Tafuta

2019.08.09 Kambi ya wakimbizi nchini Venezuela 2019.08.09 Kambi ya wakimbizi nchini Venezuela 

Marekani:Kanisa laadhimsha miaka 15 ya kampeni ya Haki

Imepita miaka 15 tangu Baraza la Maaskofu nchini Marekani walipoanzisha kampeni ya haki kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Katika waraka wa Baraza la Maaskofu kupitia kwa Rais na Makamu rais wa Kamati ya Baraza la kitaifa la Maaskofu kwa ajili ya wakimbizi wametoa tamko linalowataka waamini katika Mwezi wa kimisionari kuwaokoa, kuwalinda, kuhamasisha, na kufungamanisha shughuli za wakimbizi.  Tangu mwaka 2005 ilianzisha harakati hizi ambapo Kanisa Katoliki nchini Marekani (Usccb) wameziendeleza ili kuweza kuwatendea haki wakimbizi na kuwa na umoja utakao zisaidia taasisi za kikatoliki kuwategemeza wakimbizi walio katika kambi za uhamiaji. Kwa muda wa miaka 15 jitihada hizi zimeongezeka na   kusukuma mbele harakati za upatikana wa haki za wakimbizi na utungaji wa sheria zitakazowalinda wakimbizi.

Katika waraka uliotiwa sahini na Askofu Mkuu José H. Gomez na Askofu Mario E. Dorsonville, Rais na makamu wake unasema “Nguvu zetu zimeelekzwa  kwenye Injili na katika ulazima wa kuutambua uso wa Yesu kwa kila mtu”. Katika mstakabali huo, Baraza la Maaskofu Marekani wanajikita kuelimisha wakatoliki katika mafundisho ya Kanisa ya kuhamasishaji utu wa kila mmoja wakiwemo wahamiaji na wakimbizi. Kwa kusisitiza wanasema “Tuzidi kuwapa moyo watunzi wa sheria na viongozi wa jumuiya huku tukijihadhari na kuweka siasa katika utoaji wa huduma kwa ndugu zetu wakimbizi”.

Maaskofu katika kutimiza miaka 15 ya siku ya haki na wakimbizi wameweka hati katika mitandao wa Barara kuhusu kipaumbele cha kisiasa juu ya uhamiaji. Hati hiyo imeundwa karibu na vitenzi vinne vilivyoonyeshwa na Baba Mtakatifu Francisko, kuhusu kukaribisha, ambapo wanasema watunga sheria wanaalikwa kuzingatia sababu kuu za uhamiaji hasa kwa ombi la hifadhi au hadhi ya wakimbizi.  ‘Kuhamasisha uelewa mzuri’ wa suala la uhamiaji, ni katika kuanzisha mipango ambayo husaidia kukabiliana na mwelekeo wa uhalifu, kutengwa na kubaguliwa; na kuendeleza mipango ya kujitoa kuchunguza kesi za uhamisho.

Kuhusu kitenzi ‘kulinda’, hati hiyo inasisitiza umuhimu wa kuwapa wahamiaji ufikiaji wa huduma za afya, chakula, makao, huduma za kidini na kisheria katika vituo vyote vya kizuizini vya serikali, pamoja na huduma za utafsiri na utetezi. ya Mahakama; Hakikisha uwezekano wa muda mrefu na upatikanaji wa hifadhi kwa wakazi wanaohitaji ulinzi; kutumia mitindo ya binadamu na ya usawa  katika ufuatiliaji wa wahamiaji kama njia mbadala ya kuwekwa kizuizini, Kufuta marufuku ambayo yanahusu wahamiaji kwa misingi ya rangi, dini au sifa za kibinafsi.

02 October 2020, 15:37