Tafuta

2019.02.19:Kituo cha Mapokezi ya watoto cha Caió, nchini Guinea-Biassau 2019.02.19:Kituo cha Mapokezi ya watoto cha Caió, nchini Guinea-Biassau 

Guinea Bissau:Mipango yakimisionari inayosaidiwa na maaskofu wa Brazil yaleta tumaini katika nchi!

Kanisa letu limekua katika kuelewa umuhimu ambao sisi sote tuliobatizwa tumetumwa.Na kuhani aliyefundishwa vizuri na aliye na nia nzuri ni baraka kubwa kwa jumuiya yote ya Kanisa na kwa wakazi wote wa nchi.Ni pongezi za Askofu wa Guinea Bissau kwa Kanisa nchini Brazil linalosaidia utume nchini humo na mafunzo kwa makuhani wa kesho,katika fursa ya siku ya kimisionari ulimwenguni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mshikamano na utume havijuhi mipaka. Wanatambua vema waamini wa Guinea - Bissau ambao wa kwa miaka kadhaa wanapokea msaada kutoka katika Kanisa Katoliki la Brazil. Kwa njia ya tume ya Maaskofu kwa ajili ya shughuli za kimisionari na  ushirikiano muungano wa makanisa kwa dhati maaskofu nchini Brazili walianzisha katika nchini ndogo mipango miwili ya kimisionari. Mpango wa kwanza unaendelea katika jimbo la Bissau ambao unaitwa Utume wa Mtakatifu Paulo VI, ulioanzisha mnamo 2012  kwa kujikita katika sekta ya uinjilishi, afya, na mafunzo. kwa mantiki hiyo, kwa namna ya pekee, tarehe 15 Oktoba 2020 umezinduliwa pia  shule ya awali yenye watoto 90 waliogawanyika katika madarasa matatu.

Mpango wa pili wa kimisionari utazama  jimbo la Bafatá, mahali ambapo mwaka 2004 walianzisha program ya mshikamano kwa ajili ya mafunzo ya vijana wanaonjiandaa kuwa makuhani wa kesho. Tangu 2019, mpango huo pia unasaidiwa na Taasisi ya Kipapa ya Chuo Kikuu katoliki cha Rio de Janeiro ambacho kinatoa kozi za uzamili na udaktari. Hiyo yote shukrani kwa Kanisa nchini Brazi ambao wanatuma walimu wao na progma zao zina mafanikio makubwa kwa mujibu wa askofu Pedro Carlos Zilli wa jimbo la Bafatá.

Akifafanua zaidi kuhusu mafunzo hayo amesema “haya ni mabadilishano ya kiutamaduni ambayo kila mtu ukua kama waalimu, jamuiya, jimbo parokia, makanisa katika nchi zao”. Walakini, shida hasikosekani kwani waalimu ambao wanafikia kutoka Brazil, kwa mujibu wa Askofu “wanakaa Guinea- Bissau kwa muda kidogo  wa mwezi na nusu, wakati ambao wanapaswa kutoa kozi kubwa inayofanana na wale nusu mwaka. Lakini kwa neema ya Mungu matokeo ni sawa sawa kwa wote”. Kwa njia hiyo amesema “Kanisa letu limekua katika kuelewa umuhimu ambao sisi sote tuliobatizwa tumetumwa. Na kuhani aliyefundishwa vizuri na aliye na nia nzuri ni baraka kubwa kwa jamii yote ya kanisa na kwa 'wakazi wote wa nchi'.

17 October 2020, 15:34