Tafuta

Viongozi wa kidini nchini Kenya wana wasiwasi wa manai k kufuata na  maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2022 Viongozi wa kidini nchini Kenya wana wasiwasi wa manai k kufuata na maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2022 

Kenya:Viongozi wa kidini nchini kenya watoa wito wa kusitisha mizozo na kukuza amani!

Viongozi wa kidini nchini Kenya katika utibitisho wa waraka wao wa pamoja wa kikundi cha mazungumzo(Drg)wanaomba kukomesha kwa mvutano na kukuza amani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyikatarehe 16 Otoba 2020 jijini Nairobi, wahusika wa kidini wamebainisha umuhimu wa kufanya mazungumzo ya kitaifa ambayo yanajumuisha wakenya wote ili kuweza kufikia upatanisho wa kweli wa nchi. Wasiwasi wa kikundi hiki hasa ni kwamba katika matazamio ya uchaguzi mkuu wa 2022 unaweza kuongeza hali ngumu ya migogoro na vurugu kama ilivyojionesha mwaka 2018. Wito huo unaoelekezwa kwa wanasiasa, watu wa dini na raia wote  unaangazia hali mbaya zinazowezekana iwapo kutakosekana amani. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kwanza inasomeka ile ya mgogoro sugu, ambao mizozo msingi hadi sasa haijasuluhishwa, na inabaki palepale katika eneo lote, na kusababisha ukiukwaji endelevu wa haki za binadamu, kutokujali,  dharura , utawala wa sheria, na vile vile kuenea kwa rushwa, bila mageuzi yoyote. Kwa maana hiyo hivi  sasa, kwa mujibu wa viongozi wa kidini wanaelezea, kuwa Kenya inakabiliwa na hali hii, lakini hali ya pili inazidi kuwa karibu nayo, ambayo ni kurudi tena kwenye mzozo. Hii kiukweli ikiwa makubaliano yaliyoanzishwa kati ya rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, inawezekana kuibuka wanamgambo wa siri, ili kudhoofisha taasisi za kijamii na kuhatarisha machafuko kwa mujibu wa maelezo yao viongozi wa dini.

Hali ya tatu, kwa upande mwingine, ni ile ambayo  Kikundi hiki cha kidini (Drg) kinaonesha kama hali nzuri, kwa sababu wanasema  itaruhusu mazungumzo ya umoja, utatuzi wa mizozo ya mara kwa mara kati ya jamii na mageuzi ya uchaguzi muhimu ili kufikia kuaminika, huru, haki na uwazi. Katika suala hili, viongozi wa kidini wanakumbusha Mpango wa “kujenga madaraja” (BBI), iliyozinduliwa baada ya makubaliano kati ya Rais Kenyatta na Odinga. Mpango huo umekusudiwa kuleta mgawanyiko zaidi kuliko umoja kwa mujibu wa hati ya pamoja  na kwamba “ikiwa itaendelea kuijadili kutoka katika maoni ya kisiasa, badala yale  yaliyomo”. Jambo jingine la kudumu lililokumbukwa na Kikundi hiki cha kidini nchini Kenya (DRG) ni mapambano dhidi ya adhabu ya wazi ambayo ni msingi wa rushwa nchini humo. Hakuna haki katika ufisadi, chombo hiki kinasisitiza na kinamtaka raisi Kenyatta kuanzisha mchakato mpana wa ushauri  ili kuandaa mkakati wa kutokomeza janga hilo la ufisadi katika kiwango cha kitaifa.

Kwa kuzingatia mazingira magumu ya janga la Covid-19, viongozi wa kidini wanakumbuka kwamba imesababisha umaskini zaidi ya asilimia 45 ya idadi ya watu na hii inamaanisha kwamba kuna raia maskini zaidi, waliokata tamaa, wenye njaa na wenye hasira, au viungo ambavyo ni nguvu kwa mzozo wa kulipuka . Kwa kuongezea, chombo hiki cha kidini Drg kinasema wana wasiwasi juu ya vipindi vya hivi karibuni ambavyo , kwa vikosi vya usalama vimezuia shughuli katika sehemu za ibada. “ Hizi ni hatua zisizofaa ambazo tunaomba kukomeshwa mara moja, wanasema viongozi wa dini, wakisisitiza kwamba sheria na utaratibu wa umma lazima utumiwe kwa njia ile ile kwa kila mtu”. Vivyo hivyo, Kikundi hiki kinawakumbusha hata viongozi wote  wa kidini kudumisha utakatifu wa maeneo ya ibada, bila kuzitumia kwa malengo mengine kama propaganda za kisiasa.

Viongozi wa kidini pia wanadai kwamba nafasi nne zilizobaki wazi katika Tume ya Uchaguzi zijazwe na kupendekeza kwamba maafisa wa chombo hicho kila wakati wasasishe raia juu ya maandalizi ya uchaguzi. “Tunachopaswa kuepuka, kiukweli, ni kusimamia uchaguzi kana kwamba ni dharura”. Haki ni ujazo wa ubinadamu na wa taifa thabiti lakini haki inategemea ukweli. Kwa maana hiyo sote tukubali ukweli na tuwapinge wale wanaozua uwongo”. Tamko la pamoja Kikundi hiki kilichoundwa kunako 2016 ili kuhakikisha uchaguzi huru, wa amani na wa kuaminika na mnamo 2017, DRG kilifanya kazi ili kuendeleza utawala bora wa Kenya, amani, mshikamano na utulivu. Kiongozi wake mkuu ni Askofu Mkuu katoliki Martin Kivuva, wa Mombasa. Kikundi hiki kinaundwa na wawakilishi wa mashirika  ya kidini nchini Kenya, ambao ni shirikisho la Kiinjili, Baraza la Wahindu, Baraza la Kitaifa la Makanisa, Waadventisti, Wasabato na Baraza Kuu Waislamu.

19 October 2020, 16:20