Tafuta

Askofu Mkuu Pizzaballa Msimamizi wa Kitume wa Upatriaki,Yerusalem Askofu Mkuu Pizzaballa Msimamizi wa Kitume wa Upatriaki,Yerusalem 

Ask Mkuu Pizzaballa:kuna ulazima wa kuaminiana kati ya Israeli na Palestina!

Katika mkutano uliofanyika kwa kwa njia ya mtandao,msimamizi wa Kitume wa Upatriaki wa Yerusalem,Askofu Mkuu Pizzaballa amesema hali ya sasa ya Nchi za mashariki ni matatizo makubwa na kwa maana hiyo mchakato wa kutata suluhisho la njia ya wakati ujao japokuwa ni ngumu ni kujenga imani.Hii kwa mujibu wake amesema kujenga kuta ni ishara ya ukosefu wa imani.

Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Umefanyika mkutano mjini Roma katika makao makuu ya Shirika la Kaburi Takatifu, kwa njia ya mtandao, ukiongozwa na mada ya " Nchi Takatifu na Mashariki ya Kati. Matarajio mema ya wakati huu”. Aliyendaa Mkutano huo ni Kardinali Fernando Filoni, Mkuu wa  Shirika la Ulinzi wa Kaburi Takatifu Yerusalem katika muktadha wa Siku kuu ya Mama yetu wa Palestina, msimamzi wa Shirika hilo ambayo itafanyika tarehe 25 Oktoba. Akijibu maswali ya Mwandisi wa Rai, Piero Damosso, Msimamzi wa Upatriaki wa Yerusalem Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa,ametazama hali halisi ya nchi za Mshariki na kwamba watu wa Palestina bado wametengwa.

Ugumu wa kuwa na msimamo wa nchi za Masshariki.

Akifafanya zaidi amesema kuwa makubaliano kati ya Israeli na Nchi za Falme za uarabuni kwa kusaidia na Trump zimebagua kwa mara nyingine tena zaidi wapalestina. Masuala ya Israeli na Palestina yalikuwa tayari kwa kipindi siyo ajenda ya umma kimataifa. Wapalestina kwa muda mrefu wamebaguliwa. Kwa sasa kulingana na ulimwengu wa kiarabu, bado wanazidi kutengwa. Ni lazima kijiuliza ni jinsi gani ya kwenda mbele. Ikiwa hapatakuwapo na suluhisho lililo wazi na lenye hadhi kwa watu wa Palesinta itakuwa vigumu kuwa na msimamo wa Nchi za Mashariki, amesisitiza. Pia masuala ya kipalestina yanaingia ndani ya mantiki ya mabadiliko ya nchi  za Mashariki  kwani hasa kuna suala la Lebanon, la Siria, Uingiliaji wa Erdogan unaonyesha wazi kabisa jinsi mali zote katika nchi za Mashariki ya Kati, zinavyobadilika. 'Wachezaji' wakubwa ni Uturuki, Falme za Urabuni, Saudi Arabia na Iran. Pia kuna Urusi, Marekani na China. Lebanon na Siria, hata Iraq zinajikuta kama uwanja wa vita. Na Ulaya ambayo imezama zaidi katika shida zake, inaonekana kuwa imesahau ajenda ya kimataifa amebainisha Askofu Mkuu 

Suluhisho la nchi hizo mbili

Katika picha hii ngumu ya hali halisi ya nchi hizo Askofu Mkuu Pizzaballa amebainisha suala ambalo linaweza kuleta suluhisho la watu wa Nchi hizo mbili. "Hata kama kuzungumza juu amani ni vigumu ambapo  utafikiri hakuna njia ya kupitia lakini wakati huo huo tunajiuliza ni nini tunaweza kufanya na kwa  sababu katika wakati huu hakunamazungumzo kati ya sehemu mbili ya  Israeli na Palestina kwani  hawajazungumza kwa miaka kadhaa na kuna ukosefu wa uaminifu".  "Jumuiya ya kimataifa kiukweli haipo tena kwa hivyo tunashuhudia hali ya kusimamishwa, na ya  kusubiri ”. Kwa maana hiyo Askofu Mkuu amesema njia ipo lakini kitaalam haionekani kuwa inawezekana. Ili kufikia amani ambayo leo inaonekana kuwa ngumu ,tunahitaji kufanya kazi kwa muda mrefu. Lakini ungumu huo unaoonekana kwa  sasa hauwezi kuzuia kujenga siku zijazo". Na mustakabali wa Israeli na Palestina, kwa mujibu wa Askofu Mkuu  Pizzaballa mesema, "juu ya yote inahitaji jambo muhimu kama “gundi”.

Ukuta unaogawa ni ishara ya ukosefu wa kuaminiana

Katika kusisitiza juu ya hali hiyo Askofu Mkuu amesema "Kuna haja ya kujenga imani kati ya watu hawa wawili, ambao kwa sasa hakuna. Ukuta uliopo na inaogawanya, pia ni ishara ya ukosefu wa matarajio na kuaminiana. Zinahitajika ishara kwamba kidogo inawezekana kujenga upya imani, na hii haifanyiki kati  leo na kesho, inahitaji pia maono na uongozi bora. Lazima tuanze upya, tukizingatia mafundisho  ya zamani, pamoja na kushindwa kwa Oslo na mikataba  mbalmbali. Na hii itachukua muda".

23 October 2020, 10:16