Tafuta

Sherehe ya Ekaristi inautambulisho muhimu wa pamoja kwa Wakatoliki na  mara nyingi huadhimishwa katika kumbukumbu ya shughuli za Yesu Kristo katika  kuokoa  kwa njia ya sakramenti. Sherehe ya Ekaristi inautambulisho muhimu wa pamoja kwa Wakatoliki na mara nyingi huadhimishwa katika kumbukumbu ya shughuli za Yesu Kristo katika kuokoa kwa njia ya sakramenti.  

Afrika Kusini:Makubaliano ya kutumia divai rasmi katika Misa kanda ya Afrika Kusini!

Kanda ya Baraza la Maaskofu wa Afrika Kusini(Afrika Kusini, Botswana na Swaziland)wamekubaliana kutumia divai rasmi katika maadhimisho ya liturujia.Divai hiyo inakidhi mahitaji ya kisheria ya kutumia wakati wa misa kwa mujibu Askofu Sithembele Sipuka,rais wa Baraza la Maaskofu Afrika Kusini.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Maaskofu  wa nchi ya Afrika Kusini, Botswaa na Swaziland wamekubaliana kuhusu divai rasimi ya kutumia kwa ajili ya maadhimisho ya kilitutujia na ambayo inaaelekezwa kama “Southern African Catholic Bishops Conference Mass Wine” yaani  Divai ya Misa ya Mababaraza ya Maaskofu wa Afrika Kusini”. Habari hiyo iliripotiwa kwenye wavuti wa Baraza la Maaskofu wa Afrika Kusini. Kama inavyooneshwa kwenye lebo, kwamba divai hiyo inakidhi mahitaji ya kisheria ya kutumiwa wakati wa Misa.

Kwa mujibu wa maelezo ya Askofu  Sithembele Sipuka, rais wa Baraza la Maaskofu Afrika Kusini  anasema “Sherehe ya Ekaristi inautambulisho muhimu wa pamoja kwa  Wakatoliki, na mara nyingi huadhimishwa katika kumbukumbu ya shughuli za Yesu Kristo kwa njia ya ili kuokoa  na ni kielelezo cha umoja wa Kanisa, na kwa sababu hiyo kila askofu analo jukumu, katika jimbo analoliongoza,kuhakikisha kuwa njia ambayo Ekaristi inaadhimishwa inaambatana na kanuni zilizowekwa na kanisa katika ulimwengu,na  ambazo ni pamoja na vitu vinavyotumika kuadhimisha Ekaristi, ambayo ni mkate na divai”.

Tangu ilipoundwa Kanda ya Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika ya Kusini inayounganisha ( Afrika Kusini, Botswana na Swaziland) imeonesha hatua muhimu sana kati yao na kila Askofu katika jimbo lake amechukua jukumu la kuhakikisha kuwa divai na mkate katika adhimisho la Ekaristi vinakidhi mahitaji ya kisheria. Wakati uwajibikaji huo bado uko mikononi mwa kila askofu, maaskofu kwa mara ya kwanza wamekubaliana juu ya divai ya kutumia pamoja na  ambayo inawezekana  kutumika katika eneo lote.

16 October 2020, 12:05