Tafuta

Shukrani kutoka kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) Kardinali Bassetti kwa Papa kwa uteuzi wa Makardinali wapya 13 Shukrani kutoka kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) Kardinali Bassetti kwa Papa kwa uteuzi wa Makardinali wapya 13  

Kard.Bassetti:Shukrani kwa Papa kwa uteuzi wa makardinali wapya

Kama Rais wa Baraza la Maaskofu Italia, Kardinali Guartiero Bassetti kwa niaba yao ametoa shukrani kwa Papa Francisko, kufuatia kuwatangaza majina ya makardinali wateule wapya tarehe 25 Oktoba ambao watakuwa katika baraza la Makardinali tarehe 28 Novemba ijayo .

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Kardinali Gualtiero Bassetti, Askofu Mkuu wa Perugia- Pieve na Rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) kwa niaba ya Maaskofu wa Italia  ameonesha furaha  ya kutangazwa kwa makardinali wateule  hasa kwa Kanisa la Italia ambalo limewapa makardinali sita kati ya kumi na tatu. “Ninatoa shukrani kwa Baba Mtakatifu kwa ajili ya kuwaita ndugu sita ili kuweza kumsaidia katika huduma yake ya Kanisa la ulimwenguni. Kwa Makanisa ya Italia  tunawakabidhi Bwana hawa makardinali wateule”.

Akiendelea kuonesha furaha hiyo Kardinali Basseti kwa ajili ya  makardinali hao kwa upande wa Italia watakoshiriki baraza la Makardniali  tarehe 28 Novemba 2020 ameawataja kuwa ni kardinali mteule Marcello Semeraro, Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza watakatifu  Kardinali mteule Augusto Paolo Lojudice, Askofu Mkuu wa  Siena-Colle Val ya Elsa-Montalcino, Kardinali Mteule Mauro Gambetti, Mfansiskani wa Conventuali , na Msimamizi wa Conventi Takatifu Assisi. Kardinali mteule Silvano M. Tomasi, Askofu Mkuu wa Asolo, Balozi wa Kitume , Kardinali mteule Raniero Cantalamessa, Mkapuchini, na  Mhubiri Mkuu wa Nyumba ya Kipapa, Kardinali Mteule Enrico Feroci, Paroki wa Mtakatifu Maria wa Upendo wa Mungu  huko  Castel  ya  Leva, na kwamba ni matunda  na zawadi ya jumuiya yetu”.

Kwa kuongezea amesema “Tunajua kila mmoja wao na nina uhakika kuwa watajua namna ya kuishi uwajibijaji wao huo wa kina na unyenyekevu”. Kardinali amekumbusha kuwa “Baba Mtakatifu si kwamba anakuza, wala kutoa heshima, wala mapambo; kwa ujumla ni huduma tu inayodai kupanua mtazano na  na kupanua moyo. Urafiki na upendo wa Maaskofu wa Italia, pamoja na kumbu kumbu katika sala, kwa makardinali wapya”, amefafanua.

26 October 2020, 14:49