Tafuta

2019.11.26 Maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Senagal,Mautitius,Capo Verde na Guinea Bissau 2019.11.26 Maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Senagal,Mautitius,Capo Verde na Guinea Bissau 

Capo Verde-Askofu wa Mindelo:Kuelimisha umoja na mshikamano

Janga limebisha hodi katika milango yetu na kuonesha wazi udhaifu wetu na kuondoa mipango yetu kwa kutufanya tutambue vema udogo na udhaifu tulio nao.Zaidi ya hayo ni ukweli kwamba wakati wa shida,ni lazima na wakati wote kutegemea kupokea na msaada wa ndugu zetu.Ni katika maelezo kutoka barua ya kichungaji 2020-2021 ya Baraza la Maaskofu wa Capo Verde.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuelimisha maadili ya umoja na mshikamano kwa ajili ya kurudisha ubinadamu katika moyo wa mtu ndiyo ushauri uliolekezwa kwa waamini na Askofu Ildo Fortes, wa jimbo katoliki la Mindelo, huko  Capo Verde,yaliyomo kwenye barua ya kuchungaji kwa mwaka 2020-2021. Waraka huo wa kichungaji wa Baraza la Maaskofu kwa namna ya pekee unaangazia mambo mawili muhimu. Kwanza kuhusu janga la virusi vya corna  na wakati huo huo jambo la pili ni kuhusu udugu na urafiki kijamii ambao ni matashi makubwa ya Papa Francisko katika “Waraka wake wa  “Fratelli tutti”, yaani Wote ni ndugu uliotangazwa mnamo tarehe 4 Oktoba 2020.

Janga limebisha hodi katika milango yetu na kuonesha wazi udhaifu wetu na kuondoa mipango yetu kwa kutufanya tutambue vema udogo na udhaifu tulio nao.Zaidi ya hayo ni ukweli kwamba wakati wa shida,ni lazima na wakati wote kutegemea kupokea na msaada wa ndugu zetu.  Lazima tuungane na tufanye mshikamano tena ikiwa hatutaki kuzama, kwa mujibu wa waraka huo.  Na kwa maana hiyo huo wito wake kwa wakati huu ni ule wa kuwa na tumaini, kutembea pamoja ili kugundua ubinadamu mpya unaokaa ndani mwao na kuwaimarisha furaha ya mshikamano.

Askofu wa Mindelo katika barua hiyo haifichi,  shida nyingi ambazo waamini wa nchi hiyo wanajikuta na wakikumbana nazo leo hii: “Umaskini na hali ya wasiwasi kiukweli yalikuwa tayari ni mamabo ambayo yapo kwa   walio wengi, lakini sasa wanachukua mitindoa mingine mipya kwa sababu ya janga la uchumi. Kwa sababu hiyo, jukumu la familia linabaki kuwa kitovu.  Familia ni hazina ya ubinadamu  na ni muhimu kujitoa kwa upyaisho wa uchungaji wa vijana na elimu ya haraka katika maadili hayo ya kijamii ambayo yanahitaji ukuaji mara moja, amesisitiza.

Sasa zaidi ya hapo awali, familia mabayo ni  Kanisa  nyumbani linaitwa kuchukua nafasi yake kuu  ya kutoa  maamuzi kwa ajili ya kuponyesha ubinadamu katika moyo wa mwanadamu. Na ubinadamu ambao Askofu Fortes anamaanisha ni kwa  yule anayejua jinsi ya kuangalia maadili ya kweli ambayo Mungu Muumbaji amepanda ndani ya mioyo ya watu wote: upendo, ukweli, haki, mshikamano, heshima kwa yule anayeitwa, kama yeye, kuishi na uhuru na hadhi katika ardhi moja. Ni ubinadamu kwa maana ya kuleta njia mpya ya kuishi katika jamii, kwa sababu anasema “tunahitaji jamuiya inayotuunga mkono na ambayo ndani yetu tunasaidiana kutazama mbele kwa matumaini”. Akiwaelekeza kwa namna hiyo wanafamilia wote, jumuiya, walimu na watoa huduma Askofu wa Mindelo amewashauri kutimiza kazi ya umisionari kwa kuhamasisha zaidi mshikamano katika moyo wa kila mwanamke na mwanaume.

Familia, kiukweli, zinaitwa katika utume wa elimu msingi na ya  lazima kwa sababu ndiyo mahali pa kwanza ambapo maadili ya upendo na udugu yanaishi na kupitishwa; jumuiya za parokia na shule, kwa upande mwingine, lazima ziwe na utambuzi wa  kazi nzuri waliyonayo, ambayo ni kuelimisha katika maadili hayo ambayo husaidia kufikiria juu ya maisha ya mwanadamu kwa njia ya umoja zaidi na kuchangia katika kuboresha jamuiya hizo. Kwa kuongezea, Askofu  Fortes anawakumbusha vijana umuhimu wa kuchukua majukumu ndani ya jamii na kuishi na wengine kwa tabia ya kujitoa na upendo wa kidugu, ukarimu na huruma, kwa sababu ni suala la kukumbatia changamoto ya Kanisa linalotoka nje na kutomsahau jirani yoyote kwa sababu ya  wasiwasi binafsi na shida maalum.

Kwa kuhitimisha anasema askofu wa Capo verde kuwa kwa kutiwa moyo na uhakika wa tumaini la Kikristo tutaweza kuponya mioyo isiyotulia na kuzishinda nyakati za kuchanganyikiwa za historia yetu anasema na kwa sababu Neno lilolofanyika mwili lina uwezo wa kubadilisha na kuamsha ubinadamu mpya. Shida, kiukweli ni fursa ya ukuaji, siyo kisingizio cha kuwa na  huzuni.

13 October 2020, 13:35