Tafuta

2020.10.10 kutangazwa mwenyeheri Carlo Acutis 2020.10.10 kutangazwa mwenyeheri Carlo Acutis  

Mwenyeheri Carlo Acutis:Upendo kwa Ekaristi na Mama Maria!

Kuhudhuria misa kila siku,kuabudu ekaristi na kusali rosari kwa Mama Maria ndiyo ilikuwa roho iliyomwezesha kuishi ugonjwa wake na kukabiliana kwa utulivu hadi mauti.Upendo wa maskini na waliobaguliwa pia ilikuwa roho ya utume wake.Ni maneno ya Kardinali Vallini wakati wa mahubiri kwenye misa ya kumtangaza Mwenyeheri katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Francis wa Assisi,Jumamosi,tarehe 10 Oktoba 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

“Akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote. (Yh. 15,5), kwa maneno hayo tumesikia katika Injili ya Yohane, Yesu katika karamu yake ya mwisho anawambia mitume wake na kuwashauri wabaki wameungana na Yeye kama mti wa mzabibu na matawi yake. Picha ya mti wa mzabibu na matawi yake ni mambo muhimu yanayaelezea ulazima wa maisha ya kikristo kuishi katika muungano na Mungu. Ndivyo alivyoanza mahubiri Kardinali Agostino Vallini kwa niaba ya Papa Francisko, kumtangaza Mwenyeheri Carlo Acutis, Jumamosi tarehe 10 Oktoba 2020 huko Assisi nchini Italia. Kardinali Vallini amesema sisi sote kwa namna ya pekee tunashangaa na kuvutiwa na maisha na ushuhuda wa Carlo Acutis, ambaye Kanisa linatambua kuwa  mfano wa maisha ya kikristo na kupendekeza hasa kwa ajili ya vijana. Hii inajitokeza swali la ghafla kujiuliza, je alikuwa na jambo gani muhimu, kijana mdogo mwenye umri wa miaka 15 tu? Kwa kupitia kutazama katika maisha yake tunapata baadhi ya mambo muhimu yenye tabia tabia ya ubinadamu.

Yeye alikuwa kijana wa kawaida, rahisi, mkarimu, (inatosha kuangalia picha zake) alikuwa anapenda uoto wa asili na wanyama, alikuwa anacheza mpira, alikuwa na marafiki wengi wa rika lake na alikuwa anavutiwa na vyombo vya kisasa vya mawasiliano ya kijamii, mwenye hamu kubwa ya inteneti na kwa kujifunza peke yake ambapo alitengeneza program za kuweza kueneza Injili ili kuwasilisha thamani na uzuri wake (Papa Francisko). Alikuwa na zawadi ya kuvutia na alikuwa anatambuliwa kama mfano.  Akiwa mtoto kwa mujibu wa ushuhuda wa familia yake alikuwa akihisi mahitaji ya imani na alikuwa na mtazamo wake akiuelekeza kwa Yesu. Upendo kwa ajili ya Ekaristi aliyokuwa nayo   kwa undani na kuhifadhi  uhai wote ule uhusiano wake na Mungu. Alikuwa mara nyingi anasema “Ekaristi ni njia yangu ya haraka ya kwenda mbinguni”. Kila siku alikuwa anashiriki Misa takatifu na alikuwa anabaki kwa muda mrefu akiabudu mbele ya Ekaristi Takatifu. Carlo alikuwa anasema “Unakwenda Mbinguni ikiwa unakaribia Ekaristi kila siku!”

Kwake Yesu alikuwa ni rafiki, Mwalimu na Mwokozi, alikuwa ni nguvu ya maisha yake na lengo kuu la kila kitu afanyacho. Alikuwa anaamini kwamba kwa kupenda watu na kuwafanyia mema ni lazima kuchota nguvu kutoka kwa Bwana. Kwa roho hiyo alikuwa kweli mwenye ibada kubwa ya Mama Maria. Shauku yake kubwa ilikuwa ile ya kuvutia watu wengi kwa Yesu kwa  kuwatangazia Injili hasa kwa njia ya mfano wa maisha. Ilikuwa ni ushuhuda wake wa imani ambao ulimsukuma kufaulu kuendeleza shughuli ya uinjilishaji katika mazingira ambayo alikuwa anakwenda na kubadilishana maisha na kukaribia Mungu. Kardinali Vallini aidha amesema na alifanya hivyo kwa hiari, na tabia yake ya upendo kwa hakika, kuwa na uwezo wa kushuhudia maadili aliyoamini  na ambayo yalikuwa ni ya kushangaza, licha ya  vizingiti vya  kukabiliwa navyo  hata kutokueleweka na  wakati mwingine hata kuchekwa. Carlo alikuwa anahisi kwa nguvu haja ya kusaidia watu wagundue kuwa Mungu yuko karibu,  na ni vizuri kubaki na Yeye ili kufurahia urafiki wake na neema yake. Ili kuweza kuwasilisha hili kiroho alikuwa anahitaji nyenzo, hata kwa njia za kisasa za mawasiliano ya kijamii, ambazo alikuwa anajua kuzitumia vizuri sana kwa namna ya pekee Intaneti ambayo alikuwa akifikiria kama zawadi ya Mungu na zana muhimu ili kukutana na watu na kuendeleza  urafiki na maadili ya Kikristo.

Njia hii ya kufikiri ilimfanya aseme,  njia za mitandao  siyo njia za kukwepa tu, lakini ni nafasi ya kufanya mazungumzo, maarifa, kushirikisha, kuheshimiana, kutumiwa kwa uwajibikaji, bila kuwa watumwa na kukataa uonevu wa kidigitali. Katika ulimwengu mpana  kabisa lazima mtu ajue kutofautisha mema na mabaya.  Kwa mtazamo huu mzuri, alihimiza utumiaji wa mitandao kama njia ya huduma ya Injili, ili kufikia watu wengi iwezekanavyo na kuwajulisha uzuri wa urafiki na Bwana. Kwa lengo hilo alijitahidi kuandaa maonesho msingi ya miujiza ya Ekaristi iliyotokea ulimwenguni na ambayo ilikua ikimsaidia kufanya katekisimu kwa watoto. Alikuwa ni mwenye ibada kuu ya Mama Mari na alikuwa anasali Rosari kila siku na kujiweka wakfu mara nyingi kwa ajili ya kupyaisha upendo wake na kuomba ulinzi wake. Kutokana na hatua hii tunaweza kusema  sala na utume ndiyo mambo mawili yanayojikitka katika imani ya shujaa wa huyu Mwenyeheri Carlo Acutis, ambaye katika maisha yake mafupi amejua kujikabidhi kwa Bwana kila wakati wa maisha yake hasa katika wakati mgumu sana, ameisitiza Kardinali Vallini.

Katika roho hiyo aliweza kuishi ugonjwa wake kwa kuukabili kwa utulivu na kumfikisha katika kifo. Carlo alijiachia katika mikono ya Mpaji na chini ya mtazamo wa Mama Maria alikuwa akirudia “Ninataka kutoa mateso yangu yote kwa Bwana kwa ajili ya Papa na kwa Kanisa. Sitaki kwenda kwenye Moto (Purugatorio); Ninataka kwenda moja kwa moja Mbinguni (Positio, Wasifu wake, hati, 549).  Tuumbuke lakini aliyekuwa anazungumza hivyo ni kijana mdogo wa miaka 15 huku tayari  akionesha ukomavu wa kikristo wa kushangaza, ambao unatuchochea na kututia moyo ili kuchukua hata ya maisha ya imani kwa uzito zaidi. Carlo alikuwa wa kushangaza hasa kwa bidii ambayo katika mazungumzo alikuwa akitetea utakatifu wa familia na utakatifu wa maisha dhidi ya utoaji mimba na euthanasia.

Mwenyeheri mpya bado anawakilisha mfano wa nguvu, kwa aina yoyote ya maelewano, tukijua kuwa ili kubaki katika upendo wa Yesu, ni muhimu kuishi Injili kwa dhati (Yh 15,10), hata kwa gharama ya kwenda kinyume na ulimwengu. Yeye aliishi kweli maneno yake Yesu asemaye “ Hii ndiyo amri yangu, pendaneni kama nilivyowapenda ninyi (Yh 15,12). Uhakika wake huu wa Maisha ulikuwa unamepelekea kuwa na upendo mkuu kwa ajili ya jirani, hasa kwa maskini, wazee na walioachwa peke, bila kuwa na makazi, walemavu na watu ambao jamii inawabagua na kuwaficha. Carlo daima alikuwa anapokea wale waliokuwa wanahitaji na wakati akienda shule, akikutana nao barabarani alisimama na kuzungumza nao. Alikuwa anasikiliza matatizo yao na kwa mipaka ya uwezekano wake, aliwasaidia. Carlo hakujikunja yeye binafsi bali alikuwa na uwezo wa kueleza mahitaji na dharura za watu, ambamo aliona uso wa Kristo. Kwa maana hiyo kwa mfano hakukosa kamwe kuwasaidia wenzake darasani kwa namna ya pekee wale waliokuwa na matatizo zaidi. Maisha yake angavu kwa hakika aliyatoa kwa wengine kama Mkate wa Ekaristi.

Kardinali Vallini aidha amesema Kanisa lina furaha kubwa kwa sababu kijana huyo Mwenyeheri anatimiza maneno ya Bwana. “ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kudumu; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.” (Yh 15,16).  Ni Carlo aliyekwenda na akapelekea matunda ya utakatifu, kwa kuonesha jinsi ambavyo wote tunaweza na siyo kitu ambacho kimewekwa kwa walio wachache tu. Maisha yake ni kielelezo hasa kwa vijana, ambao hupata kuridhika katika mafanikio ya muda mfupi, badala ya yae  maadili ya kudumu ambayo Yesu anapendekeza katika Injili, ana mbayo ni kumtanguliza Mungu, katika hali kubwa na ndogo ya maisha, na kumtumikia ndugu, hasa walio wa mwisho. Kutangazwa kwa Carlo Acutis, mtoto wa ardhi ya Lombaridia na mpenda ardhi ya Francis wa Assisi ni habari njema na tangazo la nguvu ambalo kijana wa enzi zetu kama wengi amependezwa na Kristo na kuwa kama taa ya mwanga kwa wale ambao watataka kumjua na kumfuata kama mfano. Yeye alishuhudia kwamba imani haitutengi na maisha, lakini hutuzamisha kwa ndani zaidi, ikituonyesha njia thabiti ya kuishi furaha ya Injili. Ni juu yetu kuifuata, tukivutiwa na uzoefu wa kupendeza wa Mwenyeheri Carlo ili hata maisha yetu yaweze kuangaza mwanga na tumaini. Mwenye heri Carlo Acutis, utuombee.

CARLO ACUTIS

 

10 October 2020, 18:00