Uingereza:Ungereza yaongoza katika rekodi ya utoaji mimba
Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican
Huzuni kubwa na majuto ndiyo maoni yaliyotolewa na viongozi wa Baraza la Maaskofu wa Uingereza na Wales kupitia tovuti yao, kuhusu idadi kubwa ya utoaji mimba ulioneshwa kwenye ripoti Uingereza. Kwa mujibu wa takwimu iliyochapishwa Juni iliyopita na Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii, utoaji mimba ni 109,836 uliofanywa kwa wakazi wa Uingereza na Weles katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, ambayo inajumuisha kipindi kutoka tarehe 1 Januari, hadi tarehe 30 Juni 2020 ikiwa na ongezeko zaidi ya utoaji mimba elfu nne ukilinganishwa na kipindi kama hicho cha mwaka jana 2019.
Inasikitisha sana kwamba akina mama wengi wamehisi hawawezi kuendelea na ujauzito wao wanasema maaskofu , na ni matarajio yao kwamba wanaweza kupata msaada wa kweli wanaohitaji kupata watoto, bila kujali hali zao,.
Takwimu hiyo ni ya juu zaidi kuwahi kutokea nchini Uingereza, ambapo utoaji mimba umekuwa halali tangu 1967. Kwa mujibu wa taasisi ya Iona, ambayo inahamasisha jukumu la familia katika jamii imefafanua kwamba utafiti huo ni wa kushangaza kwani inamaanisha kila watoto watatu wanaozaliwa, mtoto mmoja hutolewa mimba.