Tafuta

2020.10.25 Mons. Antoine Kambanda,Askofu Mkuu Kigali/Rwanda ameteuliwa kuwa Kardinali 2020.10.25 Mons. Antoine Kambanda,Askofu Mkuu Kigali/Rwanda ameteuliwa kuwa Kardinali 

Ask.Mkuu Kambanda:Kuwa kardinali ni furaha na changamoto

Askofu Mkuu wa Kigali ni mmoja wa makardinali 13 wapya waliotangazwa na Papa Francisko kuunda Baraza la Makardinali kunako tarehe 28 Novemba 2020 katika mkesha wa Dominika ya Kwanza ya Majilio.Kardinali mteuli ameeleza jinsi alivyopokea tangazo hilo akihojiwa na Vatican News.Ninamshukuru Bwana kwa sababu ndiye Bwana wa historia".Yuko tayari kumtumikia Mungu zaidi kwa nafasi hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Mara baada ya tangazo la makardinali wapya watakao ongezeka kuunda Baraza la Makardinali kunako tarehe 28 Novemba 2020 katika mkesha wa Dominika ya Kwanza ya Majilio, Kardinali mteule  wa Jimbo Kuu la Kigali Rwanda  ambaye ni mmoja kati ya wateule 13 akihojiwa na Vatican News amesema  kuwa “ umekuwa mshangao mkubwa kwangu. Sikutegemea. Nilikuwa katikati ya maisha yangu ya kawaida na mtu mmoja akaniita kwa simu. Sikuweza kuamini. Lakini baadaye nikasikia tangazo la Papa wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana. Nilishangaa".  Aidha ameongeza kusema kuwa "Ninamshukuru Bwana kwa sababu ndiye Bwana wa historia, kwa jumla au historia ya binafsi. Sikuwahi kuota kuwa Kadinali", ameeleza mteule na kwamba ni mapenzi ya Bwana. Kama Injili ya Jumapili ilivyosema, ninampenda Bwana na nimejitoa maisha yangu kumtumikia. Kuwa Kardinali kunanipa nafasi ya kufanya kazi zaidi kwa ajili ya Bwana. Ninamshukuru sana Baba Mtakatifu kwa kunikabidhi ofisi hii. Ninapenda Kanisa, ninapenda kufanya kazi kwa ajili ya Kanisa na hii itanipa nafasi ya kujitoa zaidi kwake".

Kwa maneno hayo yanaonesha hisia za nguvu za Kardinali mteule Antoine Kambanda, askofu Mkuu wa Kigali Rwanda ambaye ni mmoja wa makardinali 13 waliotangaza na Papa Francisko baada ya sala ya Malaika wa Bwana tarehe 25 Oktoba 2020. Kardinali mteule akijaribu kujibu kuhusu kipindi kigumu walichokipitia nchini mwao hasa suala la kuponesha majeraha na kuishi mapatano hasa katika changamoto ambazo pia atakabiliana nazo kama Kardinali katika kipindi ambacho Papa Francisko ametangaza hivi karibuni Waraka wa Fratelii tutti, amethibitisha juu ya kuhitimisha hivi karibuni miaka 26 tangu  yafanyike mauaji ya kimbari na kwamba wamefanya kazi sana kwa ajili ya upatanisho.

kwa mujibu wa Kardinali mteule amesema "Ilikuwa ni chungu sana kuona jamuiya ya Wakatoliki na Wakristo imetengana, wakiuana hadi mauaji ya halaiki. Tunamshukuru Bwana kwa njia ambayo tumechukua hadi sasa. Kwa sasa, hata hivyo, tumefikia kiwango cha upatanisho na umoja, na Waraka wa Papa kuhusu " Fratelii tutti" yaani “Wote ni Ndugu umepokelewa vizuri nchini Rwanda. Tunatafakari kwa sasa na kuweka makini zaidi.  Waraka huo utaimarisha na kuwezesha kazi yetu ya kichungaji katika mantiki ya upatanisho. Kwa sasa ni changamoto kwangu, kwani kuna jukumu hili katika uinjilishaji, ndani ya Kanisa la ulimwengu: Ninapenda pia kutoa ushuhuda wa kujitoa kwangu, kwa kile kinachowezekana kushirikisha na wengine ambao wanateseka sana pia kutokana na mizozo na vurugu ya jamuiya”. amesisitiza kiongozi huyo.

Akijibu swali kuhusu kuteuliwa kuwa Kardinali wa Kanisa la Ulimwengu hasa kipimo cha ukuu wa ofisi hiyo katika imani ambayo Kanisa limekabidhi, kwa kuzingatia kwamba Kardinali Mteule  hapo awali aliteuliwa kuwa Askofu wa jimbi la Kibungo kunako tarehe 7 Mei 2013 na tarehe 19 Novemba 2019 Papa Francisko akamteua kuwa Askofu Mkuu wa Kigali na sasa Kardinali. Kardinali Mteule ameshukurnu Mungu kwa neema hiyo ambayo inatendeka ndani ya Kanisa lake ambalo kwa sasa linaendelea kukabiliana na changamoto tofauti. Amesisitiza kuwa lazima kufanya kazi kwa nguvu zaidi ili kueneza na kufanya kuwa na uelewa wa Ujumbe wa wokovu. Na wakati huo huo ni furaha na jitihada kubwa na changamoto.

Hata hivyo Nchini Rwanda, Kardinali mteule ni wa kwanza katika historia ya Kanisa hilio. Shirikisho la Baraza la Maaskofu wa Afrika ya Kati (ACEAC) ambalo linajumuisha nchi ya Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi, walikuwa na Kardinali mmoja wa Congo. Na sasa kwa furaha kubwa katika Kanda ya Maziwa makubwa na kwa ajili ya shirikisho la mabaraza limempata Kardinali wa pili. Kwa kuhitimisha Kardinali mteule katika kutoa ujumbe kwa watu wak ewa Rwanda kwa furaha hiyo ya kuwa na kardinali wa kwanza hata katika Kanda ya Maziwa makubwa amesema “Ninawashukuru sana maaskofu wenzangu wa Rwanda na ACEAC kwa ushirikiano wao, mshikamano na kazi tunayofanya. Ikiwa Papa ameniteua kuwa kardinali pia ni shukrani kwa imani, kazi na shughuli za kichungaji za jumuiya nzima. Ninawahakikishia ushirikiano wangu na mshikamano, hasa kwa amani na maridhiano katika Kanda. Tunaishi wakati wa mvutano, uliochanganywa na janga la Covid-19. Kama wachungaji, lazima tuongoze watu kwa amani na udugu. Katika muktadha huu, Waraka wa Fratelli tutti yaani Wote ni ndugu  utatuangazia na kutusaidia sana katika kazi yetu ya uchungaji , ya upatanisho na udugu katika Kanda”.

27 October 2020, 08:46