Tafuta

Maandalizi ya Siku ya Vijana nchini Ureno 2023 yanaanza Maandalizi ya Siku ya Vijana nchini Ureno 2023 yanaanza  

Ureno-Siku ya vijana Lisbon 2023:uwasilishaji wa nembo ya siku hiyo kukaribia!

Nchini Ureno inajiandaa na maandalizi ya siku ya vijana 2023 ambapo tarehe 16 Oktoba 2020 inawasilishwa nembo itakayoongoza siku hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Tarehe 16 Oktoba itawakilishwa rasmi nembo ya Siku ya Vijana dunia inayotarajiwa kufanyika jijini Lisbon nchi Ureno kunako mwaka 2023. Ni taarifa kutoka kwa waandaaji wa tukio hilo kupitia ukurasa wa Facebook. Andikeni tarehe katika ajenda! Wameandika kwenye ukurasa wao katika  taarifa na kuonesha hatua muhimu sana ya njia inayaoelekeza kufikia siku ya vijana ulimwenguni. Waandaaji wa tukio hilo  wanasisitiza kuwa tarehe iliyo chaguliwa ya tarehe 16 Oktoba siyo kwa bahati mbaya kwa sababu ilikuwa tarehe na mwezi huo mwaka 1978 ambapo Mtakatifu Yohane Paulo II alichaguliwa  na Siku ya vijana ulimwenguni ikawa inawazwa na kuhamasishwa.

Nembo ya toleo la mwaka 2023 imechaguliwa kwa misingi ya shindano lililotolewa kunako Oktoba 2019 na tume ya maandalizi mahalia. Hii inawahusu wataalam wa ufundi wa kuchora  na wanafunzi wanaojifunza katika shule za umma na binafsi ulimwenguni kote na ambapo shindano hilo limehitimishwa hivi karibu hivyo muda si mrefu watatangaza mshindi.

Ikumbukwe kwamba Siku ya vijana (WYD) mjini Lisbon ilipaswa ifanyike mnamo mwaka  2022, kama kawaida ya kila baada ya miaka mitatu baada ya ile ya awali, iliyofanyika huko Panama mnamo Januari 2019. Walakini, janga la Covid-19 limelazimisha tukio hilo kuahirishwa kwa mwaka mmoja tena. Kauli mbiu ya Siku hiyo, sasa ambayo inafikia toleo la 38, ni “Maria aliinuka akaenda haraka”, iliyochukuliwa kutoka Injili ya Mtakatifu Luka (1,39).

Kuahirishwa kwa siku hiyo  pia iliahirishwa hata uwasilishaji wa alama za  Siku ya vijana ulimwenguni (WYD)  ambazo ni Msalaba na picha ya Bikira Maria kwa vijana wa Ureno. Kwa kawaida, ni tukio lifanyika siku ya Jumapili ya Matawi ambayo inajulikana pia ni Siku ya Vijana kijimbo kwa uwaakilishaji wa  vijana walitangulia kuwa na  tukio hilo  ( WYD) kwa kuwakabidhi  alama hizo  mbili katika Uwanja wa Mtakatifu Petro  kwa wenzao kutoka  taifa ambalo watakaribisha siku inayofuata. Kwa sasa, sherehe ya makabidhiano imepangwa kufanyika tarehe 22 Novemba 2020, kwenye sikukuu ya Kristo Mfalme, lakini kila kitu kitategemea na badiliko ya hali ya kiafya.

13 October 2020, 15:00