Tafuta

Inahitajika kuchangia mafunzo ya wataalam wa utetezi ambao wanaweza kuongea juu ya haki za walio hatarini zaidi katika nyakati zetu. Inahitajika kuchangia mafunzo ya wataalam wa utetezi ambao wanaweza kuongea juu ya haki za walio hatarini zaidi katika nyakati zetu. 

Italia:Caritas Internationalis kuanzisha mafunzo ya Sheria ya Maendeleo,sera za kisiasa na utetezi!

Mapambano ya haki za walio hatarini yanahitaji maandalizi ya busara na yenye sifa,kwa mujibu wa Bwana Aloysius John,Katibu mkuu wa Caritas Internationalis,akifafanua kuhusu kozi ya mafunzo ya juu ya Sheria ya maendeleo,sera za kisiasa na utetezi itakayoanza tarehe 14 Januari 2021.Ili kushiriki katika kozi hiyo,lazima ombi liwasilishwe ndani ya tarehe 4 Novemba 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuandaa wahudumu wenye taaluma kwa ajili ya shughuli za utetezi au shughuli zinazohusiana na maendeleo na utekelezaji wa sera za maendeleo ndani ya mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi katika maeneo ya maendeleo na kwa kulinda haki za binadamu. Hili ndilo lengo la kozi ya juu ya mafunzo ya juu katika Sheria ya Maendeleo, sera za kisiasa na utetezi ambayo Caritas Internationalis imeandaa pamoja na Taasisi ya Sekondari ya Mtakatifu Anna huko Pisa,na  ambayo itafanyika kuanzia tarehe 14 Januari 2021.

Ili kushiriki katika kozi hiyo, lazima ombi liwasilishwe ifikapo tarehe 4 Novemba 2020. Caritas Internationalis, ambayo inajikita katika kukabiliana na umaskini na ukosefu wa haki, pia kwa kuunda mazingira ya maendeleo endelevu, imeona kuwa utetezi ni kama njia moja wapo ya kushughulikia ukosefu wa haki, ambayo ni  moja ya sababu kuu za umaskini, na ndiyo sababu imefikiria mafunzo yenye kiwango cha juu. Mapambano ya haki za walio hatarini yanahitaji maandalizi ya busara na yenye sifa, kwa mujibu wa Bwana Aloysius John, katibu mkuu wa Caritas Internationalis. Aidha ameongeza kusema kuwa wanaamini sana katika thamani ya mafunzo na kushiriki maarifa na uzoefu wao. Mpango huu una thamani ya ziada ya kuwa miongoni mwa kozi chache za ushirikiano wa maendeleo zinazozingatia utetezi.

Kozi hiyo ina sehemu mbili: sehemu ya kwanza ya mafunzo ina masaa 120, ambayo, ni kupitia nidhamu mbali mbali ambapo itashughulikia masuala yenye mantiki yya Ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu, (SDGs) kama vile umaskini na ukosefu wa usawa,uhamiaji, mabadiliko ya tabianchi na uwezeshaji; Sehemu ya pili ambayo itakuwa pia  na mafunzo ya masaa 120 katika taasisi na mashirika ambayo yanashirikiana na Shule ya Mafunzo ya Juu ya Mtakatifu Anna, pamoja na Caritas Internationalis.

Kwa kufafanua zaidi Bwana Aloysius John amesema ni shauku yao ya kuchangia mafunzo ya wataalam wa utetezi ambao wanaweza kuongea juu ya haki za walio hatarini zaidi . Wakati huu wa janga, Caritas inazingatia hasa shughuli za utetezi na kushughulikia dhuluma kubwa za hivi sasa za kijamii, hasa katika kiwango cha uchumi. Kwa mfano wanajtahidi  kuomba kufutwa kwa deni la nchi maskini na uhamishaji wa fedha kwenye mipango ya maendeleo ya jamii mahalia zinazosimamiwa na mashirika ya kidini kama Caritas ”.

14 October 2020, 15:23