Tafuta

Vatican News
2020.08.01 Biblia ni maandiko matakatifu ya Mungu. 2020.08.01 Biblia ni maandiko matakatifu ya Mungu. 

Malawi:Wakatoliki waalikwa kugundua kwa upya Neno la Mungu!

Kwa mujibu wa kile kilichoandikwa kwenye ukurasa wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika Mashariki(AMECEAPadre Henry Chinkanda mratibu wa kichungaji kitaifa wa Baraza la Maaskofu nchini Malawi(Ecm),amehimiza wakatoliki kugundua kwa upya Neno la Mungu na kulisoma kila siku.Ni katika kuhitimisha Mwezi wa Bibblia uliowekwa Septemba na Baraza la Maaskofu nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Umehimitimishwa mwezi wa Biblia nchini Malawi  kwa kutoa mwaliko kwa waamaini kugundua kwa upya Nen0 la Mungu na mafundisho ya mavuno ya Biblia. Mwezi Septemba kwa hakika ulikuwa umewewkwa kwa ajili ya Neno la Mungu na zaidi katika kuenzi  kumbu kumbu ya Mtakatifu Yeronimo mtafsiri wa wa  Maandiko matakatifu katika lugha ya kilatino.

Kwa mujibu wa kile kilichoandikwa kwenye ukurasa wa Shirikisho la Mabaraza ya Maasfofu Afrika Mashariki(AMECEA) Padre Henry Chinkanda, mratibu wa kichungaji kitaifa wa Baraza la Maaskofu nchini Malawi (Ecm), amehimiza wakatoliki kugundua kwa upya Neno la Mungu. Amesema hayo wakati wa Misa iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Pietro huko Mzuzu, tarehe 30 Septemba 2020 ambapo kiliturujia ilikuwa ni sikukuu ya Mtakatifu na Yeronimo mwalimu wa Kanisa. Padre Chinkanda katika mahubiri yake, kwa kuona ongezeko la wakristo wengi nchini Malawi amesema kusoma Biblia ni sababu ya kushughulika jambo hili kwa dhati, na kusisitiza umuhimu wa kuwa na tabia ya kusoma Neno la Mungu kila siku ili kujimwilisha kwao katika maisha ya kiroho.

Neno la Mungu linaweza kuwazadia  na kuwaongoza katika matendo, lakini pia ni kisima cha kuchota nguvu  na kitulizo, kichocheo cha kutokata tamaa wakati wa shida za maisha, amesisitiza hilo Padre Chinkanda huku akikumbuka tafsiri ya Kilatino ya Mtakatifu Yeronimo ambaye iliwezesha uelewa kwa wote wa Maandiko matakatifu kupitia kilatino. Maadhimisho ya Kibiblia kwa kawaida uadhimishwa na wakatolika katika  mzima na zaidi katika Bara la Amerika ya Kusini. Ikumbukwe, kauli mbiu iliyoongoza mwezi wa Kibiblia mwaka huu nchini Malawi ilikuwa ni “ Neno la Mungu ni wanaga na taa ya miguu yangu”.

12 October 2020, 15:26