Tafuta

Vatican News
Balozi wa kitume nchini Kenya,Sudan na Eritrea Askofu Mkuu  Hubertus Matheus Maria van MEGEN,amekabidhi zawadi kwa Chuo kikuu katoliki cha Afrika Mashariki (CUEA) Balozi wa kitume nchini Kenya,Sudan na Eritrea Askofu Mkuu Hubertus Matheus Maria van MEGEN,amekabidhi zawadi kwa Chuo kikuu katoliki cha Afrika Mashariki (CUEA) 

Kenya:Chuo Kikuu cha Afrika Magharibi (Cuea) kimepokea vitabu na fedha!

Balozi wa kitume wa Kenya,Sudan na Eritrea askofu Mkuu Hubertus van Megen amekabidhi zawadi kwa Chuo Kikuu cha Afrika Magharibi (CUEA)vitabu na fedha za kuwezekeza kwenye suala la kidigitali la Chuo kikuu hicho ili wanafunzi waendelee na mafunzo yao ya karibu na kwa mbali kufuatia na janga la corona linaloendelea.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Mkusanyo wa mamia ya vitabu na pesa za kugharimia mchakato wa kufanya kozi za masomo ya karibu na mbali pamoja na uendeshaji wa utawala, ndivyo Chuo Kikuu cha Katoliki cha Afrika Mashariki (Cuea), jijini Nairobi Kenya kilipokea katika siku za hivi karibuni kutoka kwa Balozi wa kitume wa Kenya Sudan na Eritrea, Askofu Mkuu Hubertus van Megen. Kwa mujibu wa taarifa ya Blog ya AMECEA vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa makamu kansela wa Chuo hicho Padre Stephen Mbugua Ngari, na ambaye ametoa shukrani za kina kwa ishara hiyo ya ukarimu na ambapo amesema inaonesha umakini wa Papa na kwa maana hiyo kwa Kanisa la ulimwengu kwa ajili ya elimu katoliki na utambulisho wake.

“Balozi wa Kitume ametupa vitabu katika taaluma mbalimbali za elimu  zinazojikitia katika nyanja mbali mbali za kitaalimungu, pamoja Sheria za Kanisa, sheria za kiraia, uhusiano wa kimataifa, uchumi, elimu, liturujia na mazingira” ameelezea na  kwa maana hiyo ameongeza “vifaa hivi vitakuwa muhimu kwa wanafunzi wetu katika  utafiti  pia kama  vile maandishi ya utamaduni kwa ujumla kwa sababu yanahusika na masuala ya kihistoria na ya kisasa”. Ameshukuru pia ufadhili wa  Pesa kwa ajili ya chuo kikuu, katika mchakato wa kidigitali ambao ulianza kabla ya dharura ya virusi vya corona wa na azidi ambao  umeonekana kuwa muhimu sana wakati wa karantini  kwa sababu ya janga hilo.

Katika siku za hivi karibuni, chuo kikuu kimeanza tena masomo ya ana kwa ana, yaliyokuwa yamesimamishwa tangu Machi, kufuatia na maamuzi ya Serikali kwa kuanza kufunguliwa polepole kwa vyuo vikuu. Kufunguliwa kwake ni taratibu na kwa kufuata kanuni za afya ili kuzuia kuambukizwa ten , wakati kozi pia za umbali zitaendelea.

Taasisi hiyo ilianzishwa mnamo 1984 na Amecea kama Shule kuu ya kitaalimungu kwa jina Taasisi ya Elimu ya Juu  ya taalimungu na kuzinduliwa rasimu kwa ina la Taasisi ya Juu katoliki ya Afrika Mashariki (CUEA ) mnamo 1985 na Mtakatifu Yohane  Paulo II na  Cuea ikawa chuo kikuu mnamo 1992. Katika mchakato wa miaka hii kwenye Kitivo cha Taalimungu , viemeongezeka  vitivo vingine 10 na  na taasisi nyingine. Kati ya hizi, Nyaraka na  na Sayansi Jamii, Uchumi na Biashara, Uchumi wa viwanda, Sayansi ya Maktaba. Taasisi ya Sheria ya na Kituo cha Haki za Jamii na Maadili ilizinduliwa mnamo 2003 ili kukuza maarifa ya mafundisho ya Kanisa ya kijamii. Utume wake unaounganishwa ni kukuza ubora katika utafiti, ufundishaji na huduma kwa jumuiya kwa kuandaa viongozi waadilifu wanaoongozwa na utamaduni wa kiakili wa Kanisa Katoliki.

12 October 2020, 15:38