Tafuta

Askofu  Luiz Fernando Lisboa, wa Pemba, Msumbiji Askofu Luiz Fernando Lisboa, wa Pemba, Msumbiji 

Msumbiji-uhamisho wa ndani unazidi kuongezeka huko Capo Delgado

Askofu wa Pemba huko Cabo Delgado nchini Msumbiji ametoa taarifa juu ya kuongezeka uhamisho wa ndani na kwamba watu wanahitaji msaada.Watu wengine wanatumia muda wa siku tatu au nne katika bahari na kufika wakiwa na kiu na njaa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ombi la msaada limetolewa ili kuwa na mshikamano kutoka kimataifa kwa ajili ya jamuiya ya Msumbiji kutokana na vurugu na mzozo mkubwa wa kibinadamu unaoendelea katika mkoa wa Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji. Ni wito uliozinduliwa hivi karibuni Askofu  Luiz Fernando Lisboa, wa jimbo katoliki la wa Pemba, akizungumza kwenye video iliyotumwa  kwenye shirika la habari za Baraza la Maaskofu Italia (SIR) na vyanzo vingine vya kimisionari.

Katika maelezo yake Askofu wa Pemba kutoka Brazil anaonekana kuwa katika fukwe huku akizungukwa na mitumbwi karibu 170 zilizojaa watu wanaokimbia mashambulizi ya makundi ya kijihad na ambayo yanazidi kufika bila kukoma katika maeneo yao. Ni karibu watu 300,000 waliohamishwa ndani tangu mwanzo wa migororo ya ndani katika kanda kunako 2017.

Hali halisi ni ngumu anasimulia Askofu Lisboa na kwani mamia ya watu wanalala fukweni na wengi wao pia wanafariki wakiwa njiani amesema. Na wengine wanatumia muda wa siku tatu au nne katika bahari na kufika wakiwa na kiu na njaa. “Ni mgogoro mbaya sana wa kibinadamu. Tunahitaji msaada  kimataifa kwa ajili ya mshikamanowa jamii ya Msumbiji” amesisitiza. Hata hivyo ikumbukwe kwamba Papa Francisko alikuwa amempigia simu Askofu Lisboa mnamo tarehe 21Agosti iliyopita akionesha ukaribu wake na mshikamano.

30 October 2020, 12:19