Tafuta

Mafuriko nchini Ghana Mafuriko nchini Ghana 

Ghana:mafuriko Kaskazini Mashariki ya nchi watu kuhitaji msaada!

Kufuatia na mafuriko Kaskazini Mashariki mwa Ghana,Kanisa limetoa wito huku wakiomba msaada kwa ajili ya kutatua matatizo makubwa ya bwawa la Bagre karibu na nchi ya Burkina Faso.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Watu 7 na zaidi ya watu 19,000 wamekundikana ndani ambao  na kati ya hao ni watoto 6,000,  nyumba 2653 zilizo haribika na karibia Hekari 4,500 za mazao yalisombwa na maji. Ndiyo tathimini ya mafuriko katika Mkowa wa Kaskazini Mashariki na Kusini Mashariki mwa  Ghana kwa pigo  la wiki hizi na kuongezea kufurika kwa Bwawa la Bagre, karibu na nchi ya Burkina Faso.

Bwawa linalomwaga maji tangu tarehe 10 Agosti limekuwa moja ya safu za matatizo ambayo yamekuwapo, kwani ni karibu miaka 20 sehemu hiyo imekuwa chini ya maji kwa sababu ya mafuriko ya Bwawa na  kusababisha waathirika wengi na madhara ya vifaa vingi. Kanisa la Ghana mara moja limeweza kuwa mstari wa mbele  kutoa msaada kwa njia ya Caritas ili kuwasaidia watu mahalia na kwa namna ya pekee katika jimbo la Navrongo-Bolgatanga, ambalo linafunika karibu wilaya 8 ambazo zimepata pigo kubwa. Mipango ya upendo kwa upande wa maaskofu limekwisha wakabidhi vyakula na vifaa vingine vyenye thamani ya Dola 13,000 na hundi ya fedha dola  1.900  ili waweze kununua vyakula.

Kiasi cha fedha kwa mujibu wa shirika la Habari katoliki Afrika, zimekabidhiwa katika afla fupi ya  tarehe 28 Setemba 2020  na Mratibu wa Kitaifa wa Caritas nchini Ghana, Bwana Zan Akologo,  kwa Askofu mahalia Alfred Agyenta na ambaye amethibitisha hali mbaya sana. Hata hivyo kiwango kamili cha janga la kibinadamu bado hakijajitokeza, kwa sababu bado kuna athari zinazowezekana kutoka kutokana na uchafuzi wa maji unaondlea kusababishwa na mafuriko, amesema kiongozi huyo, ambaye pia ameonyesha athari za mafuriko kwenye mazao yajayo na kuomba misaada mingine kwa ajili ya watu walioathirika.

Wito ambao  Unatoka Caritas mahalia anautuoa akiunga  mkono na kukumbuka ushauri wa Baba Mtakatifu Francisko watu wasijihisi kuzidiwa na dharura ya kibinadamu, lakini kupata majibu kwa njia ya mshikamano wa kindugu. Mkuu wa Caritas pia alichukua fursa hiyo kuangazia hitaji la kutatua shida ya mafuriko yaliyosababishwa na bwawa la Bagre akikumbuka kwa maneno ya Waraka wa Laudato si  kwamba “kilio cha dunia ni pia kilio cha maskini”. Na jitihada za kupata suluhisho la kudumu katika  shida hii sugu limetoka kwa Makamu Rais wa Ghana, Mahamudu Bawumia aliyetembelea maeneo yaliyoathiriwa mnamo tarehe 10 Septemba 2020.

01 October 2020, 13:57