Tafuta

Vatican News
Askofu Mkuu Franz Lackner, wa Jimbo Kuu latoliki la  Salisburg na rais wa Baraza la Maaskofu nchini Austria. Askofu Mkuu Franz Lackner, wa Jimbo Kuu latoliki la Salisburg na rais wa Baraza la Maaskofu nchini Austria. 

Austria:Maadhimisho ya kiekumene na Bunge:Tunarithishaje maadili kwa kizazi?

Kila kizazi kina alama ya maadili.Je ni maadili yapi yamesambaratika,yamefutwa au hata kupunguzwa thamani yake.Sisi pia tutalazimika kujiuliza ni kwa jinsi gani ufahamu wetu wa maadili tuliyokabidhiwa tumeshughulikia vipi na jinsi gani tulivyouruthishwa kwa wengine”.Ni tafakari ya rais wa Baraza la Maaskofu nchini Austria kwa viongozi na bunge zima nchini humo katika fursa ya ufunguzi wa bunge 2020/21.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Jumanne tarehe 13 Oktoba 2020 katika Kikanisa kidogo cha Hofburg jijini Vienna, yamefanyika maadhimisho ya kiekumene pamoja na Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Austria, Askofu Mkuu Franz Lackner, Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox Arsenios Kardamakis na Mwenyekiti wa Kanisa la Kiinjili Ingrid Bachler, kwa ushiriki wa wabunge wote wa vyama vya kisiasa ambao wanaunda Bunge la Austria. Hizi ni taarifa kutoka katika tovuti ya Baraza la Maaskofu katoliki nchini Austria ambapo linabinisha kuwa Askofu Mkuu Franz Lackner ametoa wito kwa wanasiasa ili wasichukulie maadili ya kijamii kama kawaida, kwani kwa upande wake Askofu Mkuu anasema kiukweli, isingewezekana raia kuwa uhuru ikiwa anakosea kuwa na marejeo ya asili ya kidini.

Tukio hili lilifanyika katika fursa ya ufunguzi wa kikao cha bunge kwa mwaka 2020/2021, ambacho kilihudhuriwa na wabunge kutoka vyama vyote, Rais wa Baraza la Kitaifa Bwana Wolfgang Sobotka na Rais wa Baraza la Shirikisho, Bwana Andrea Eder-Gitschthaler. Wakati wa mahubiri yake Askofu Mkuu Lackner ameongozwa na sehemu ya Injili ya Yesu mahalia anapowaita wakristo wawe ‘mwanga na  chumvi ya Dunia’. “Yesu hazungumzii juu ya  sahani msingi ya chakula;au  chakula kizuri cha Vienna, wala keki tamu, lakini chumvi, ambayo uongezwa kwa sababu huwezi kuila bila kuongeza kitu kingine”, amesema.

“Kuna jukumu la mwisho ambalo haliwezi kukwepwa Askofu Mkuu amesema akihutubia wawakilishi hawa  wa ulimwengu wa kisiasa na  kwamba ni muhimu kukumbuka kuwa maadili pia yana asili ndefu: hatupaswi kutarajia kuwa na uwezo wa kuyatoa kutoka wakati huu, au kutoka katika hali fulani. Lazima tuzingatie asili ya maadili haya, asili ambayo inakusanya maarifa ambayo yamekua kupitia historia, uzoefu uliokusanywa, maendeleo na kutofaulu kwa historia ya wanadamu na kwa maana hiyo inathibitisha uendelevu wake”, amebainisha Askofu Mkuu huyo. “Kila kizazi kina alama ya maadili, amesisitiza rais wa Baraza la  Maaskofu nchini Austria.  Je ni maadili yapi yamesambaratika, yamefutwa au hata kupunguzwa thamani yake. Sisi pia tutalazimika kujiuliza ni kwa vipi ufahamu wetu wa maadili tuliyo kabidhiwa tumeshughulikia vipi na jinsi gani tulivyopitisha au kurithisha kwa wengine”.

Katika muktadha huu, kiongozi huyo ametaja kwa mfano Mkataba wa Haki za Binadamu, ambao unategemea dhana ya hadhi binafsi, ambayo ni pamoja na kuheshimu maisha ya mwanadamu, tangu mwanzo hadi mwisho wake. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Lackner, dhana hii ilianzia katika historia ya fikira na imani ya Ugiriki, ya Wayahudi na Wakristo. Na kwa maana hiyo “Kama makanisa ya Kikristo na jamuiya za imani tuna jukumu la kuwa walinzi wa chumvi hiyo, ili isikose radha yake. Tunatoka katika mila ambayo ilitufundisha kutosimamia majivu tu, lakini kuhifadhi moto. Ongezeko la chumvi, husaidia kutokuwaharibu maadili na ni dhamana kwa muda wa maadili tunayoyaamini”, aamekazia Askofu Mkuu.  Hatimaye askofu mkuu ametoa maneno ya shukrani kwa mafanikio ya kisiasa na mamlaka ya umma na shukrani hizo pia zimeungwa mkono kamaa ilivyokuwa miaka ya nyuma, na katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu, Askofu Peter Schipka, ambaye ni muhamasishaji wa maadhimisho ya kiekumene kwa ulimwengu wa siasa.

16 October 2020, 11:12