Tafuta

Vatican News
Hati udugu kibindamu Hati udugu kibindamu 

Algeria:Hati ambayo inaeleza mambo muhimu maalum ya Kanisa!

Hati hiyo inazungumza kwa namna maalum kwa sababu inaelezea wazi fursa ya mazungumzo na waislam na ambayo inakwenda sambamba na maelezo kamili kati ya Papa Francisko na Imam mkuu kwa ajili ya kuhamasisha udugu wa ulimwengu na amani ya kuishi kati ya watu.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni matumaini ya nguvu ambayo yanarudisha dhamiri ya ubinadamu na  hatua ya safari kuelekea udugu  uliopendekezwa na Hati ya Pamoja kuhusu udugu wa kibinadamu, uliotiwa saini na Papa Francisko na Imam Mkuu wa Al-Azhar Ahmad al-Tayyeb.  Ndivyo anasema Askofu Mkuu Paul Desfarges, Jimbo Kuu katoliki la Algeria, akihojiwa na Shirika la habari kuhusiana na Waraka wa wa Papa Francisko “Fratelli tutti yaani Wote ni ndugu” uliotangazwa hivi karibuni.

Hati hiyo kwa mujibu wa taarifa imegusa karibu sana Askofu Mjesuit wa kifaransa ambaye kwa miaka 50 anatoa huduma nchini Algeria na anaishi kwa namna hiyo uzoefu wa mazungumzo ya kidini katika nchi hiyo ya Kiislam, mahali ambapo wakatoliki kwa namna nyingine ni  wachache. Kwa mujibu wake anasema Hati hiyo inazungumza kwa namna maalum kwa sababu  inaelezea wazi fursa ya mazungumzo na waislam na ambayo inakwenda sambamba na maelezo kamili kwa mafundisho  ya dhati yanayopatikana ndani ya hati iliyotiwa saini  kati ya Papa Francisko na Imam mkuu kwa ajili ya kuhamasisha udugu wa ulimwengu na amani ya kuishi kati ya watu.

Ni jitihada ambazo zinaeleza kwa mara nyingine tena sababu ya tumaini na ishara, chachu ya mchakato wa safari ya udugu, kwa mujibu wa Askofu Mkuu wa Algeria na ni safari ambayo daima ni sehemu fungamani ya maisha na utume wa Kanisa nchini Algeria. Kwa upande wao, lazima kuzingatia uwepo wa Kanisa katika mwendelezo wa uhusiano na uwepo hai ikiwa inawezekano wa kutekeleza udugu kwa ndugu, kaka na dada waislam. Kile ambacho Papa Francisko anasema Kanisa lipo kwa ajili ya kutoka nje na kwenda kukutana na wenginewa pembezoni mwa maisha na siyo kusimama. Kanisa ambalo linaishi kama waamini katika Mungu mpendelevu kwa viumbe wake na wote ni ndugu na tunaweza kuishi kama ndugu kweli.  Aidha kwa mujibu wa Askofu mkuu, tendo la Papa pia linavutia hata mfano wa Mwenyeheri  Charles de Foucauld  na ni muhimu kwa sababu uhusiano na mwengine, wa kina na ambao wakati endelevu aliweza kuuishi hadi mwisho na ndicho kinatoa maana ya maisha ya udugu na kuishi Kanisa kikamilifu.

Hatimaye akieleza  matokeo  ya jitihada hizo za Papa Francisko za kutaka kujenga daraja la udugu, Askofu mkuu amebainisha hata tathimini  ya Hati ya pamoja kwa upande wa viongozi wakuu wa kisuuni na ambao anasema ni ishara ya nguvu. Inamshangaza kuona nafasi hiyo ya msimamo hasa dhidi ya kutumia nguvu za kigaidi. Kwa mfano amesisistiza kwamba Mungu anajilinda peke yake na ndiyo linapaswa kukumbushwa kwa wote leo hii! Waislam wengi wanataka hili la usalama wa kuishi vizuri na mazungumzo ya kweli.

13 October 2020, 13:07