Tafuta

Ubatizo ni kisima na mzizi wa maisha ya kikristo Ubatizo ni kisima na mzizi wa maisha ya kikristo 

Congo Brazaville:Ubatizo ni sakramenti isimikayo mizizi ya maisha ya kikristo!

Kanisa la Congo Brazaville wamefunga na kufungua mwaka mpya wa kichungaji 2020/2021 ambapo Kiongozi wake anapendekeza tena mada ya Ubatizo kama sakramenti ambayo maisha ya kikristo yamesimikwa mizizi yake.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Janga la Covid-19 lilikuwa kikwazo cha kweli na na kipindi cha  kuumiza kwa ulimwengu wote. Na kwa Kanisa letu. Kwa malengo ambayo tulijiwekea mwanzoni mwa mwaka wa kichungajitukubali uthibitisho huu wa Covid-19 kwa imani ambamo tunaweza kuingia katika mantiki ya Mungu.  Hata katika kushinda kwa upande wetu ni ubaya unaoweza kuzuiwa na kuona kwamba ni kisiki cha kupitia ambacho Mungu ametumia kwa ajili ya  hatma yetu. Ni k ufupisho wa maneno ya Askofu Mkuu Anatole Milandou, Askofu Mkuu wa Congo Brazzaville,katika kuanza mwaka mpya wa kichungaji ambao amepitia katika jimbo lake huku akibainisha ni kwa kiasi gani dharura ya virusi vya corona vimeathiri maisha ya Kanisa.

Kwa mujibu wa taarifa za kutoka Gazeti la Wiki za ya Kanisa (Semaine Africaine),askofu amezungmza hayo katika hotuba ya kufunga mwaka wa kichungaji  2019-2020, Jumatatu  28 Septemba 2020 iliyopita katika ukumbi wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu katika mji mkuu, huku hakikimbuka mada ambayo waamini walikuwa wameitwa kutafakari kuhusu  ubatizo na athari zake kwa maisha ya Kikristo ya kila mtu. “Nilikuwa nimeaalika kuwa na ufahamu, na  kuchukua jukumu katika moyo wa jamii yetu iliyopotea, ili kurudi kwenye misingi ya imani yetu” , ameongeza Askofu Mkuu  Milandau ambaye kwa mwaka mpya wa uchungaji 2020-2021 ameamua kupendekeza tena mada ya ubatizo .

Askofu mkuu kwa kusisitiza zaidi amesema "Umuhimu ninaoutoa kwa sakramenti ya ubatizo umenichochea kurudia mada hiyo hiyo hasa ​​ kwa sababu haikuendelezwa, kama ilivyotarajiwa, pia msisitizo ni kuwa mizizi katika Kristo. Kwa sababu maisha yote ya Kikristo yamesimika mzizi wake wote  katika ubatizo". Kwa upande wa askofu mkuu wa Brazzaville, sakramenti ya ubatizo ni roho ya maisha ya Kikristo ambayo Kristo ni shina lake, ni mlango wa imani na kuingia ndani ya Kanisa na kumfanya yule aliyebatizwa kuwa mtu mpya. Hatimaye  akiufungua rasmi mwaka mpya wa kichungaji, kiongozi huyo amehimiza kila mtu kuishi ahadi zao za ubatizo, kuunga mkono katika lengo hili na kudumisha na kukaa kwa umoja.

02 October 2020, 15:43