazi Milioni 4,3 wanahudumiwa na mapadre 315, watawa 515, waseminari 150 na makatekista  1.700.

01 October 2020, 14:46