Tafuta

Vatican News
Ni umuhimu kuwa na mazungumzo kati ya Kanisa na familia ambayo ni Kanisa dogo  la nyumbani  na  kutiwa moyo wahudumu wote wa kichungaji katika sekta ya kupeleka mbele utume wa elimu katoliki Ni umuhimu kuwa na mazungumzo kati ya Kanisa na familia ambayo ni Kanisa dogo la nyumbani na kutiwa moyo wahudumu wote wa kichungaji katika sekta ya kupeleka mbele utume wa elimu katoliki 

Ureno:18/26 Oktoba ni Wiki ya Kitaifa ya elimu ya kikristo!

Kanisa nchini Ureno itafanya Wiki ya Kitaifa nchini kwa ajili ya Elimu ya Kikristo ili kusaidia familia ambayo ni Kanisa dogo la nyumbani.Wiki hiyo inaongozwa na kauli mbiu isemayo"kuongeza nguvu na kusaidia familia,Kanisa la nyumbani”.Ni umuhimu kuwa na mazungumzo kati ya Kanisa na familia na kuwatia moyo katika utume wake.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Kutegemea familia na kuhusu uwezo wake wa kuwa Kanisa dogo la nyumbani ndiyo msisitizo wa Wiki ya Kitaifa ye Elimu ya Kikristo iliyotangazwa na Maaskofu w Ureno itakayoanza tarehe 18 -25 Oktoba. Tukio hili limeandaliwa na Tume ya Maaskofu kwa ajili ya elimu na Mafundisho ya imani ambapo katika tukio hili linajikita moja kwa moja katika teknolojoa na mafundisho ya kidigitali, kwa maana hata janga la virusi vya corona haliwezeshi fursa ya kufanya mikutano mikubwa ya moja kwa moja. Katika fursa hiyo hata hivyo wametoa hati moja waliyoipa jina “kuongeza nguvu na kusaidia familia, Kanisa la nyumbani” ambapo wanabainisha kuwa ni umuhimu kuwa na mazungumzo kati ya Kanisa na familia kwa kuwapongeza huku kuwatia moyo wahudumu wote wa kichungaji katika sekta ambayo imepeleka mbele kazi kwa kujitoa na ujasiri, katika kipindi kigumu kisicho na uhakika na matatizo mbali mbali.

Katika hati hiyo inasisitza kwamba dharura ya kiafya kwa hakika imesababisha kufanya uzoefu wa umbali na kusimamisha kwa kiasi fulani tabia za mahangaiko ya hapa na pale ya kila siku, lakini wakati huo huo kwa  kusindikizwa na wasiwasi mkubwa. Hali hizo kwa mujibu wa hati hiyo umepunguza au kudhoofisha ukuu fulani wa maisha ya mwanadamu kwa kiasi kikubwa na utajiri kama ule wa kuishi kwa pamoja kijumiya au mikutano ya kidini. Pamoja na hayo yote , hata hivyo kipindi hiki kimeonesha hata umuhimu msingi wa familia katika kuonesha maisha na thamani za kibinadamu na kikristo ikiwa ni pamoja na nafasi yake msingi ambayo haiwezi kubadilishwa katu  na uhusiano wake, katika elimu ya mapendo na kukubaliana kwa pamoja.

Hali halisi uliyoundwa na dharuru ya kiafya kwa maana nyingine imeleta hata aina mpya za kiutendaji ili kwamba kuandaa wakati ujao ulio tofauti na kwa maoni ambayo yanagundua nafasi msingi ya familia. Na zaidi ni dharura kwa mujibu wa Tume ya Maaskofu nchini Ureno kwamba lazima kuwa makini na kutunza kiungo cha kifamilia katika utume wa uinjilishaji kwa mapendekezo muhimu ya kusaidia kazi yake ya kuelimisha. Kwa hakika  ni kwa njia hiyo ya kufanya mang’amuzi muhimu ya ishara za kipindi  na kwa njia ya ushirikishano inaweza kweli  kuangazia yote ambayo yanaweza kufanyika na kuhamasisha mafunzo ya kibinadamu na kikristo katika hali halisi tofauti za wakati huu.

03 October 2020, 16:37