Tafuta

Kiongozi wa Kazi Uingereza na Wales amekutana na wahudumu wa shughuli za upendo na watu wa kujitolea wanaosaidia wakimbimbizi huko Dover. Kiongozi wa Kazi Uingereza na Wales amekutana na wahudumu wa shughuli za upendo na watu wa kujitolea wanaosaidia wakimbimbizi huko Dover. 

Uingereza:AskofuMcAleenan akutana na wahudumu wa Upendo na watu kujitolea!

Askofu McAleenan mhusika wa kitengo cha wahamiaji na wakimbizi nchini Uingereza na Wales amekutana na wahudumu wa shughuli za upendo na watu wa kujitolea wanaosaidia wakimbimbizi huko Dover.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Askofu McAleenan mhusika wa kitengo cha wahamiaji na wakimbizi nchini Uingereza na Wales amekutana na wahudumu wa shughuli za upendo na watu wa kujitolea wanaosaidia wakimbimbizi na wahamiaji  kwenye michakato yao  huko Dover. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Tovuti ya Baraza la Maaskofu  ni kwamba kuwa tarehe 15 Septemba aliongoza Misa ya siku kuu ya  Mama  Yetu wa Mateso Maria ambaye  alikuwa chini ya Msalaba wakati mwanae  anakufa, kwa mujibu wa askofu Paul McAleenan na kuongeza kwamba Msalaba wa Yesu na Mama wa Mateso vyote  vinakwenda pamoja. Huko Dover imekuwa jambo zuri na la kujenga kwa kukutana na wale ambao kama Maria wanaungana na wakimbizi na wameamua kuwasaidia, kuzungumza nao kwa jina lake na kuwasaidia michakato yao ya kupata mahali pa usalama.

Askofu aidha alikutana na watu wengine wengi ambao wamezungumza kwa namna ya kushangaza kuhusu kazi yao na nia zao za kuendelea kueneza  ujumbe ambao ni wa lazima sana kwa ajili ya kuwasaidia wahamiaji na wakimbizi. Kwa njia ya kazi yao, pia alikutana na wakimbizi ambao waligundua ukweli na sasa ni wana wa Mungu, kwa maana wote ni ndugu kaka na dada wa Yesu amesema Askofu.

Kwa kuendelea  anaomba waamini kuwa “Tusali kwa ajili ya watu wa kujitolea ambao wanafanya kazi kwa ajili ya awakimbizi hapa na katika sehemu za Dover na Kaskazini ya Ufaransa na kwa ajili ya wale ambao wanakwenda kutoa msaada kwa watu wale wanaojikuta wako hatarini. Tusali kwa ajili ya wanaosadia na watoa maoni. Maombi haya tuyafanye kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo aliyefungulia mikono yake Petro ndani ya bahari la Galilaya na kutupatia utashi wa kufanya zaidi katika fukwe zetu za Kiingereza” amehimitimisha Askofu McAleenan, huku akikumbusha  Siku ya tarehe 27 Septemba  ilivyo Siku ya Kuombea Wahamiaji na Wakimbizi Ulimwenguni.

19 September 2020, 16:57